Hawa wanaume wa siku hizi ni .......................................................... (wape jina unalofikiri na linawafaa).
Mabinti, hasa nyie wadogo wa alfu mbili, hata akuambiaje,
Usijichanganye kumzalia mtoto.
- Hakuna jukumu kubwa kwenye maisha zaidi ya kuzaa na kulea watoto. Mwanaume akikuambia bado hayuko tayari kukuoa ila anataka umzalie, huyo ni tapeli kama matapeli wengine tu.
- Kama hajaja kwenu kukuchumbia, hajakuoa usizae kiholela. Na ukiolewa, hakikisha una shughuli ya kiuchumi ya kukuwezesha kuhudumia watoto wako ikitokea amefariki, amekutelekeza au mmeachana.
- Mapenzi kunoga na ahadi za kukuoa siyo sababu ya kubeba tumbo hilo. Wanaume wasio wababaifu, wenye kujua nafasi yao kwenye malezi wamebaki wachache sana ni kama bahati nasibu (Rejea hoja No 1 & 2).
- Tumia uzazi wa mpango kuepuka mimba zisizotarajiwa kama hutaki basi tumia Kalenda au Condom (Kama hujui namna ya kujikinga kwa kutumia kalenda njoo hapa wamama tukusaidie na tukuelimishe.)
Ukitaka kujua huyo baba watoto wako mtarajiwa atakuwaje mkikosana na mna mtoto nenda kasome replies za wababa kwenye uzi wa jana wa waziri
Dkt. Gwajima D -
Jamii tuzungumze kuhusu baadhi ya wababa na matunzo kwa watoto - humo wamefunguka bila kuficha makucha yao.
Usiwe kama kenge mpaka uvuje damu ndiyo usikie - USIMZALIE BILA NDOA au UHAKIKA WA KUWEZA KUHUDUMIA MWANAO PEKE YAKO BILA YEYE.
Ni hayo tu, siku njema kwenu!
********
Naomba mtoe neno kwenye hili
Lamomy ,
Leejay49 ,
nakwede97 ,
Demi ,
Aaliyyah ,
Mamndenyi ,
Bantu Lady ,
Ms R ,
leo dada ,
Numbisa ,
cocochanel ,
cocastic ,
Evelyn Salt ,
ephen_