Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Umeandika vizuriii Sana tatizo kiwewe, presha, na hofu ya kifo wakati wa ajali! Hayo yoote huwezi kumbuka!
 
Mimi nilipona kwa mbinu hii,gari ilikuwa 90.

lbda ajali ikukute tu umesinzia au unachati....lakini mimi huwa na tabia mda wote macho yapo kodo kwa dereva na barabara na huwa nakaa siti za katikati ili nione vizuri
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]yaani unakodoa macho ili upate muda wa kushuhudia ajali na kuikwepa,basi ipo siku utashangaa tu umekodoa macho na hakuna ulichoambulia kuona zaidi ya mashuka ya hospitalini

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa, sijui kama ndio alikuwa macho zaidi ya wengine au la, maana basi lilipoanza kupata mushkeli, yeye pekee ndiye aliyechoropoka dirishani, bahati mbaya akaishia kulaliwa na basi na kupoteza maisha, hakuna mwingine yeyote aliyefariki.
Kwenye ajali kiherehere hakitakiwi kabisa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Picture this🙌: Umekaa ndani ya basi liitwalo X, siti namba X ,unaenda mkoa X kumsalimia X.

Mara ghafla unashtuka basi ulilomo linaanza kuyumba yumba kwa nguvu isivo kawaida na abiria wale viherehere akina mama mostly wameshaanza kupiga kelele za mamaaaa! (statistically speaking women more alert and pay more attention to the small changes in the details of their environment,than males among homo sapens) nini unatakiwa ufanye? Twende kazi👇

NB: Hii njia inafanya kazi kama umekaa kweny siti za katikati, yani ambayo haiko karibu na ukuta wa gari.... sio dirishani wala siti za nyuma kabisa au mbele kwa dereva) maana hizi ndio sehemu ambazo haziwezi kupata direct impact ya ajari, either kwa kugongwa na kitu au kugonga kitu.

Unachotakiwa kufanya ni kuinama haraka sana na kuingia ndani ya uvungu wa siti,na kuhakikisha unakificha kichwa ndani ya siti. Stay low as possible, stay small as possible. Yani hakikisha unapunguza suface area ya mwili wako haraka sana ili kupunguza area ambayo inaweza kuwa hit. Na kupunguza damage.

This will ensure that kuna very small chance gari linapobinuka utaruka nalo na kujibonda kichwani au kwenye sehemu nyeti.

Asilimia kubwa ya majeruhi wa ajali wanaofariki huwa na majeraha ya kichwa.
Hivyo unatakiwa upambane as best as you can kukilinda kichwa chako.

Mimi sio Mungu kwahyo sikuambii kuwa njia hii ina uhakika wa kukufanya upone na kukiponyoka kifo lwa 100%, la hasha! Mimi nachokuambia hii ni njia best ya kukupunguzia probability (uwezekano) ya wewe kuwa mmoja wa marehemu watakaotangazwa kwenye habari kesho yake.

Mtegemee Mungu, sali sana, sali kila saa. Sali kabla hujapanda gari, sali ukishuka gari, sali unapoamka, sali kila unapotoka unapoishi, sali kila kabla na baada ya kumaliza majukumu yako ya siku hiyo, sali kabla ya kurudi nyumbabi, sali ukifika nyumbani, sali kabla ya kulala, sali usingizini.

Kila usqlipo Ombea kwenda jannah/mbinguni na msamaha wa dhambi zako.
Kwa maana kifo muda wote kipo around the corner kikigonga hodi ya kimya kimya, usipokiwahi na kukibania mlango, utakuja kushtukia kimeshakuvamia ndani kimeshakuingilia na hautakuwa na uweZo wa kujitetea.

Siku zote popote stay sharp, always stay alert kama wanawake na always pray.

Kifo always kipo kwa nyuma kunakuvizia...Usipende kukutana nacho maana hutakishinda nguvu, Always kikwepe kabisa na ikiwezekana jifiche kisikuone.

Always tazama macho mbele, usitingishike maana kwa nyuma kuna kifo kinasema Geuka tukuone.

👇
Umewahi kupata ajali na ukafanya hayo na ukasalimika?ajali ni kitendo cha sekunde mbili tu
 
Kwenye suala kukaa katikati na kuepuka siti za dirishani hapo uko correct.
Tuache masihara takwimu ziko wazi wanaokufa hasa location zao ni za mbele na pembeni na wacgache nyumba ingawa ajali ya kugongwa nyuma kwa mabasi si rahisi
 
Sijui kama umeishawahi kupata ajali kama hujawahi nikwambie TU kuwa walioko nje ndio hujua Nini kimetokea
Wewe akili itakurudia gari ikiwa imeshamaliza swala lake la kupinduka.

Muhimu funga mkanda Kisha muombe Mungu mfike salama
Aaf akumbuke ajali ni kitendo cha chini ya sounded 30,,je akipewa muda huo anaweza kufanya hayo yote?
 
Ushauri wa hovyo sana huo.
Usalama wako ni kufunga mkanda tu
Hizi ni mbinu zipo worldwide mkuu, mkanda ni kitu cha lazima ila haya anayoongea hata kwenye ndege(nasikia) wanatoa ushauri wa namna hii ili kupunguza impact.
 
Nilishawahi kupinduka na gari,nilitoka salama ILa nimwambie tuu kuwa agali hutokea ghafla sana hutopata muda ya kufanya hayo maamuzi mkuu,hao wanaokufa Kwa ajali sio kuwa wanapenda.kufa unaweza kufa hata watu wakikuangukia wakati wanakukuruka,baada ya ajali watu wanarukwa na akili jitahidi usikae karibu na mtu ,hasa wanawake akikukaba shingoni hakuachii au kama bonge akikuangukia kaxi unayo,
Kumbuka tuu alipokuwepo yule ,aliyeondoka tulisahau mambo ya ajali ajali ila Sasa hivi tunarudi kule kule.
Ukiona dereva anakimbia sana mkemee usishabikie kuwa utawahi kufika
Pia hizi ajali ni matokeo ya rushwa barabarani,gari ikisimamishwa mtu anapewa buku mbili Wala hakuna kuadhibiwa,no body cares
Hakuna mtu anatetea maisha yetu ndiyo maana haya yote yanatokea,no body cares ila ninaomba sana Mungu awalipe hizo damu ambazo hazina hatia zinazopotea Bure,nafikiri hao makamanda ifike wakati ajali zikitokea tatu kwenye eneo lake wapishe wengine kwenye hizo nafasi,wewe upo unalipo mshahara Kwa Kodi zetu lakini Kwa uzembe wako unashindwa kuwajibika watu wanakufa
 
.......Unachotakiwa kufanya ni kuinama haraka sana na kuingia ndani ya uvungu wa siti,na kuhakikisha unakificha kichwa ndani ya siti...........sio magari yote waweza ingia uvunguni

1. Funga mkanda
2. Kwa imani yako ombea safari mwanzo to mwisho
3. Usisinzie sana kwa gari (stay alert)
4. Salimia majirani ulokaa nao (sijasema kupiga stori, sio wote wapendao - ila salamu sio mbaya)
5. Usishangilie mwendo wa gari ama dereva anavyo overtake magari mengi
6. Usafiripo hakikisha nduzu yako wa karibu ana taarifa
 
ilo ajalo ni slow motion au,? lumbe hujui maana ya chombo cha moto,? usha panda bus linalo overtake one two!? ile body unaisikiaje ? muereka wake ukitokea ni chap kidogo watu wako ahera madukani
 
Back
Top Bottom