Fanya yafuatayo ukitaka usivamiwe sana na vibaka au hata wakuokoe kwenye hatari

Maisha......
 
Story yangu kuhusiana na hili; kuna siku nilikosea shortcut.. nikajikuta mtaa mmoja ulioashiria una wahuni kinyama kutokana na harufu harufu za ile kitu.. ilikuwa around saa 4 usiku..
Nikapata akili hapa ili nijiepushe na lolote ambalo pengine lingetokea, ngoja nicheze ngoma yao mapema.. nikashusha vioo vya mbele, nikaforward nyimbo hadi ilipo playlist yangu matata.. nikaanza na "notorious thugs".. beat nzito, nikaweka sauti ya kati, halafu katikati ya washkaji nikaita "oya man", nisaidie fegi hapo shop, nikampa buku 2, wakati nasubiri fegi tayari tukawa kwa "wu shot ya", then "hit em up"-- Nikaletewa fegi, nikamwachia jero na fegi, nikauliza njia huko mbele inatokaje; fegi nikaitupa kama mita 100 mbele..
 
So wahuni automatically walijua mimi ni mwenzao, na kwakua eneo wanalokuja kukaba, vibaka wanatoka pande tofauti tofauti wakadhani mimi ni kibaka mpya kumbe fix tu
Yataka moyo, Na uwe na hakika kile unachofanya ili wasikuotee kuwa unawaigizia
 
Kama nimemuelewa njia hiyo lengo kuu nikuwabadilisha
 
Wenzio wanatafuta pesa. Wewe unatafuta kuridhisha wavuta bhange
 
Ni kweli kabisa Ndugu kuna Siku niliibiwa Suruali zangu za Jeans kama Tatu hivi na nilipowaambia tu ndani ya dakika 45 waliniletea na wakasema aliyeziiba alikuwa bado ni Mgeni, hajazoea Mitaa na hakujua Mipaka yake ya Kuiba.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuna uwezekano raia wenzako wakakuchukulia nawe ni kibaka, usishangae wakikutia kiberiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…