Fanya hivi kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa njia ya mtandao

Fanya hivi kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa njia ya mtandao


Je ulikua unasumbuka kutafuta Cheti cha kuzaliwa ? Hivi unajua nchini Tanzania unaweza kupata Cheti chako cha kuzaliwa kupitia simu yako bila kwenda kwenye kituo cha kutolea hiyo huduma.

Kwanza inabidi utambua Kuwa E - RITA , ni mfumo wa kidigitali unaokuwezesha kutuma maombi ya huduma ya vizazi kwa njia ya kidigitali popote ulipo Tanzania. Hiki ni chombo cha Serikali kinachojihusisha na masuala yote ya huduma ya vifo na vizazi.



Sasa leo nakuambia njia rahisi ya kuweza kupata Cheti cha kuzaliwa kupitia simu yako ✋
⚡ Ingia kwenye tovuti hii www.rita.go.tz
⚡ Chagua E Rita Kisha chagua huduma za mtandao Kisha utachagua usajili wa Cheti cha kuzaliwa.
⚡ Kama huna Akaunti inabidi ujiandikishe kupitia email na Namba yako ya Simu.


hatua ya pili ni kujaza fomu ambapo baada ya kuingia kwenye Akaunti yako Sasa chagua birth certificate . Inabidi ujaze fomu Kwa taarifa zako kamili kuanzia majina yako kamili , tarehe na mahali ulipozaliwa na majina ya wazazi wako.


Utaweza kuambatanisha vitu muhimu kama vile Namba yako ya Nida, Malipo ambapo utalipia gharama utaweza kulipia benki au mitandao ya simu ndani ya wiki mbili TU utaweza kupata Cheti chako.

Kwa msaada zaidi wapigie +255 22 221 2820 au email Yao
[email protected] unakuwaje mtanzania huna Cheti cha kuzaliwa 😉.
Ahsante kwa elimu
 
Hata mtu mzima naweza kuomba cheti kingine mkuu?? Au ni kumuombea mtoto tu?
Hata vile vya zamani watu wanatakiwa waende kubali wapavye hivi vipya
 
Nataka niombe ili niwe navyo viwili, nataka kupunguza umri mana sasa hv nna 45 afu hata sijaajiriwa serikalini 😂 nataka nipunguze mpaka 25 😎
Njoo lumumba mkuu,upate buku 7 kwa kuponda CHADEMA na kusifu Mama.
 
Nawezaje kuwaombea watoto Cheti cha kuzaliwa Kwa njia ya E-RITA?
Ni Kwa kupitia kwa kipenzi chetu cha dhati Imam Hussain ibn Ali A.S aliyeuwawa kikatili kuutetea, kuulinda na kuupigania uislamu dhidi ya dhulma, ukandamizaji, unyanyasaji na uonevu.

Screenshot_2025-07-18-16-30-28-06_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg
Screenshot_2025-07-09-18-01-08-90_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg


adriz Mufti kuku The Infinity makilo Monetary doctor Arizona 1 hearly
 
Mkuu, vipi ku-approve vyeti vya ndo mtandaoni..?
 
Back
Top Bottom