Fanya hivi kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa njia ya mtandao

Kupata cheti cha kuzaliwa ni mpaka uwe na namba ya NIDA na kupata nida ni mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa, kipi ni kipi
Mimi mwenyewe nimebaki ninashanga kwanini isiwe unaweka jina lako tu kamili na maelezo machache unayo yakumbuka ?kuna wengine wamezaliwa bila ya kuwajua baba zao ni kina nani ?
 
Kuna tofauti yoyote kati ya cheti cha kuzaliwa ambacho kinatolewa hospitalini na hivyo mnavyotoa huko RITA?
 
kwenye kufungua akaunti ukifika kwenye password unaweka kwanamna gani mana nimeweka inagoma kukubali.msaada
 
Hivi vyeti wanavyotoa siku hizi hospital vya kujazwa kwa mkono mtu unaweza badili kupata ile design ya zamani?
Yaan namaanisha hivi vya rangi,
Yani kwa kweli sijawai kukipenda cheti cha mwanangu, aliyejaza ana limwandiko libayaaaa πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯😫
Miherufi mikubwa imekaa ovyoovyo,
Natamani kubadili hata kama nitalipia, maana hiki in vile unapewa bure unapoanza kliniki
Najua kuna watakaoshangaa na kuona kuwa cheti ni karatasi tu, ila wallaih jamani huu mwandiko hapana, hata wewe ungepata hasira
 
Kile cha hospitali sio cheti ni kadi ya kuzaliwa, Rita Ndo wanatoa cheti.
Ukienda Rita Pia Uwe na hy kadi kutoka hosp
Mkuu, siku hizi wanatoa hospital kwa watoto chini ya miaka mi5 bure. Sio kama zamani kwamba unapewa tangazo la kuzaliwa then unaenda kujisajili.
Baada ya kupitia comment yako nimejaribu kuangalia website ya Rita wametoa ufafanuzi pale, kuwa vile ndio vyeti na Rita vinatolewa kwa watoto chini ya miaka mi5, na wao wataendelea na makundi mengine. Na iwapo kitapotea unatakiwa kulipia 5000 kupata kingine.
πŸ˜€πŸ˜€ ngoja TU nikipoteze hiki nikachukue mwandiko mwingine wa elfu 5, huu mwandiko wa bure hapana aiseee.
 
Ukiingia kwenye mfumo wa E-RITA kuna sehemu ya imeandikwa old to new, hapo unajaza taarifa za hicho cheti ulichopewa hospitali kisha una submit.

Ndani ya siku 3 hadi 5 za kazi unakuwa umepata cheti kipya ambacho ni hivi vya kisasa.

Gharama ya kubadili old to new nadhani ni 3,500 hadi 5,000 haizidi hapo.
 
Huna haja ya kukipoteza wewe fanya kubadili kutoka old to new wala hawana shida maana wanachukulia labda kimeharibika ama kuingia maji nakadhalika

Mimi nilipata cha mwanangu ambacho nilibadili old to new ndani ya siku 3 pekee.
 
Huna haja ya kukipoteza wewe fanya kubadili kutoka old to new wala hawana shida maana wanachukulia labda kimeharibika ama kuingia maji nakadhalika

Mimi nilipata cha mwanangu ambacho nilibadili old to new ndani ya siku 3 pekee.
Mkuu asante, nitafanya hivyo, wallaih cheti cha mwanangu ukikiona unaweza kulia.
Yani huwa sielewi kwa nini huyu mama wamempa kazi ya kujaza vyeti, yan anaandika ovyoovyo, miherufi mikubwaaaa mibaya hadi inatoka nje ya mstari.
Hakika moyo wangu haujawai kukipenda, nilipopewa nikapita kufanya lamination then nimekitupa kule. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ yani ni vile najua kipo room ila sitaki kujua kipo sehemu gani, sitaki kukiangalia tena
 
Dah, noma sana mkuu. Fanya hilo zoezi kama nilivyokuekekeza ni siku 3 hadi 5 kinakuwa tayari.

Ni kweli vyeti vinavyotolewa hospital ni miyeyusho sana havina mvuto kabisa aise.

Na gharama ni nafuu haizidi elfu 5.
 
Wewe kazi yako ni kuwasilisha maombi tu,Rita ndio wanatengeneza kadri ya taarifa ulizowasilisha na kuprint,utafuata cheti chako kwenye ofisi ya Rita uliyoichagua wakati wa maombi.
Hata mtu mzima naweza kuomba cheti kingine mkuu?? Au ni kumuombea mtoto tu?
 
Dah, noma sana mkuu. Fanya hilo zoezi kama nilivyokuekekeza ni siku 3 hadi 5 kinakuwa tayari.

Ni kweli vyeti vinavyotolewa hospital ni miyeyusho sana havina mvuto kabisa aise.

Na gharama ni nafuu haizidi elfu 5.
Sasa hivi wanajitahidi,cheti kinakuwa tayari ndani ya masaa 24 kama nyaraka hazina mashaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…