Fanya yafuatayo ukitaka usivamiwe sana na vibaka au hata wakuokoe kwenye hatari

Kwangu Mimi naona ukishafanya hayo uliyosema unakuwa umefadhiri vibaka.

Huo upuuzi wao unapaswa kupingwa na kila aliye na akili timamu haiwezekani mtu atafute kwa jasho wewe ukae uchochoroni uchukue tu kirahisi. Aisee mi labda nisimiliki chuma ntawalaza wengi tu watao jaribu kuleta ujinga kwenye jasho langu
 
Kabisa Mkuu umenena
 
Correct Mkuu
 
Hii ni sawa kabisa,kwani ni watu nao wanahitàji upendo ,kwani wengine wameingia huko kwa mkumbo wa marafiki wanashindwa kuchomoka.
 
Sasa shida yote hiyo ya nn.. ishi uwezavyo kwa kifupi binadamu hatabiriki. Ata uwafanyie nn bado kuna watu watakuchukia t
 
Uliyoyaandika ni sawa na kusema "mtoto wako hata akiwa anavunja vyombo ndani kila siku makusudi/anatukana majirani usimtandike ila mnunulie pipi na umuonye kwa maneno ya upole ili asikasirike"

Oyaah hapa mtaani tuliwachakaza kinoma walipigika balaa zamani kulikua na vijiwe vya wahuni kama vinne sahivi vimevunjwa vyote maana ilikua mtu akikabwa au akivunjiwa nyumba kinawekwa kikao na tunawapigia msako huko huko kijiweni tulishawachoma moto wawili mchana kweupe maana sisi ni wengi kuliko wao ilifika hatua wengine wakakimbia had mkoa.

Sahiv mtaan vimebaki vijiwe vya alkasus tu.
 
Hata kwa sisi wadada inatuhusu hii mkuu? Kupiga story na kibaka kweli[emoji2960]asije akakuchenjia dk 0
Unaweza usikae nae kupiga story ila ukipita usiwavimbie.

Wakati fulani nilikua na kasehemu nauza pombe Mwananyamala. Pembeni ya frame yangu kulikua na kituo cha bodaboda. Wale bodaboda nilivyofika nikazoeana nao haraka kwa sababu nilikua nawatuma mara nyingi halafu siku moja moja nawapatia pombe walikua wananikubali sababu walikua wananiona wa tofauti halafu naishi nao kawaida. Katika hao kuna wengine walikua vibaka kabisaaaa. Mmoja alinihadithia kabisa namna wakienda kuiba mpaka wanabaka ila nilikua namshauri sana sana.

Ila tu waliniahidi kwamba kamwe sitokaa nikaibiwa pale na mpaka naondoka lile eneo nilikua nafunga kufuli moja tuu. Kwa kifupi walikua wananilinda na waliniambia Kino yote mpaka Sinza wanajua vibaka wao siku nikiibiwa niwaambie wanirejeshee vitu vyangu.


Wakati mwingine sio kwamba unasapoti tabia zao ila kama unajua huwezi kupambana nao bora uwe mpole maisha yaende
 
kuna siku walinipiga cm kwenye daladala.

kesho yake husb akawafata kijiweni kwao akawaambia " jana mida ya asbh mmechukua cm ya wife kwenye daladala naomba muirudishe"

cha ajabu haikufika saa10 jioni, cm ikarudishwa na msamaha nikaombwa,
na zaidi nikahakikishiwa usalama wangu popote ntakapo pita.

kuna muda wajuba ni watu poa sana
 
Hahaha!pande gani mkuu maana nishaskia case kama hyo
 
Yan inaonesha wew n mshamba Sana endelea kujidanganya endelea kujitekenya na kucheka mwenyew wale watu hawaaminiki yan hawaaminiki wakishavuta na wakishatumia madawa s wenzako tena hao tena wakijua unawajua na umewatambua n hatar Sana
 
Huo muda wa kuzoeana nao nautolea wap? Nipo busy na mamb yang ya msingi
 
Labda tumetofautiana mitaa, huku kwetu hatukabwi na wazawa wa eneo letu

Ni vibopa kutoka mitaa sita huko vinakuja survey mida mibovu, na machizi wa huku wanaji mix mitaa ya huko ambayo hawafahamiki

Street tunaishi kiniga, ukijidai unaleta falsafa za kisomi huku au ni mtu wa kuji isolate sana na watu basi unakua kwenye radar za watemi

Mimi ni mpenzi wa draft, kiukweli huu mchezo umenisaidia sana kujenga mahusiano mazuri na watu wa rika nyingi na wenye tabia tofauti tofauti kiasi cha kunifanya nijue mengi.

Kwenye kijiwe cha draft hapakosi wahuni na ni rahisi sana kujenga chemistry na wadau kupitia draft hata kama ni mgeni wa eneo hilo.

Kuna siku nilichelewa mida ya night mtaa umepoa nikawa najisogeza kuelekea gheto, ili niwahi kufika nikaamua kupita chocho

Lakini ile chocho ndio hemaya ya vibaka, watu wote wanajua eneo hilo ni maarufu kwa maskani ya watemi

Nikajisemea ili nipite hili eneo inabidi ni behave kihuni, nikarudi nyuma kuangalia duka ambalo liko wazi nikanunua sigara kali nikaiwasha

Nikapiga mlege natembea najivuta kwa kupepesuka nilipokaribia eneo lao nikawa naongea kihuni afu kwa sauti ya kilevi, "oya mazee hapo road kuna doka limepaki mamwela kibao wametanda, mi ningeweza kuamsha peke yangu sema nikaona dusko siwezi nikawakataa wanangu afu sema nini shikeni na huu mjiti (nikawarushia ile sigara kali moja ambayo sijaiwasha)

Wakasema "fresh mwanangu bora umetusanua ngoja tuamshe"

Afu nikawapita

So wahuni automatically walijua mimi ni mwenzao, na kwakua eneo wanalokuja kukaba, vibaka wanatoka pande tofauti tofauti wakadhani mimi ni kibaka mpya kumbe fix tu
 
Hiyo namba 4 ni hatari....unaweza kutwa kakamatwa kwa dawa za kulevya utashangaa na ww unaunganishwa kwenye kesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…