Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Shida ni kwamba mkisikia mtu anauza mkaa mnatengeneza picha ya sehemu chafu chafuuu..

Mtu anauza sabuni mnatengeneza picha za namna hiyo hiyo,na sababu ni kwamba watu wengi biashara hamtaki kuwa wabunifu.

Uchafu Uchafu biashara za hivyo ni kwa wale wajasiriamali wa zamani sio wajasiriamali sisi tuliobahatika kupata vi elimu kidogo.

Jitofautishe muuza mkaa mwenye bachelor ya Account na Muuza mkaa wa darasa la saba Biashara zao ni sawa lakini muonekano ni tofauti.

Nafanya biashara local sana ila ukibahatika kuona 1 ya ofisi zangu utajua nini maana ya kuwa mjasiriamali aliepita darasani kidogo.
 
Huwezi kuuza mkaa na ukawa msafi hata kama una Phd achana na bachelor labda usiwe mkaa huu wa kuchoma miti.
Nimekwambia hapo juu labda hizi biashara ziwe mbali mbali lakini sio sehemu moja
Any way tukubali kutokubaliana ki mitazamo.
 
Nafanya biashara local sana ila ukibahatika kuona 1 ya ofisi zangu utajua nini maana ya kuwa mjasiriamali aliepita darasani kidogo.
Ulichoandika hapa kinapingana na ulichoandika siku zilizopita huko nyuma.

ukisema Office iwe local local sio classic ili
*Yasivute ma TRA nk
*Usiogopeshe wateja
 

Mabeberu walishaacha kutumia hizi akili za miaka 1935 ndio maana unakuta kiwanda cha kutengeneza magari wananunua betri sehemu nyingine,funguo sehemu nyingine na tairi sehemu nyingine!jinsi ya kutumia akili ndio tunatofautiana
 
Ulichoandika hapa kinapingana na ulichoandika siku zilizopita huko nyuma.

ukisema Office iwe local local sio classic ili
*Yasivute ma TRA nk
*Usiogopeshe wateja
umeelewa nini nilivyoandika pale juu? kuna mahali umeona nimefanya vitu vya kumuita TRA??

Unajua ili TRA atamani kuingia ofisi yako kukagua anaangalia nini anapopita nnje ya ofisi yako?

Unaweza niambia ktk hiyo sentensi wapi nimeandika biashara zangu zinatisha wateja?
 
Reactions: apk
Huwezi kuuza mkaa na ukawa msafi hata kama una Phd achana na bachelor labda usiwe mkaa huu wa kuchoma miti.
Nimekwambia hapo juu labda hizi biashara ziwe mbali mbali lakini sio sehemu moja
Any way tukubali kutokubaliana ki mitazamo.
sawa,nimekubali kutokubaliana na wewe.
 
Dah aiseee huku ndo kuwaza nje ya box...shukran sana mkuu kwa madini haya hakika nimejifunza sana..kwel elimu haina mwisho..asante kwa darasa hili la bure kabisa
 
CONTROLA fungua blog ya hizi mambo ni elimu kubwa sana unatoa juu ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla zikae humo tuwe tunavisit madarasa hayo
 
Mkuu hii tunaifanya kwenye biashara kubwa.
Fikiria kila mmoja akiwa na wazo kama hili....hivyo viazi utakula mwenyewe.
Biashara ni kugawana riziki.

Kwenye chips
Mkaa ukachome
Mafuta ukalime alizeti
Chumv ufuate baharini
Mayai ufuge kuku
Maji ukinge ya mvua
Pilipili..carot...nyanya... Navyo ukalime

Uone kama maisha yataenda.

Au twende na hii.
Una mtaji mdogo then unafuata viaz gunia ili usev 6,000 hapo kuna usafiri...ubebaji mzigo....kuli....

Hata sijui naandika nn
 
Nakuomba kwa faida ya wengine utuwekee tofauti kati ya (1)machinga
(2)mjasiriamali
(3)mwekezaji
(4)mfanyabiashara
(5)mchuuzi.
 
Unapoamua kufanya biashara shart la kwanza ni kujitofautisha na wengine na usfikiri wote watafanya unachofanya.
 
Mawazo mazuri ya mtu umeyajibu ovyo kabisa...idea ya jamaa ni nzuri kama wataka kufanya biashara na yenye tija na kuikuza bhc ushaur wake ni mzuri .matumiz kwenye biashara ndio jambo kubwa xnaa ..afu mwishobwa siku unafanya biashara kwa ajili yako na familia yako mambo ya riziki kugawana hio sio kazi yako kugawa riziki
 
Wap
Huwez kufanya kila kitu pekee yako
Kwann ushindwe sasa kama huezi c ukae home tuh ...unaenda fanya biashara upate faida ukijiongeza unapata faida mara mbili ...na ukisema riziki kugawana huoni kama ukifungua biashara nyingi itabid uajiri watu wengi ...hapo hamjagawana hio riziki
 
Mimi Naomba msaada nawezaje kupata post zako kwa wakati Maana hii toka umeiweka alhamis ndo naiona leo CONTROLA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…