Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Wiki juzi nilipata ajari na wakati inatokea sikuwa naamini kama inawezekana na sikuwa nafikiria kuumia au kufariki. Nilitulia kawaida kabisa sikufanya ujanja wala kupiga kelele. Nashukuru Mungu nilitoka salama bila kuumia ila maumivu ya uti wa mgongo kwa mbali maana tulipinduka.

Huwa naamini ukitaka kuongeza chances za kutoumia wewe tulia kabisa. Ukianza movements za kuama seat na kulala chini sijui hapo unakunja mwili na unaweza banwa kwenye harakati hizo au ukarushwa.

Watoto wengi huwa hawafi kwenye ajari sababu hawana panic wala ujanja ujanja na wana miili midogo.
 
Labda hilo gari ulilopanda liwe linasukumwa yaani libovu.
Ati uingie chini ya seat ajali ni sekunde tu kila kitu kinabaki history.
 
hio ajali ni slow motion
Sijui hata utafanya hayo saa ngapi.
Hilo Bus linatoka hapo Ubungo full mbio kwenda Mbeya au Mwanza. Mbeya, Tunduma Swanga kuja Dar hizo ndo kabisaa, ni gia kwa gia uombe tu dereva hajalewa usiku.
Vinginevyo mnajikuta mtaroni au bondeni huko.
 
Sijui kama umeishawahi kupata ajali kama hujawahi nikwambie TU kuwa walioko nje ndio hujua Nini kimetokea
Wewe akili itakurudia gari ikiwa imeshamaliza swala lake la kupinduka.

Muhimu funga mkanda Kisha muombe Mungu mfike salama
Ukipiga mzinga utajikuta MOI pale km uko Dar, mkoa utaletwa pale baada ya siku kadhaa.
Panda ndege au treni ufike salama.
Hivi vipepeo (yutong) vinawamwaga saa yoyote.
Sasa wewe useme utakaa uvungu wa siti toka Moro mpk Mbeya eti unalinda kichwa
si ughairi safari tu.
Huna hela kaa nyumbani.
New force video picha zipo hapa.
Limedondoka kichwa chini miguu juu.
Fikiria we upo hapo chini ya kiti.
 
Back
Top Bottom