Mkuu mi siwabembelezi kabisa kuku kwa sababu nimeamua ni business. Kuna bike mmoja alikuwa analalia mayai 18 sasa simu ya 17 akashinda nje, mie namwangalia tu. Nikamwambia wife chemsha maji. Ikafika saa kumi na mbili nikamkimbiza kwa hasira nikamkata kichwa kikawa kitoweo saafi.
Sasa upande wa pili nikaanza kupiga dili nafanyaje....nikakamata box la viroba vya konyagi nikashindilia maranda nikaweka mayai yote. Nikamkimbiza jike mwingine kwa hasira kwelikweli, na mabuti nakumbuka alikula. Nikamkamata nikamuweka ndani ya box kisha nikafunga na gundi. Mayai yake, yalikuwa 7 nikayaweka kwa jike mmoja alikuwa na mayai 10. Nimemfungia hadi siku ya tatu nikaanza kusikia chwiichwiii...kutoa vifaranga wote kaangua.
Nikambeba nikampa maji na tikiti nusu na msosi kisha nikamwendea yule was mayai 17 ambapo sasa alifikisha 19 nikamfukuza na nikamuweka huyu aliyetoka jela. Akalalia. Huyu sasa aliyefukuzwa nikamtia tena jela siku mbili katoka hana muda na mayai tena. Hapa naposema ndo kati ya wale ninaotazamia mwezi ujao atatotoa.
Vifaranga wako OK kabisa sema walinipa jambajamba maana ikawa bajeti ya kerosine ipo juu, wanataka joto wale. Leo kunguru kamkamata mmoja nimefoka balaa hom hapakaliki nataka kifaranga wangu. Wife kasema kesho analeta jike mmoja.
Kwenye business mie sitaki utani, na kuku wangu wanalijua hilo. Jogoo wangu juzi alitaka kuwa kitoweo baada ya kutoonyesha umahili wa kuwashugulikia matetea, wife kama kawaida nikamwambia bandika maji jikoni, bahati nzuri nikamuona kachachamaa anapanda fastafasta...sitaki uhuni mie.