Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Mimi Naomba msaada nawezaje kupata post zako kwa wakati Maana hii toka umeiweka alhamis ndo naiona leo CONTROLA
Namfatiliaga sana sana huyu kaka,mwanzo nlikua kama wewe ila nilipo m follow nikawa sipitwi na nyuzi zake nahisi ndio njia nzuri yakupata mada za mtu humu JF.
 
Namfatiliaga xana xana huyu kaka,mwanzo nlikua kama wewe ila nilipo m follow nikawa sipitwi na nyuzi zake nahisi ndio njia nzuri yakupata mada za mtu humu JF.
Nimesha mfollow lakni simpati kwa wakati sijui kuna mkono wa mtu!?
 

🤣🤣🤣
 
Nimesha mfollow lakni simpati kwa wakati sijui kuna mkono wa mtu!?
Hapo sasa sijui kwanini au nenda setting sehemu ya allert na notification nahsi kule unaweza kuset set japo sina uhakika xannaaa
 
Tatizo la wajasiriamali wengi, wanafanya biashara ilituu wapate basic needs hawaangalii 10 miles extra, katika kazi yao, ndio maana ya kusema biashara flani hailipi. Mimi ninachoamini every business it pays chamsingi piga hesabu uitafute break even point... hapo ndipo mtihani kwa wengine....
 
Uzi upo poa lakini kuandika na kuongea vipo tofauti na field huko mkuu.
 
Sijui hata nisemeje, yaani mkuu hichi ulichoandika hapa kina umuhimu mkubwa mkubwa sana ni vile tu baadhi ya wachangiaji wanachelewa kukupata. Hii principle ulioizungumza hapa umeweza kweli kweli kuiweka kwny local environment labda tuipeleke kwny large scale kidogo wataelewa.

Hii principal ulioiandika hapa ndo Elon Musk aliyoitumia kuunda kampuni yake ya Space X. Wakat anaingia kwny game alikuta rockets za kwenda anga za mbali na sayari nyingne bei ilikua kubwa sana. Na katika kuchunguza akagundua kua sababu ni kua parts mbali mbali zinazotumika kuunda hizo rockets znatengenezwa na makampuni tofauti tofaut na kisha znakua assembled together hivyo kufanya bei ya rockets kua kubwa.

Basi mwamba alichoamua kufanya ni ku draw a list ya parts tofauti tofauti znazounda rocket na kuamua kuzitengeneza yeye mwenyewe na kisha kuzi assemble yeye mwenyewe lengo ni kupunguza cost na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na rockets za kampuni ya Space X zinauzwa kwa bei nafuu. Kwa wale wafuatiliaji wa masuala ya anga za mbali na sayari nyingne wanajua ndo maana hata idea ya "re-usable" rockets imekuja sabab lengo ni kupunguza cost ili kufanya biashara ya kwenda sayar nyinginezo kua affordable.

Back to the topic I believe kwa concept ile ile leo hii Elon Musk angekua anauza chipsi angefanya kama mkuu wangu CONTROLA alivyoandka hapo juu key principle ni kwamba huwezi kua mjasiriamali mzuri usipojua how to minimize the cost of production as far as u can. Level of profit it depends on ur ability to minimize the cost of production.
 
Mkuu hawa raia ukiwapa mifano mikubwa hivyo ndio utawachanganya kabisaaa yani watasema unatupa habari za ma rocket wakati sisi tunauza mkaaa, huoni wanalalamika kila siku kwanini serikali inanunua ndege wakati mkulima hata bus tu hajawahi panda?

Wanasema ndege hazina faida wala hazina msaada wowote kwa muuza karanga,sasa ukija na mifano ya namna hyo watakuelewa wachache sana ila wengi utawaacha nyuma..ila naamini kwakua ktk 100 hakosekani walau mmoja ataenielewa basi huwa namshukuru Mungu kwa kuokoa walau maisha ya mjasiriamali mmoja mahali flani.

Si lazima nieleweke na kila mtu natamani walau kila thread yangu ipate mtu 1 tu ila ikitokea wakapatkana wengi wakaelewa nafurahi na wakibeza na kujifanya hawaelewi pia nafurahi maana tumetofautiana kimaisha.
 
Nimeliona mapema hili kama kila mtu atalinda pesa yake kwa mtindo huu maendeleo sahau.

Huo uchumi wamakaratasini mtaani haupo
 
Mabeberu walishaacha kutumia hizi akili za miaka 1935 ndio maana unakuta kiwanda cha kutengeneza magari wananunua betri sehemu nyingine,funguo sehemu nyingine na tairi sehemu nyingine!jinsi ya kutumia akili ndio tunatofautiana
Hivi ndivyo maisha yanavyotaka hatakama unamudu vyote inakulazimu uchangie wenzio ili na wewe uchangiwe.

Unamkataa msukuma mkokoteni asikubebee nyanya zako wakati huohuo ndo unamtegemea aje anunue nyanya gengeni kwako.
 
You are right.... mie nauza kiduka cha mangi na mteja wa kwanza ni mimi mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…