Fanya hivi kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa njia ya mtandao

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833
​

Je ulikua unasumbuka kutafuta Cheti cha kuzaliwa ? Hivi unajua nchini Tanzania unaweza kupata Cheti chako cha kuzaliwa kupitia simu yako bila kwenda kwenye kituo cha kutolea hiyo huduma.

Kwanza inabidi utambua Kuwa E - RITA , ni mfumo wa kidigitali unaokuwezesha kutuma maombi ya huduma ya vizazi kwa njia ya kidigitali popote ulipo Tanzania. Hiki ni chombo cha Serikali kinachojihusisha na masuala yote ya huduma ya vifo na vizazi.


​

Sasa leo nakuambia njia rahisi ya kuweza kupata Cheti cha kuzaliwa kupitia simu yako βœ‹
⚑ Ingia kwenye tovuti hii www.rita.go.tz
⚑ Chagua E Rita Kisha chagua huduma za mtandao Kisha utachagua usajili wa Cheti cha kuzaliwa.
⚑ Kama huna Akaunti inabidi ujiandikishe kupitia email na Namba yako ya Simu.

​

hatua ya pili ni kujaza fomu ambapo baada ya kuingia kwenye Akaunti yako Sasa chagua birth certificate . Inabidi ujaze fomu Kwa taarifa zako kamili kuanzia majina yako kamili , tarehe na mahali ulipozaliwa na majina ya wazazi wako.

​

Utaweza kuambatanisha vitu muhimu kama vile Namba yako ya Nida, Malipo ambapo utalipia gharama utaweza kulipia benki au mitandao ya simu ndani ya wiki mbili TU utaweza kupata Cheti chako.

Kwa msaada zaidi wapigie +255 22 221 2820 au email Yao
info@rita.go.tz unakuwaje mtanzania huna Cheti cha kuzaliwa πŸ˜‰.
 
Cheti cha kuzaliwa alafu unaambatanisha namba ya nida? Unaipataje namba ya nida bila cheti cha kuzaliwa?
 
Cheti cha kuzaliwa alafu unaambatanisha namba ya nida? Unaipataje namba ya nida bila cheti cha kuzaliwa?
This is not Proof of Citizenship

NEither NIDA nor BIRTH CERTIFICATE so unaweza tumia njia yyte kupata chochote kat ya hivyo hapo juu.
 
Blaza unataka tukale wapi sisi wa steshenari?...
Kwa anaehitaji cheti Cha kuzaliwa mahali popote pale nione inbox
Mahitaji unayotakiwa Kama ni Cha mtoto wako..

1. Kadi lake la kliniki
2. Leaving certificate (Kama amemaliza kidato Cha nne
3. Kitambulisho chako mzazi(baba/mama) Cha mpiga au nida
4. Kitambulisho Cha mumeo au mkeo Cha mpiga kula au nida...

Hapo utasubiri tu siku nikupigie simu ukachukue hicho cheti ofisi za Rita karibu na wewe..
Gharama ni 25000/=
Elfu 20000 hii ntakutumia control number ulipe mwenyew ulipo..
Elfu 5000/= utantumia Mimi ...
 
πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ Sio wote watakao weza kaka utaendelea kula TU pesa πŸ˜€πŸ˜€ usijal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…