Fanya biashara ndani ya biashara yako, uokoe pesa unazopoteza na ujiongezee faida

Hivi ndivyo maisha yanavyotaka hatakama unamudu vyote inakulazimu uchangie wenzio ili na wewe uchangiwe.

Unamkataa msukuma mkokoteni asikubebee nyanya zako wakati huohuo ndo unamtegemea aje anunue nyanya gengeni kwako.
Fact
 
Hapa nimepaelewa mnoooo. Ngoja niendelee kusoma. Asante sana mkuu
 
Nimekuelewa sana controla..hii ni aina ya biashara ambayo ni changa ama yenye mtaji mdogo ama kubwa lakini ushindani ni mkubwa.biashara hizi pia hufanywa sana na wahindi na waarabu...ninao mfano tosha wa boss wangu wa zamani
 
Tujifunze kugawana riziki jamani,kila mtu akifanya hivyo biashara na riziki za watu zitapotea
 
Tujifunze kugawana riziki jamani,kila mtu akifanya hivyo biashara na riziki za watu zitapotea
Riziki ya kila mtu ipo katika juhudi zake kuitafuta,mtu mwingine hawezi ziba au zuia wewe usipate riziki yako.
 
Tujifunze kugawana riziki jamani,kila mtu akifanya hivyo biashara na riziki za watu zitapotea
Ukienda masokoni kila.mtu anauza nyanya meza ya kwanza mpaka ya 10 wote wauza nyanya ukiingia unakaribishwa wengine mpk na shati wanakuvuta..

lakini wale wafanyabiashara wote jioni kila mtu anaondoka na kidogo Mungu alichomjalia.

Uwepo wao kwa wingi haumzuii mtu kupata riziki yake, riziki kama ipo ipo tu hakuna wakuizuia riziki yako.

Weka Juhudi katika utafutaji wako na Riziki yako utaipata tu hakunaga binadamu anaeweza fanya binadamu mwenzake akakosa riziki aliyopangiwa na Mungu,hayupo na hatatokea.
 
Mwisho utatuambia tufuge kuku wenyewe ili tuwe tunapata mayai yakukaangia chips
Ngoja nikusapoti katika hamna mana jamaa kaja na idea nzuri we unaenda mbali. Mwisho utage mwenyewe ili uwe na almost zero costs za uendeshaji.
 
Boss nakuita tena boss mbona katoa mifano rahisi tu mnaenda mbali mf Kama una salon nunua powder cartoon ujiuzie Ila ukipata mteja muuzie maana faida ni kusevu gharama but to every general rule there is an exception
Wamiliki wa sheli nao unashauri wakamiliki visima vya mafuta uarabuni siyo? Maisha hayako hivyo mkuu
 
Maisha yanajibalance yenyewe wako watakao ona sawa wakafanya, wako ambao hawatafanya, wako watakao fanya ivyo wakashindwa. Naomba nkuakikishie hakuna mtu anaetaka kugawana na mtu riziki, ni kwamba watu hatuna uwezo wa kufanya yote hayo effectively, ila kila mtu akipata namna ya kupata pesa anaitumia kama anaweza. Sijui ntabania wengine ridhiki io ni defensive mechanism ya kushindwa kufanya kitu. mgawa riziki ni MUNGU
 
Mabeberu walishaacha kutumia hizi akili za miaka 1935 ndio maana unakuta kiwanda cha kutengeneza magari wananunua betri sehemu nyingine,funguo sehemu nyingine na tairi sehemu nyingine!jinsi ya kutumia akili ndio tunatofautiana
Aga Khani anamiliki hospitali ya Aga Khan DSM, anamiliki magazeti ya mwananchi communication, anamiliki serena hotel, anamiliki jubilee insurance, anamiliki PWC auditing firm, anamiliki standard chartered bank.
Makampuni yote yanapeleka matangazo mwananchi, yote yanakaguliwa na PWC, yote Wageni wao eg wakileta ma-consultants wanalala serena, yote wafanyakazi wanakopa standard chartered, bima za magari yote ya ofisi pamoja na bima za matibabu ya wafanyakazi wanakatiwa jubilee insurance
 
Asante sana!
Moja kati ya thread bora sana ambazo kwa hakika zinaongeza maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…