Anania haikuwa Fungu la kumi Mzee wangu anania ilikuwa Ni fedha walizokubaliana watu wote..
Baada ya watu wengi Kuongezeka waliokubali Injili iliyokuwa Ikienezwa na Petro..walihitaji Kupatikane Pesa zaidi za kusambaza injili hiyo Na kusaidia watu wenye Uhitaji hivyo kwa Hofu ya Mungu watu walijitoa sana Kusaidia wengine wenye Pesa walipeleka..
Wale wenye Mashamba walipeleka..
Na hata Yusuph aitwaye Barnaba yeye aliuza shamba lake lote na kupeleka fedha kwa mitume..
Matendo 4:32-37
View attachment 2963149
Sasa kilichotokea kwa Anania ni kwamba Alichagua sehemu ya Shamba Akaliuza ilutakiwa ile pesa aipekeke kwa mitume ila akachukua Baadhi ya pesa na kuzificha akapeleka Nusu Pesa..
Na ndo maana Petro anamuuliza kuwa kilipokuwa Shambani hakikuwa Mali yako??
Maana angeweza kutoa Kipande kidogo tu cha shamba akauza na kingine akauza kwa matumizi yake na kingine kwa matumizi ya kutoa..
Ila alipotia Nia kwamba anauza kwa sababu Ya Mungu hapo ndo ilipoleta shida..
Nakuacha utafakari maSwali haya Kilipokuwa Kwako hakikuwa mali yako?, kilipokuwa Kimekwisha kuuza thamani yake Haikuwa kwa uwezo wako??
maana alikuwa Na uwezo wa Kuuza Kidogo na pia alikuwa na Uwezo wa kupandisha Thamani na kuchukua kiasi alichoahidi kupeleka na kiasi kingine kutumia..
MIND YOU HAIHUSIANI NA SADAKA WALA ZAKA HIYO NI MAKUBALIANO WALIYOWEKA NA ANANIA ALIYAVUNJA
View attachment 2963158