Fasihi ya Askofu Dkt. Benson Bagonza kuhusu Miafaka vs Muafaka

Fasihi ya Askofu Dkt. Benson Bagonza kuhusu Miafaka vs Muafaka

dada embu kunywa fanta hapo nakuja kukulipia aunt yangu, nasikia inasaidia kupunguza stress kdg
Unafikiri mimi nmezoea kunywa vinywaji vya watu kama wewe?

Hiyo ni tabia yako uliyotoka nayo nyumbani na unaishi hapa mjini kwa tabia hiyo tu.

Sasa malipo yake utayapata soon, we endelea kujilegembua kwa wanaume
 
Sahihi Mzee wetu.

Ongeza na hizi.

1. Kuna waabudu wachonga sanamu na wanaoabudu sanamu lenyewe, muafaka unahitajika aabudiwe anaestahiki.

2. Kuna makelele na zogo. Kelele nyingi huamsha zogo na zogo jingi sio kelele Hawa wapiga kelele na zogo wanahitaji muafaka.

3. Kuna wapambanaji waliopitwa na muda na kuna na muda unapambana na wakati. Muda hauwezi kushindana na wakati kamwe. Uje muafaka kwanza ili watu watambue kwamba wakati haukumbatiwi.

4. Kuna stress za maisha bila ajira na mipango ya Ajira bila stress. Stress za watu zinachanganywa na mipango ya ajira. Mara watu wanataka ajira za mipango, mara mipango ya ajira kupata ajira.

5. Kuna watu wa Mungu na Mungu Watu. Ajabu ni pale Mungu Watu wanavyoigiza ya Watu wa Mungu na kujibandika uso wa Kondoo.

6. Duniani kuna masokwe, kima, tumbiri na komba. Sokwe sio kima, na tumbiri sio komba(Bush Baby), Ifike wakati yajulikane mahitaji ya komba na Tumbiri, Sokwe na Kima. Tunahitaji Muafaka.

Asante Baba Askofu.
 
INAHITAJIKA MIAFAKA siyo MUAFAKA.

Kuna harufu ya mparaganyiko kila mahali. Ni kama tuna nchi moja yenye mataifa mengi ndani yake. Badala ya muafaka wa kitaifa, inahitajika miafaka kadhaa ili kuunda muafaka mmoja.

1. CCM si moja. Kuna CCM-Mpina na CCM-January. Kuna CCM-Mwendazake na CCM-Samia. Kuna CCM-Asili na CCM-Yatima. Hizi CCM zote zinahitaji muafaka ili tupate CCM moja.

2. Wapinzani si wamoja. Kuna wapinzani-Katiba Mpya na Wapinzani-Nusu Katiba Mpya. Kuna wapinzani-Mtungi na Wapinzani-Mahela. Kuna Wapinzani-Zanzibar huru na Wapinzani-Zanzibar Mkoa. Unahitajika muafaka kati ya wapinzani kabla ya muafaka wa kitaifa.

3. Serikali si moja. Kuna serikali awamu ya 5 rais wa sita na Serikali awamu ya sita rais wa sita. Kuna serikali-2025 na Serikali-2030. Hizi serikali zinahitaji muafaka.

4. Kuna bunge-live na bunge-giza. Kuna bunge-haramu ndani jengo halali na bunge-halali nje ya jengo halali. Kuna sheria halali zilizotungwa na bunge haramu.

5. Kuna Polisi-Tii sheria bila shuruti na Polisi-Tii shuruti bila sheria. Kuna IGP bila Polisi na Polisi bila IGP.

Unashangaa? Tanzania ni eneo la utalii. Kila kitu ni kiburudisho. Hatuambukizani Corona, tunaambukizana tabia. Mwenyekiti wa msiba anamuiga Spika namna ya kuongoza kikao cha mazishi. Askofu anamuiga OCD ili kuongoza kanisa. Kocha wa Simba anamuiga kocha wa Yanga lakini anafungwa mengi kuliko Yanga.

Bei ya mafuta imepandisha hata rushwa ya barabarani.
Pascal Mayalla wana wa lumumba sii mkubali mmeshindwaa miaka yote hii zaidi ya 50
 
Ni kweli kabisa, naiona CCM - Makamba na CCM - Mpina, ila CCM Makamba wasije kumtengenezea zengwe Mpina ili aondoke bungeni.

Kwani wanachelewa, wameishaanza kumwambia arudishe ekari 1000 za Ardhi ya Kijiji wanazosema alipora wananchi Mkoa wa Morogoro alipokwa Waziri wa Mwendazake!!! Kumbuka kuwa kule wizara ya Ardhi kuna KI-DOT kama naibu waziri na yeye ni team Makamba!! Ngoma inogile ccm!!!
 
Akili ya kibavicha?

Ndiyo ningekuwa mwehu maaana ukiwa na akili za kibavicha lazima uwe xhizi
Unavyoandika tu inaonekana akili yako ndogo. X= c ni sawa? Unafikiri kila mwenye mawazo kinzani ni bavicha! Kwani kuwa bavicha ni dhambi??? Wizi wa mitihani unawasumbua sana vijana
 
Unavyoandika tu inaonekana akili yako ndogo. X= c ni sawa? Unafikiri kila mwenye mawazo kinzani ni bavicha! Kwani kuwa bavicha ni dhambi??? Wizi wa mitihani unawasumbua sana vijana
Kuwa bavicha ni sawa na kuwa kuzimu
 
Yule ndiyo kiboko yenu nyie chawa wa lile fedhuli lililopigwa ngwara na corona
Fedhuli lako lilikubutua mpaka leo una hasira nalo!

Na bado hadi 2025 hangaya atawapelekea moto alafu utalilaumu fedhuli lako!

Fedhuli linakuchapa hata baada ya kufa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
INAHITAJIKA MIAFAKA siyo MUAFAKA.

Kuna harufu ya mparaganyiko kila mahali. Ni kama tuna nchi moja yenye mataifa mengi ndani yake. Badala ya muafaka wa kitaifa, inahitajika miafaka kadhaa ili kuunda muafaka mmoja.

1. CCM si moja. Kuna CCM-Mpina na CCM-January. Kuna CCM-Mwendazake na CCM-Samia. Kuna CCM-Asili na CCM-Yatima. Hizi CCM zote zinahitaji muafaka ili tupate CCM moja.

2. Wapinzani si wamoja. Kuna wapinzani-Katiba Mpya na Wapinzani-Nusu Katiba Mpya. Kuna wapinzani-Mtungi na Wapinzani-Mahela. Kuna Wapinzani-Zanzibar huru na Wapinzani-Zanzibar Mkoa. Unahitajika muafaka kati ya wapinzani kabla ya muafaka wa kitaifa.

3. Serikali si moja. Kuna serikali awamu ya 5 rais wa sita na Serikali awamu ya sita rais wa sita. Kuna serikali-2025 na Serikali-2030. Hizi serikali zinahitaji muafaka.

4. Kuna bunge-live na bunge-giza. Kuna bunge-haramu ndani jengo halali na bunge-halali nje ya jengo halali. Kuna sheria halali zilizotungwa na bunge haramu.

5. Kuna Polisi-Tii sheria bila shuruti na Polisi-Tii shuruti bila sheria. Kuna IGP bila Polisi na Polisi bila IGP.

Unashangaa? Tanzania ni eneo la utalii. Kila kitu ni kiburudisho. Hatuambukizani Corona, tunaambukizana tabia. Mwenyekiti wa msiba anamuiga Spika namna ya kuongoza kikao cha mazishi. Askofu anamuiga OCD ili kuongoza kanisa. Kocha wa Simba anamuiga kocha wa Yanga lakini anafungwa mengi kuliko Yanga.

Bei ya mafuta imepandisha hata rushwa ya barabarani.
Askofu nae ana mambo sana. Naona anataka kuupa nguvu isiyo na maaana mgogoro wa JM NA MPINA
 
Nilikuwa sijagundua kwamba ya kubrashia viatu na yenyewe imeathiriwa na vita ya yukreini.........bagonza noma.
 
Wengi wetu tunamiparaganyiko ndani ya nafsi zetu pia tunahitaji miafaka ndani ya nafsi zetu ndio maana baadhi yetu tunapinga andiko hili bila kutoa hoja za msingi. Tulizoea kutii shuruti bila sheria.
Amalize kwanza MIAFAKA ndani ya KKKT kila uchao migogoro.

Atoe kwanza Boriti kwenye jicho lake ili aone kibanzi cha wenzie.
 
Unafikiri mimi nmezoea kunywa vinywaji vya watu kama wewe?

Hiyo ni tabia yako uliyotoka nayo nyumbani na unaishi hapa mjini kwa tabia hiyo tu.

Sasa malipo yake utayapata soon, we endelea kujilegembua kwa wanaume
Relax dada angu, mafuta yamepanda bei unajua lkn??maana una stress sana shangazi yangu
 
Back
Top Bottom