Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

SI Biblia inasema fungu la kumi watoe wale waliotoa MISRI ili iwe ukumbusho kwamba Mungu aliwatoa huko kwa mkono wake wenye nguvu? sisi ni lini tulipewa hilo Agizo? Je siku hizi kuna walawi wasio kuwa na kwao? au walawi sasa nao wanafanya biashara,wanajenga n.k
 
Kibongo bongo haitekelezeki

Huwezi kuwa na familia let's say yenye mke na mtoto uweke matumizi 200,000 plus mchepuko lazima

Hapo extended family hujaiweka, Kodi ya nyumba, usafiri, mavazi

Hiyo bajeti haiendani na maisha ya Kiswahili
Mangi kama wewe umeshindwa usitishie wengine kuwa haiwezekani
Lazima iwe ngumu ili wawe nao wachache
 
Mangi nidhamu ya hela ipo karibu na uchoyo so usiogope hata kuitwa bahili ili kulinda uchumi wako
You better tell us something realistic bro. Siyo porojo tu ukiwa nyuma ya keyboard. Hakuna chembe yoyote ya uchoyo kwenye huo mfano nilioutoa.
 
Uzi umekaa vizuri sana mkuu hongera sana. Tatizo siku hizi vipato vyetu vinakuwa na madeni kweli na unajikuta hauna namna. Yaani kabla ya kuanza kugawanya kipato katika huu mchanganuo unajikuta kuna mambo yamejitokeza ya lazima yanaharibu kabisa huo mchanganuo na fedha inakuwa haitoshi kabisa, ila ni kanuni nzuri sana.
Umesema kweli ila jitahidi utumia ata aslimia 50 tyu ya mfumo
 
Point kubwa ni NIDHAMU YA MATUMIZI

Ukiwa nayo hautahitaji hizo percentage zote ulizoweka. Kwa nini nasema hivyo?

Sio kila siku maisha yataenda kama hizo asilimia ulizoweka. Kuna dharura nyingi sana maishani

Ila ukishakuwa na nidhamu ya matumizi utajua jinsi gani ya kubalance matumizi yako na kusave
 
You better tell us something realistic bro. Siyo porojo tu ukiwa nyuma ya keyboard. Hakuna chembe yoyote ya uchoyo kwenye huo mfano nilioutoa.
Mangi hatanikikwambia ukweli bado utaamini uongo .
Sikia tumia mfumu huo lazima utoboe
 
Point kubwa ni NIDHAMU YA MATUMIZI

Ukiwa nayo hautahitaji hizo percentage zote ulizoweka. Kwa nini nasema hivyo?

Sio kila siku maisha yataenda kama hizo asilimia ulizoweka. Kuna dharura nyingi sana maishani

Ila ukishakuwa na nidhamu ya matumizi utajua jinsi gani ya kubalance matumizi yako na kusave
Ni kweli nidhamu ya matumizi inajengwa !! Ndio kitu nataka kukiingiza kwa watu
 
SI Biblia inasema fungu la kumi watoe wale waliotoa MISRI ili iwe ukumbusho kwamba Mungu aliwatoa huko kwa mkono wake wenye nguvu? sisi ni lini tulipewa hilo Agizo? Je siku hizi kuna walawi wasio kuwa na kwao? au walawi sasa nao wanafanya biashara,wanajenga n.k
Enyi kizazi cha wabalisha maandiko !!
Soma matendo ya mitume
Juu ya anania na mkewe walivyodanganya fungu la kumi
 
Hata kwa bachelor anayeishi Dar atatumia nguvu kubwa kuishi tena maisha duni kwa bajeti hii

Ulipata nafasi ya maisha ishi
Si eke assumptions zako mangi!!wewe juu mkono unaotoa zaidi ndio unapokea ,sio mambo ya ubachelor wewe toa maana ukisaidia usiangalie unafaidika nni?
 
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.

Kanuni
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5
Jumla 100%

Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata kama pato lako la mwezi.

Mfano Kama unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata kama umepewa fedha kama zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.

Faida za Fungu la kumi
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.

Akiba 30
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
mfano kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,00/= asilimia 30 ni sh. 150,00/=

Matumizi 40
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
angalizo matumizi yasizidi fedha hiyo.

Dharura 10
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia kama msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•Kama pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.

Msaada 5%
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.

Sadaka 5%
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utaenda kutoa sh. 6,250/=.

Kumbuka;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
•Jaribu na anza hata na kidogo kidogo, kuwa na nidhamu ya fedha uone nayo itakavyokuheshimu.
NB:

#MAENDELEO HAYANA CHAMA#
Nimependa mchanganuo wako ila ningependa kutoa ushauri..

Chukua Sadaka na Zaka Weka Kwenye Msaada..

Saidia watu sana walio na shida Usipeleke pesa kwa watu wenye Vitambi waile
 
Back
Top Bottom