'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

Mwizi kaingia kwa Muandishi wa Habari Farouk Karim usiku wa kuamika leo Jumapili akaiba nguo na viatu na akaingia kwenye gari ya Farouk akachukua power window lakini hakuondoka tena akalala hapo hapo hadi asubuhi ya leo, wenyewe wakamgundua na kuja kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.

Farouk hii Teknolojia ulotumia naiomba nzuri sana, duh kaganda hapo hapo!

---

Farouk anena kwamba kumuomba Mungu akulinde ndiyo silaha muhimu

Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya familia.

Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.

Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi.

"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo zilizokuwa zimeanikwa kaziwekwa kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.

Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua nitafute inbox".

sketch-1591136367169.jpg

Ila huyu afande amejenga nje ya Beacon anatakiwa abomoe [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Wazanzibari kwa uchawi mbona wa Sumbawanga wakasome.

Mwizi mwenyewe mbona kama ananjaa hajala toka juzi.
Kama Wazanzibari wangekuwa wachawi kuliko Sumbawanga basi Zanzibar ingekuwa kama Somalia au Darfur. Ila mbona hata siku moja haijawahi kutokea kupiga radi kavu kavu Zanzibar wakati Sumbawanga zinatokea??
 
Huwa sifurahishwa na tabia ya mtu kujua kitu kisha unapohitaji msaada akataka afuatwe inbox. Dua inaitwa "Ratib Al Haddad" ni kwa ajili ya kulindwa dhidi ya wizi.
 
Kama anatumia ndumba kwenye ulinzi anashindwaje kutumia ndumba kwenye kazi ya utangazaji ili awe maarufu? Mtumia ndumba huyo.
Si kweli haingii akilini kusema anatumia ndumba kwenye kazi yake... Si kila mtangazaji maarufu anakua anatumia ndumba na Farouk si ripota maatufu saaana yupo sawa tu na wenzake akina juma kapipi,oscar makongo, Godfrey monyo, mabele makubi na wengine
 
Kwa nini waganga wasiweke hiyo Tech sokoni yaani itapunguza kwa kiwango kikubwa tabia ya wizi na ukwapuaji pia itawatajirisha hawa waganga na kua mabilionea kwa hali za maisha ya waafrika watapatikana customers wengi mno
 
Unalizungumziaje hili tukio mashana jr ukiwa kama balozi wa kudumu na Mwakilishi mkazi wa kanda ya afrika mashariki ukiwakilisha Tasisi ya wachawi na waganga duniani

Tuambie Hii level ilotumia Farouk... ukizingazitia no casualities[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwenye kaliba ya uchawi na ulozi/ushirika kuna levels lakini pia kuna aina.. Yaani unataka aina gani ya level gani
Kuna aina ya kudhuru mwili ina level zake
Kuna aina ya kunasisha kuna level zake
Kuna aina ya usahaulifu kuna level zake
Kuna aina ya uono ina level zake
Kuna aina ya kuganda ina level zake
Kuna aina ya uchovu ina level zake pia

Aina aliyotumia Bwana Farouk ni hii ya uchovu daraja la kwanza.. Yaani baada ya kuiba mwizi anachoka mpaka analala hapo hapo akiwa na vidhibiti vyake.. Hapa pamoja na mengine vitu vinavyotumika ni pamoja na macho ya pono na manyoya ya fisi
Aina ya pili ni ya kuchoka baada ya kutoka eneo la tukio
Aina ya tatu ni ya kuchoka mwizi akifika kwake

Hiyo aina ya kudhuru pia ina level zake
Je unataka afe?
Je unataka adhurike kiungo au viungo?
Je unataka adhurike ufahamu?

Ya kunasisha ni ile ya kitu ulichoiba kukunasia mwilini
Ya usahaulifu ni kila ukifika nyumba husika unaisahau
Ya uono kila ukifika eneo la tukio huoni kitu ama unaona kitu kingine kabisa... Unaweza kuona msitu
Unaweza kuona bahari
Ama unaweza kuona uwanja tuu

Jr[emoji769]
 
View attachment 1467247
Ila huyu afande amejenga nje ya Beacon anatakiwa abomoe [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
[emoji30][emoji30][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Kwa nini waganga wasiweke hiyo Tech sokoni yaani itapunguza kwa kiwango kikubwa tabia ya wizi na ukwapuaji pia itawatajirisha hawa waganga na kua mabilionea kwa hali za maisha ya waafrika watapatikana customers wengi mno
Hiyo dawa wateja wake wakubwa ni wezi wenyewe... Unalazwa usingizi mzito.. Jamaa wanaingia mpaka chumbani kwako wanachukua kila kitu na kusepa.. Unastuka asubuhi nyumba nyeupee

Jr[emoji769]
 
Tunafanya makosa makubwa kabisa kwenye hili tunapofikia conclusion ya kuwa eti mwizi alikuwa teja... Teja halali akiwa kwenye uraibu ama akiwa kwenye mishe ya kuiba... Akishaiba na kwenda kuuza akapata dozi yake hapo ndio atalala hata mpaka kesho.. Lakini si kabla ya kutimiza mission.

Haya mambo yapo sana na watu wengi sana wanaibiwa majumbani kwa staili hii ya kulazwa usingizi wa pono... Hii imekuwa habari kwakuwa mtenda ndio katendwa.. Wateja wakubwa wa hii dawa ni wezi wa kuvunja majumba usiku.

Kuna wakati hii style ilikuwa maarufu sana.. Jamaa wanaingia wanaiba kila kitu.. Wanaweza hata kukutoa kitandani na kukuvueni nguo zote mkabaki uchi kama wakiamua kuwadhalilisheni... Wengine huzinduka alfajiri na wengine huja kuamshwa na majirani kukiwa kumepambazuka kabisa

Jr[emoji769]
 
NI kutokea visiwani Zanzibar ambapo kumetokea kisa cha Mwizi kusinzia eneo la tukio baada ya kufika nyumbani kufanya uhalifu, itazame hii video hapa ujionee nilichokuandalia ufahamu zaidi mkasa huo.
 

Attachments

  • B55F9F17-C08F-4F38-8262-02032337DD5E.jpeg
    B55F9F17-C08F-4F38-8262-02032337DD5E.jpeg
    26.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom