matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
- Thread starter
- #21
Jali mwili wako, mwili wako ndipo mahali pekee unapoishi.Mkuu’
Umenena vyema.
N muhmu sana tukazitunza afya kwa kufuata kanuni angali tu vijana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jali mwili wako, mwili wako ndipo mahali pekee unapoishi.Mkuu’
Umenena vyema.
N muhmu sana tukazitunza afya kwa kufuata kanuni angali tu vijana!
HahahahaNamba 4 mstari wakwanza mi nimeshindwa yani apo ndo najiona kabbisa umenizeesha
YapUnazeeka kama Mzee Mwinyi
ShukranWatu wengi ni wazee lakini vibogoyo, wamepinda, hawaoni, hawanusi, wanatembea na chupa za mikojo na vidonge vya rangi mbalimbali. Huu uzee unagharama sana. Kuna mambo ukianza kufanya leo yanaweza kukusaidia ukazeeka huku huku ukiwa unanguvu na kila kitu kiko vzr.
1: Asilimia kubwa ya vyakula vyako viwe mzao wa ardhi (plant based), Maana mwili wako ulikuwa designed kutumia mazao ya ardhi sio wanyama wenzako.
2: Epuka magomvi na mafarakano. Pima jambo kama halina manufaa kubali kushindwa. Simba ni mfalme wa Pori lakini anazeeka akiwa na miaka 14, wakati kobe mchovu wa pori anazeeka akiwa na miaka 100+. Kwa sababu simba ni mkali na muda wote anafokafoka hovyo.
3: Fanya mazoezi ya kawaida. Wanaokimbia mabio umbali mreefu huzeeka vibaya. Tembea tu kwa miguu mara nyingi. Hili ndio zoezi salama na la bei nafuu.
4: Kuwa na mke mmoja mnayependana. Pia tafuta marafiki na watu au baadhi ya ndugu mnaoendana muwe na muda wa chakula cha pamoja na kuenjoy.
5: Amini katika Mungu anayekuongoza wewe binasi sio kama kanisa au kikundi cha dini au kupitia mtu flani wa kiroho. Hata kama unasali hii ya Mungu binafsi itakupa faida kubwa kiafya na kiuwekevu.
Hizi ni baadi ya sababu kwa nini ni shemu tatu tu duniani ndio kuna idadi kubwa ya wazee ambao hawaumwiumwi wala kuomba kufa kila muda (okinawa, roma linda na kisiwa kimoja huko Italia). Wazee wengi duniani ni wagonjwa na wamejaa masumbufu mengi wanajiombea kufa.
Mjomba wangu alikuwa na zaidi ya mil 200 kwenye account hiyo ni akiba na biashara zinaendelea ila sukari ilimtesa mpaka aliomba mtu asimpeleke tena hospitali ameteseka sana tumwache ampuzike. Omba afya njema ni mtaji mkubwa.Mchawi pesa tu... Hizo nyingine ukiwa hauna pesa ni mbwembwe
Umenena vyema sana.Watu wengi ni wazee lakini vibogoyo, wamepinda, hawaoni, hawanusi, wanatembea na chupa za mikojo na vidonge vya rangi mbalimbali. Huu uzee unagharama sana. Kuna mambo ukianza kufanya leo yanaweza kukusaidia ukazeeka huku huku ukiwa unanguvu na kila kitu kiko vizuri.
1: Asilimia kubwa ya vyakula vyako viwe mzao wa ardhi (plant based), Maana mwili wako ulikuwa designed kutumia mazao ya ardhi sio wanyama wenzako.
2: Epuka magomvi na mafarakano. Pima jambo kama halina manufaa kubali kushindwa. Simba ni mfalme wa Pori lakini anazeeka akiwa na miaka 14, wakati kobe mchovu wa pori anazeeka akiwa na miaka 100+. Kwa sababu simba ni mkali na muda wote anafokafoka hovyo.
3: Fanya mazoezi ya kawaida. Wanaokimbia mabio umbali mreefu huzeeka vibaya. Tembea tu kwa miguu mara nyingi. Hili ndio zoezi salama na la bei nafuu.
4: Kuwa na mke mmoja mnayependana. Pia tafuta marafiki na watu au baadhi ya ndugu mnaoendana muwe na muda wa chakula cha pamoja na kuenjoy.
5: Amini katika Mungu anayekuongoza wewe binasi sio kama kanisa au kikundi cha dini au kupitia mtu flani wa kiroho. Hata kama unasali hii ya Mungu binafsi itakupa faida kubwa kiafya na kiuwekevu.
Hizi ni baadi ya sababu kwa nini ni shemu tatu tu duniani ndio kuna idadi kubwa ya wazee ambao hawaumwiumwi wala kuomba kufa kila muda (okinawa, roma linda na kisiwa kimoja huko Italia). Wazee wengi duniani ni wagonjwa na wamejaa masumbufu mengi wanajiombea kufa.
Tafuta pesa tu, ukiwa na pesa utazeeka vizuri
Wapo wenye pesa na wanateseka vibaya
ANina over 60 na sasa hivi nimetoka kutembea kwa mda wa saa moja
Namshukuru Mungu sina maradhi yoyote yale hata tezi dume
Sijisifii ila najitahidi kwa kula vizuri na kazi nyingi sio mvivu wa kukaa kaa na kupiga soga kijiweni
Wazee wenzangu wananishangaa nikiwapita na baiskeli 😄
Ni kweli mkuu tajiri mzungu anaishi kwenye nymba yenye eneo kubwa balaa. Upepo wa kutosha mazoezi golf etc.Ukiishi kijijini automatically utafanya mazoezi ya kutembea, kula kiasili, kuwa na mke mmoja kwa Wakristu, n.k
Ujumbe huu utufikie sisi wenye maisha yafuatayo
1. tunaojiita matajiri wenye nyumba za mageti na ka-gari ka kuendea kazini
2. tukifika kazini tunakalia viti vya kuzunguka 4.saa nne tunakula supu, chapati na Coca-Cola.
3. Mchana tunakula makaange na pepsi baridiiiii
4.jioni kabla ya kufika nyumbani tunapiga Serengeti baridiiii
5. Wenye hasira na tusiokuwa wavumilivu kwa mawazo ya watu wengine
6. Tunaotumbua fedha ya mshahara mnono bila kuwekeza tukisubiri fedha za pensheni kuanzisha Miradi ya uzalishaji mali
7. Tunaozaa ovyo na kumwachia mke ndo alee watoto sisi tuko bize na safari za ulaya. Utakuta una fedha lakini mitoto ni mapapai.
Kuna jamaa anaitwa Methusela aliishi miaka zaidi ya 900. Kama 100 au80 unaona ni mingi au ni halali kufika ukiwa hoi ibn taabani utakuwa hujitendei haki. Ni suicidal mindset ambazo umemezeshwa na wajanja wa dunia.Ukae saaaana ugundue nn hapa duniani.
Kupiga story napiga nao sana don't get me wrongKama hupigi stori na age mates wako Kuna shida mahali
A
Maisha ni maamuzi na uchaguzi. Ukiona kuuza viatu na kugombana na watu kwa ukondakta hadi unakufa ndio kunakufaa uko sahihi. Ukifika sehemu ukasema sitaki ngoja niexplore mawimbi mengine ya maisha ambayo yataniletea amani shangwe uzima mrefu na vicheko pia utapata.Natembeza viatu, maisha ni magumu , mke anakaanga maandazi, watoto wanasoma shule za kidumu na fagio, nyumba ya kupanga.
Kufokafoka katika mazingira haya ni lazima, maisha yenyewe tu ni zaidi ya mazoezi.
Ushauri wako utafaa kwa wale wenye maisha fulani ya kati au ya juu, kwetu sisi huku magoloka ni ngumu sana.