Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Mimi nilipona kwa mbinu hii,gari ilikuwa 90.

lbda ajali ikukute tu umesinzia au unachati....lakini mimi huwa na tabia mda wote macho yapo kodo kwa dereva na barabara na huwa nakaa siti za katikati ili nione vizuri
Bro uzi wako ni wa maana sana watu wanachukulia simple tu, Anyway tahadhari ni muhimu sana siku zote na ulichokifanya hapa ni kutoa tahadhari nini mtu afanye when there's a chance to do but when there's no chance no problems coz ulikuwa unajua nn cha kufanya lakini hukupata chance ya kujiokoa!.

Tatizo linakuja kwamba hata watu wenyewe wanapo give up kwamba hakuna chance yeyote ya kufanya hivyo hali ya kuwa wanajua kwamba kuna Ajali zingine hupitia stage kadhaa kabla ya Ajali yenyewe kutokea, I think kwa Ajali za Aina hii hizi Protective Measures zinafit kabisa.

All in all Dua na Maombi ni Muhimu sana katika kufanikisha hili ingawa pia kuna wakati muda ukiwadia basi ni lazima tu uchukuliwe kwani Ajali hiyo inakuwa ni SABABU tu lakini siku na saa yako ikitimia ndio COURSE ya wewe kuchukuliwa inapokuwepo Ingawa wanasayansi hawataki kabisa kukubali hichi kitu but myself I do believe on that. NO EXCUSE WHEN YOUR TIME COMES.
 
Kama hujafunga mkanda kumbatia kiti mwanawane nasema tena kumbatia kiti kwa mikono yote usiachie kama unavokumbatia baby wako utakuja kunishukuru baadae. Wazee wakukesha safarini tunalijua hilo na limewaokoa wengi.
Physics inakataa theory yako. Huwezi kumbatia sababu gari litaruka na wewe utapaa juu ukishuka chini hutakiona hiko koti
 
Unasema kana kwamba ni kwenye ndege mnaambiwa fungeni mikanda oops hali ya hewa ni mbaya ,

Kwenye bus hujui kitu ujikute hosp au Mbinguni au Mungu akuokoe.

Ajali ni mbaya
 
Ukipiga mzinga utajikuta MOI pale km uko Dar, mkoa utaletwa pale baada ya siku kadhaa.
Panda ndege au treni ufike salama.
Hivi vipepeo (yutong) vinawamwaga saa yoyote.
Sasa wewe useme utakaa uvungu wa siti toka Moro mpk Mbeya eti unalinda kichwa
si ughairi safari tu.
Huna hela kaa nyumbani.
New force video picha zipo hapa.
Limedondoka kichwa chini miguu juu.
Fikiria we upo hapo chini ya kiti.
Dah acha tu ni balaa
 
Mi nimekuelewa mbinu yako niliitumia pale IYOVI mbinu yako inatumika kwa watu wenye roho kubwa yaani sio warahisi kupanic kama mimi
 
Bro uzi wako ni wa maana sana watu wanachukulia simple tu, Anyway tahadhari ni muhimu sana siku zote na ulichokifanya hapa ni kutoa tahadhari nini mtu afanye when there's a chance to do but when there's no chance no problems coz ulikuwa unajua nn cha kufanya lakini hukupata chance ya kujiokoa!.

Tatizo linakuja kwamba hata watu wenyewe wanapo give up kwamba hakuna chance yeyote ya kufanya hivyo hali ya kuwa wanajua kwamba kuna Ajali zingine hupitia stage kadhaa kabla ya Ajali yenyewe kutokea, I think kwa Ajali za Aina hii hizi Protective Measures zinafit kabisa.

All in all Dua na Maombi ni Muhimu sana katika kufanikisha hili ingawa pia kuna wakati muda ukiwadia basi ni lazima tu uchukuliwe kwani Ajali hiyo inakuwa ni SABABU tu lakini siku na saa yako ikitimia ndio COURSE ya wewe kuchukuliwa inapokuwepo Ingawa wanasayansi hawataki kabisa kukubali hichi kitu but myself I do believe on that. NO EXCUSE WHEN YOUR TIME COMES.
Bangi hizi mnazovuta na begu zake hizi...
 
Raha ya ajali ufe
Kabisa,
Yale mateso ya pale kibasila ward ni zaidi ya ajali.
Doctor mmoja mshenzi yule alafu kuna fundi seremala anatengeneza magongo enzi hizo boda hizi zimeanza anza.
Kumbe wana deal lao.
Unakatwa mguu fundi anakutengenezea magongo.
Bill ilikua elfu 70.
Ndugu zako watalipa.
Watu tungekua vilema sa hii
Mungu Saidia nilikurupuka namkuta huyo jamaa wa magongo anapima urefu wa mguu.
Wakakate
wanipe magongo..
Huku mguu umeteguka tu kwenye gari.
Alikula kofi hatasahau.
Nikakimbia hadi reception kuwaambia wanataka kukata mguu wangu mzima.
Aisee watu ni wanyama.
Hao vijana wa boda kibao wamechinjwa miguu hapo.
Kumbe ni biashara.
Leo ni vilema maskini.
 
Ubaya tendo la ajali ni la haraka sana kiasi spidi ya ubongo kuchakata hadi kufanya maamuzi sahihi inakuwa ngumu labda zile ajali unaona kabisa dereva anafanya jitihada za kujiokoa au zile ajali ambazo unakuwa umekaa mbele unapoweza kuangalia mwenendo wa basi na reaction ya dereva.
 
Mkuu hujawahi kupata ajali

Ni tukio linalotokea within a second na wala ubongo hauwezi kuchakata nini cha kufanya
 
Kuna wale tunaosafiri na mziki masikioni hadi uje ushtukie tukio basi lishapita.
Nimewaza basi kila mtu akiingia uvunguni watu watatosha?
Hata hivyo hii hatafanya kila mtu so atakayeona inamfaa siku akifikiwa aitumie
 
Huo muda wa kuficha kichwa chini ya siti utaupata sasa? Si unapanic tu....labda ungeshauri tuvae helmet na kufunga mikanda
 
Ni tukio la ghafla sana. Nafasi ya kufanya mipango ikafanikiwa ni ndogo kama nafasi ya mtu mwenye tumbo kali la kuhara akatoa hewa chafu bila kujiharishia.

Kama ilikutokea ni kushukuru MUNGU tu maana mara nyingi si kwa ujuzi wako. Kuna watu wanapona ajali ukiitazama gari unajiuliza kaponaje huyu?
 
Back
Top Bottom