matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Watu wengi ni wazee lakini vibogoyo, wamepinda, hawaoni, hawanusi, wanatembea na chupa za mikojo na vidonge vya rangi mbalimbali. Huu uzee unagharama sana. Kuna mambo ukianza kufanya leo yanaweza kukusaidia ukazeeka huku huku ukiwa unanguvu na kila kitu kiko vizuri.
1: Asilimia kubwa ya vyakula vyako viwe mzao wa ardhi (plant based), Maana mwili wako ulikuwa designed kutumia mazao ya ardhi sio wanyama wenzako.
2: Epuka magomvi na mafarakano. Pima jambo kama halina manufaa kubali kushindwa. Simba ni mfalme wa Pori lakini anazeeka akiwa na miaka 14, wakati kobe mchovu wa pori anazeeka akiwa na miaka 100+. Kwa sababu simba ni mkali na muda wote anafokafoka hovyo.
3: Fanya mazoezi ya kawaida. Wanaokimbia mabio umbali mreefu huzeeka vibaya. Tembea tu kwa miguu mara nyingi. Hili ndio zoezi salama na la bei nafuu.
4: Kuwa na mke mmoja mnayependana. Pia tafuta marafiki na watu au baadhi ya ndugu mnaoendana muwe na muda wa chakula cha pamoja na kuenjoy.
5: Amini katika Mungu anayekuongoza wewe binasi sio kama kanisa au kikundi cha dini au kupitia mtu flani wa kiroho. Hata kama unasali hii ya Mungu binafsi itakupa faida kubwa kiafya na kiuwekevu.
Hizi ni baadi ya sababu kwa nini ni sehemu tatu tu duniani ndio kuna idadi kubwa ya wazee ambao hawaumwiumwi wala kuomba kufa kila muda (okinawa, roma linda na kisiwa kimoja huko Italia). Wazee wengi duniani ni wagonjwa na wamejaa masumbufu mengi wanajiombea kufa.