Somo zuri sana ila sasa ndugu yangu controla umekosea hapo padogo sasa kama ukitaka malighafi nazo uuze mwenyewe je maduka ya wenzako nayo si yatafungwa? hujua tunainuana kwa kila kitu ?
je mwinuko wa uchumi kwa mwingine utapandaje kama sio kuinuana kwa bidhaa tufanyazo?
Sio kila mtu atafanya hivyo,wewe ukifanya kuna wengine hawatofanya
Ninachojaribu kusema ni kwamba "kuwa watofauti" darasani kuna wanafunzi 100
ila wanaotoka na GPA za kueleweka wanahesabika,wanaotoka na Div 1 wanahesabika
wewe kuuza haina maana wengine wasiuze,mimi nitauza vitu vya ndani ya biashara yangu
wewe utauza vitu vya ndani ya biashara yako,nina duka langu la Nguo "siwezi kuuza mkaa"
oviously mkaa nitakuja kuku ungisha tu hata iweje, Nauza zangu Magari Siwezi Uza Chakula
vyovyote vile lazima ntakuja canteen kwako kula, Hata uuze kila kitu bado kuna vitu hutouza
hivyo naendelea na nakazia hakikisha unafanya Biashara ndani ya Biashara Yako Uokoe pesa
unazopoteza na ujiongezee Faida,hiyo ndio siri ya kufanikiwa kama mfanyabiashara na mjasiriamali.