Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

Kwenye bajeti zako hamna sehemu ya wazazi mkuu?
 
Uzi umekaa vizuri sana mkuu hongera sana. Tatizo siku hizi vipato vyetu vinakuwa na madeni kweli na unajikuta hauna namna. Yaani kabla ya kuanza kugawanya kipato katika huu mchanganuo unajikuta kuna mambo yamejitokeza ya lazima yanaharibu kabisa huo mchanganuo na fedha inakuwa haitoshi kabisa, ila ni kanuni nzuri sana.
 
Kibongo bongo haitekelezeki

Huwezi kuwa na familia let's say yenye mke na mtoto uweke matumizi 200,000 plus mchepuko lazima

Hapo extended family hujaiweka, Kodi ya nyumba, usafiri, mavazi

Hiyo bajeti haiendani na maisha ya Kiswahili
 
Ni rahisi sana kusema kuliko uhalisia. Yaani upate 500,000 na matumizi yawe 200,000? Labda kama hiyo 500,000 unaivuna sehemu hiyo hiyo unayoamkia na kulala, hauna mke/mme na watoto (familia), si mpangaji wa nyumba za watu na unaishi sehemu ambako mahitaji hayakumbani na mfumko mkubwa wa bei. Mfano mtu unaeishi Dar na unalazimika kupanda magari mawili hadi kufika kazini kwako ambako mwisho wa mwezi utavuna hiyo 500,000/= kwa siku utatumia shilingi ngapi pamoja na kula? Nauli tu kwenda na kurudi ni karibia 3,000/= na ukiweka na chai na chakula cha mchana tu tuseme kwa kujibana iwe 5,000/= jumla kwa siku imeshakuwa 8,000/=. Kama kwa mwezi unalazimika kufanya kazi kwa siku 6 ni 48,000/= na kwa mwezi tayari ni 200,000/=. Hapo haujaweka hesabu ya chakula cha usiku na mahitaji mengine ya binafsi na kama una familia haujaweka mahitaji binafsi ya mwenza, watoto, wazazi na mahitaji ya pamoja kama familia kama vile kodi ya nyumba kwa mpangaji, chakula, bills za umeme, maji, king'amuzi n.k. Ndiyo maana nasema ni rahisi kusema ila kiuhalisia ni ngumu.
 
Peleka kwa wasiojiweza hata matajiri wanafanya tena wapo sahihi kupeleka moja kwa moja kwa walengwa kama wahanga wa dhoruba ,mayatima ,wagonjwa na mafukara.
 
Mimi binasfi nalipwa 400,000 kutoka kwenye kibarua changu maana sio ajira.
Niko nna familia , kila siku kwa kubana sana nyumbani inatumika 7,000
Kodi ya nyumba kwa mwezi 80,000.
Bili za maji umeme na taka 20,000
Mtoto shule kila mwezi 30,000
Nauli ya kazini kwa mwezi haipungu 35,000.
Matumizi mengine kama dawa za meno sabuni mafuta nk haipingui 10,000

Jumla inakaribia 360,000
Sasa hapo mleta mada ukisema utoe tu fungu la kumi 40,000 sadaka, akiba , msaada dharura ni vipi itawezekana?
 
Budget iko tight.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…