Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Kukaa karibu na dereva unachosha akili yako maana kila muda miguu yako inafunga break
Hiyo ndio seat Mimi naenjoy na hasa kuondoka na na uchovu maana hizo seat za kwanza za mbele unanyoosha miguu kabisa, haufiki destination yako na uchovu sana.
 
Ni heri LATRA waje na kanuni ili abiria wawe wanavaa helmet kwenye mabasi.

BTW:Kuna jamaa aliwahi nisimulia mkasa wa ajali aliyopata miaka ya 2000,Mohamed Trans iliacha njia ikiwa mafuta.

Enzi hizo Shy-Mza gari nyingi zinapitia Old Shinyanga siyo Maganzo barabara ilikuwa vumbi bado.

Viti vingi viling'oka na wasiokuwa wamefunga mikanda wengine walitokea kwenye kioo cha mbele maana basi lilipiga tuta la jaruba likaanza ku-roll.
 
Umetukosea sana vibonge mkuu, kuingia chini ya siti na kujiviringisha kuwa wadogo kama mpira?
 
Umeandika porojo tupu, ukiweka mwili huko chini utajigonga gonga na kuumia kichwa sana na kuna uwezekano mkubwa kuvunjika vibaya.

Cha msingi ni kufunga mkanda ili ajali inapotokea uweze kutulia hapo hapo mengine ni mipango ya Mungu tu.

Alafu pia ajali inapotokea huwa ni kitendo cha dakika au sekunde chache huwezi kujificha huko unakosema.
 
Ukisikia pah fahamu lisasi imekukosa kwa sababu sipidi yake ni sawa na sipidi ya umeme,gali linaweza kuanza kuyumba likaanguka umbali mita 200 mwendo wake wakati huo mwendo wake huwezi jisaidia na chochote kufumba na kufumbua hiko miguu juu kichwa chini
 
Mimi mama yangu alipata ajali ya gari miaka ya nyuma ila Mungu mkubwa alipona na aliumia kidogo sana alichanwa na kioo juu ya jicho.

Anasema jirani yake kwenye siti alikufa,watu wengi walikufa kutokana na kutaka kujiokoa.

Gari ilikua inapanda mlima sekenke ika fail ikaanza kurudi kinyume kwa kasi sana na break zilifail sasa watu baadhi wakaanza kutaka kujiokoa kwa kuruka na wengine wakiwa kwenye harakati hizo. Ile gari ilienda kuanguka kwenye korongo refu, mama yeye alisema alivoona vile alikaa pale pale kwenye seat yake akiwa amefunga mkanda ila watu wengi walifungua mikanda wakataka kuanza kujiokoa na wengi walikufa na kupata majeraha makubwa.

Baada ya ajali walipelekwa hospital mkoa wa singida, mama aliruhusiwa siku ya pili tu ila wengi walikufa kwa kutaka kujiokoa
 
kama ajali ingekuwa predictable kiasi cha kukufanya uweze kujiandaa, sidhani kama tungekuwa tunashuhudia vifo. Ajali hutokea ndani ya sekunde tuu na hakuna kitu unaweza fanya, kikubwa SALI, SALI, SALI SANA, funga mkanda, FUNGA MKANDA KISHA SALI Mungu akufikishe salama na kukulinda ktk saa ya ajali.

Ajali haina maandalizi
 
Kwenye ndege ile brace brace lengo sio kufungua mkanda ni kuinama ili usiumie zaidi
Lengo sio kufungua mkanda hata kwenye misukosuko ya ajali za magari, lengo ni kuinama kupunguza surface ya mwili ili kupunguza impact. Kwa nini mara nyingi watoto hawadhuriki kwenye hizi ajali?(usijesema ni malaika)
 
Mimi nilipona kwa mbinu hii,gari ilikuwa 90.

lbda ajali ikukute tu umesinzia au unachati....lakini mimi huwa na tabia mda wote macho yapo kodo kwa dereva na barabara na huwa nakaa siti za katikati ili nione vizuri
Kwahiyo unadhani kilichokuokoa usife ni uko kua macho kodo na kujificha?.ndugu kikija kinakuja.haijalishi utakua wapi na utasali kwa kiwango gani.Ukitoka mzima usifikiri ni jitihada zako.jua siku yako bado sio zaidi ya hapo.
 
Nishawah pinduka na bus asee Mungu tu yan hakuna mda huo ni just a matter of two seconds vilio tu mtu upo siti ya nyuma unajikuta mbele huko....


Lakin dah kuna wale jamaa wezi sijui wanatoka wapi wanakomba kila kitu.
 
Before ajali “mungu nakuomba utufikishe salama”

Baada ya ajali “Namshukuru mungu nimepona”

Unamuombaje akulinde safarini halafu unakuja kumshukuru ajali ikitokea?

Nielewesheni
 
Sasa usiombe ianguke halafu iripuke hapo ndo utajua hujui ukiwa chini ya siti
 
Abiria wa kwenye gari lilipata ajali wengi ni waongo. Yumkini husimulia waliyopata kusimuliwa na mashuhuda ama hujitungia stori zao za uongo na kweli.
 
Physics inakataa theory yako. Huwezi kumbatia sababu gari litaruka na wewe utapaa juu ukishuka chini hutakiona hiko koti
Nishawahi fanya hivo wazee wa fursa wa kwenda Minandani Lilipinduka basi karibia na stendi ya Itigi nilikuwa naelekeaTula Tabora mnadani mpira wa mbele ulibasti buuuu mm nakiti changu nimekumbatia kiti hilo linakosa muelekeo mimi na kiti tu nimekumbatia kwa nguvu zote sjakaa sawa likala mueleka likalala linaburuzika mm nakiti tuu naskuumia zaidi yakuangiwa na mabegi mkuu nasema tena kamata kiti[emoji2][emoji2][emoji23]
 
ENDELEENI KUBETI KWENYE MABASI
ENDELEENI KUWAHIMIZA MADEREVA
WAKIMBIZE
wabongo mtazidi kufa kama inzi na maajali,wabongo si wabishi hawasiki

Ova
 
Sijui kama umeishawahi kupata ajali kama hujawahi nikwambie TU kuwa walioko nje ndio hujua Nini kimetokea
Wewe akili itakurudia gari ikiwa imeshamaliza swala lake la kupinduka.

Muhimu funga mkanda Kisha muombe Mungu mfike salama
Sina maneno mengi zaidi ya kusema Asante Mungu aliniepushia kifo kwenye ajali ya gari Tena harrier baada ya kuipiga semi trailer kwa nyuma . What if it was head to head collision... Sasa hivi ningekuwa mavumbini futi sita nimetulia tuli peke yangu .[emoji58][emoji58]
 
Nakupongeza sana umejitahidi kuongea jambo zuri sana.

Lakini bahati mbaya ajali nyingi zaidi 95% ni sudden occasion ambapo huwez pata huo muda wa kurespond kwaajili ya kujikinga.
Ni kweli unalosema ila amini binadamu sometimes tuna kitu kinaitwa sixth sense au tumezoea kuita malaika mlinzi sijui. Hii inaweza kukuonyesha early warning au signs ila kama kawaida yetu sisi wanadamu tunapuuzia vitu vidogo vidogo sana na ndivyo vinavyotugharimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…