Fastjet: Kwa wale mlikuwa mnadhani itakuwa msaada kwa watanzania, someni hapa.

Wabongo kwa majungu, hamtaki walalahoi wapande ndege jamani?
Na mleta mada anaongea bila ushahidi wowote, huenda hajui hata ladha ya pipa ikoje. By the way low cost airlines ndio mkombozi wa nchi nyingi za Ulaya, hapa tunaongelea kampuni kama Easy Jet, Ryanair, Cimber Airlines na kadhalika. Humo hata maji hupewi, wanachotoa wao ni usafiri tu.
 

Hakika na mende tena???
Ila leo kwenye magazeti nimeskia huko duniani kuna abilia amegongwa na nyoka ndani ya pipa
 
Last edited by a moderator:

Idimi hizo kampun ndo nazipenda
 
Last edited by a moderator:
Idimi hizo kampun ndo nazipenda

We cha tu. Nimepiga sana boksi za deiwaka toka nchi moja na nyingine kwa usafiri huo, hasa Cimber Airlines (enzi hizo ikiitwa Sterling Airlines) na SAS, halafu mwingine anakuja anaponda Fastjet bila kufanya upembuzi kwamba wengine nao wamepita njia hizo hizo.
Nimependa mfano wa mmojawetu hapo juu, aliyeongelea gharama kubwa za simu enzi hizo ndio zinaingia. Kupiga na kupigiwa ilikuwa lazima ulipe kwa dola, lkn makampuni yalipoongezeka kupokea simu ikawa bure na gharama sasa zimeshuka sana. Hata kwenye ndege, yakija makampuni mengi zaidi gharama zitashuka tu.
 
hapa ndio watz wengi na baadhi ya waafrika tunashindwa kusonga mbele kwa ile kitu inaitwa 'resistance to change'. Unajua mkuu kuna watu wameangaika sana, wameloga sana nk wakipigania kubakiza ajira zao RTC, Halmashauri, TRA, URAFIKI, ATC, Mawizarani and the like wakiamini kabisa kuwa hakuna maisha sehemu nyingine yoyote bila kuajiriwa katika hizo taasisi.
Laiti hawa wangelijua kuwa nje ya huo mfumo wa kifikra wangetokea mamilionea wa kuendesha hii nchi kwa kipato halali na kutoa ajira kwa watanzania wenzao (namaanisha wajasiriamali wanaolipa kodi leo)

 



mkuu kilo 20 ni standard, mkuu unataka upande hadi na viroba vya ndizi au unapeleka mchele kilo 50 moshi ambao tofauti ya bei kwa kilo moja dar na moshi ni Tsh 100! acha kuishi kwa mazoea boss. hawa jamaa ni wakombozi kwetu
 
Wateja wa PW wanalalamiiika, wao wenyewe wenye ndege wanajua ndo maana wameshusha bei. Wameshusha ya nn kama hawaogopi? Wamezoea monopoly na kunyanyasa abiria, check in ya domestic flight wanafanya sawa na international flight kisa kwa sababu wako peke yao. Wanafanya fitna na travel agent kuwaumiza competitors hasa TC. Nadhani muda umefika wabadilike, there is more to come. Karibu fast Jet the economy airline utukomboe na ubeberu wa PW.
 
kwa wate wanaoujua marketing strategy kunakitu kinachoitwa Introductory Marketing unanaza bishara yuko kwa kujiendesha kihasara for short time kwa mantik kuwa ukamate wateja na kuteka akiri zao,na wakishaingia katika bishara yako wakishakuwa aware na biashara yako unapandisha bei chini au zaidi ya competitors wako unaanza kujiendesha kifaida zaidi..kipindi hicho utakuwa na wateja wengi zaidi..na wanapofanya hivyo wamekwisha kuona..kuwa ni ngumu penetration(marketing penetration) into air market with the some the price with other competitors..

Faida ambayo wangeweza kuipata kwa 5 yrs wataipata for 2 or 3 yrs.

Makampuni makubwa duniani yaliyofanikiwa yanianza kwa strategy hii baadaye yakajiendesha kifaida zaidi.


Kunakitu kinaitwa S.W.O.T--nondo nyingine nitafute...
 

Mkuu nilikuwa bongo last year! nilishangaa, yaani PW ni kampuni ya ajabu, inajifanyia inavyotaka kwa abiria wake!!! Nikasema bado tunahitanji "low cos airlines" ili wapate adabu. I am happy FastJet have led the way!!!

Nasikia wameshusha bei ya DR-MWZ-DAR to 199,000 inclusive of all taxes! I am saying they are still high!!!

Go go go FastJet, let them feel the pinch!!:A S angry:
 
wewe mtoa mada nakushauri uachane na mambo ya vitabu na notisi za shuleni na vyuoni na pia story za mtaani,, nenda kanunue ticket ukirudi utajua kuwa ulikuwa chaka mbaaya,,, me nimemchukulia ticket m2 mmoja juz juz hapa from mwanza to dar then to mwanza,(yaan to and fro au go & return) total ikaja elfu 90, yupo dar sa hivi na amekubali fast jet iko poa........ sasa huo mchanganuo wako umeutoa wapi???


au we ni presicision/ air tanzania???
 
Ni kweli kabisa. Cha msingi hapa Precision na makampuni mengine yajipange na wao wapunguze bei. Bei zao ni juu sana kwenda Mwanza utadhani unakwenda India!
Tutaheshimiana tu hapa mjini sasa hivi.
 
Huwa natoka dar - mwanza na Atc kwa 398,000 na precission kwa 368,000 jaani trip moja kwa 198,000 mkp 200,000 hawa jamaa hata wangesema 100,000 bado wangekuwa cheap, hayo mahesabu uliyotoa hapo hayaeleweki kajipange tena
 
Huwa natoka dar - mwanza na Atc kwa 398,000 na precission kwa 368,000 jaani trip moja kwa 198,000 mkp 200,000 hawa jamaa hata wangesema 100,000 bado wangekuwa cheap, hayo mahesabu uliyotoa hapo hayaeleweki kajipange tena
Achana na vibaraka wa Precision wanawewe hao. Taarifa nilizo nazo hawa jamaa Fast Jet muda wowote kuanzia sasa wanaingiza Air bus mbili na ATR moja.

Kuna madai kwamba hii ni kuwavuta wateja ila baada ya miezi 3 bei itapanda na kuwa sawa na wengine, na mimi nasema hivi wakipandisha bei na kuwa sawa na wengine na sisi tunarudi kwenye mabasi yetu kama zamani.
 

Hiyo gharama bado ni chini sana kulinganisha na Precision Air. Hizi ndege ni kwa ajili ya watu wanaofanya biashara au safari za muda mfupi. Ni mtindo huo huo wa kulipisha mizigo wanafanya EasyJet na Rynair. Mtu kama unakwenda Mwanza kwa mkutano na kurudi Dar, unahitaji mabegi ya nini. Kama unaenda Holiday Mwanza kwa siku nne mabegi mazito ya nini. Wenzetu ndo wanavyofanya. Kwa EasyJet and Ryanair hakuna kupangiwa seat, unawahi kupata seat, ukitaka chai au kahawa unanunua, lakini bado ni usafiri wa bei nafuu na watu wanautumia sana.
 
Kuna watu hawapendi mabadiliko aisee!!
wanataka wabaki wao tu.
 

Tutaanza kushika mabomba kwenye ndege muda si mrefu. hahahaha kweli watanzania mnapenda vya bure!
 


Fastjet ni 'no-frills/low -cost carrier. Hizo marketing rhetoric unazoongea na mambo ya 1st year. Jaribu kutafiti low-cost carriers zinafanye kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…