Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

hapo ndio huw nafeli kiasi cha kukaa na ukata kwa mda mrefu, nashindwa kuicontroll fedha jamaa zangu
 
Sadaka za madhabahuni zinanguvu mno iyo kusaidia watu ni lazima sio sadaka Mangi !!
Sitokufundisha kila kitu
Inategemea madhabahu yako umeiandaa wapi! Nimeona watu wapo madhabahuni wanatongoza wake za watu ibada ikiendelea. Kuna siri kubwa sana na vinavyoitwa madhabahu kwenye hizi mainstream churches. Ukienda kanisani angalia kwa macho ya rohoni utaona vitu vingi vya kuogofya kwenye sadaka na madhabahu
 
Watumishi huwa wanawadanganye kwa kusoma kimstari kimoja tu badala ya kusoma neno kamili
Ni kweli Kabisa!
Wanang'ang'aniza maandiko Ili waibe Pesa za Watu Waliozichumia Jasho wakati nao hawana uhitaji wana mikono Miwili na miguu wanaweza kwenda shambani na wakalima..

Pesa Inatakiwa iende Direct kwa Wanaoihitaji kama Mayatima , Wasiojiweza Nenda kwenye vituo vya kulelea Watoto yatima wape msaada ..Tafuta watu wenye Mahitaji Wape msaada..

Utabarikiwa Saaana plus Uwe Na nidhamu ya Pesa
 
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.

Kanuni
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5
Jumla 100%

Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata kama pato lako la mwezi.

Mfano Kama unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata kama umepewa fedha kama zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.

Faida za Fungu la kumi
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.

Akiba 30
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
mfano kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,00/= asilimia 30 ni sh. 150,00/=

Matumizi 40
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
angalizo matumizi yasizidi fedha hiyo.

Dharura 10
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia kama msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•Kama pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.

Msaada 5%
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.

Sadaka 5%
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utaenda kutoa sh. 6,250/=.

Kumbuka;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
•Jaribu na anza hata na kidogo kidogo, kuwa na nidhamu ya fedha uone nayo itakavyokuheshimu.
NB:

#MAENDELEO HAYANA CHAMA#
Unaandika formula ulizozisoma kwenye vitabu sizizo na uhalisia?

Hiyo hela unsyoipigia asilimia Iko wapi? Benki unadaiwa, vikoba unadaiwa, kwa mangi unadaiwa, shule watoto wamerudishwa nyumbani. Unaongea nini? Huo mkupuo wa kupigai asilimia uko wapi,?
 
Back
Top Bottom