Fastjet: Kwa wale mlikuwa mnadhani itakuwa msaada kwa watanzania, someni hapa.

Fastjet: Kwa wale mlikuwa mnadhani itakuwa msaada kwa watanzania, someni hapa.

kampuni za mabasi ya mikoani endapo watapandisha nauli wajiandae kubeba mabegi yatakayotumwa kama parcel ,abiria wengi wtapanda ndege kwenda na kurudi hii ni changamoto fast jet waongeze ndege biashara ipo .
 
Kwani hawaruhusu mtu kupanda na chapati zake?
hili ni tatizo letu lingine, safari ya dakika 45 - saa 1 na dakika 25 hivi unakuwa na njaa gani hiyo!?
Si ajabu kukuta mtu kwenye daladala mara kituo cha kwanza utasikia "maji, maji, maji ...lete", kituo chapili "kalanga, kalanga, ....lete" nk Na unashangaa mtu asiyeweza kumudu kutoka Mbagara-Kariakoo bila kulakula njiani!
 
Ukiacha ushabiki wa kibiashara na ushabiki kama wa waumini wa huduma moja. Mimi naona usafiri kwa Fast jet ni ukombozi, tunaomba isifanyiwe hujuma kama waleeeee, tunawakumbuka.

- bei ni sh 32000
- Bei yao ukiongeza na VAT (kwa wale wasiorudishiwa) ni kama 45000 au chini ya hapo,
- kama unataka chakula, menu ba bei utapewa
- kama una mzigo 8000 kwa 20kg za kwanza
- kama una zaidi 8000 kwa kila kilo ya ziada

kuna siri gani kuficha haya? Lazima tujue hizo breakdowns

pima mwenyewe, wenzio tumekata ticket za familia kwa bei ya ticket ya mtu mmoja ya precision.
Tunaipenda preciosion ila lazima wakubali changamoto, wasianze kujisifia kwa kuwakashifu wenzao, soko sasa ni lao, inabidi wagawane. Wajenge imani kwa kazi yao,


Wawaue mende kwenye ndege zao, tunaogopa kula mikate kwa uwezekano kuwa imetembelewa na mende jamani hawana hela ya Expell
Mkuu ya nini kuandikia mate wakti wino upo, Fast Jet wameweka kila kitu kwenye mtandao wasiliana nao!! Wanawapa changamoto Precision Air!!

 
Tutaanza kushika mabomba kwenye ndege muda si mrefu. hahahaha kweli watanzania mnapenda vya bure!
Wewe sasa ni mgonjwa unashushiwa nauli unadai Watanzania wanapenda vya bure, huoni kuna unafuu mkubwa kwa nauli ya Dar kwenda na kurudi Tshs 90,000/=???? Hiyo ndio biashara watu wameona kuna chance ya kuteka soko la usafiri wa anga TZ, KARIBUNI FAST JET Mkombozi!!!

 
Nilikuwa miongoni mwa abiria wa kwanza kupanda ndege yao ya kwanza kabisa kuruka kwenda Mwanza trh 29Nov na nimerudi Dar Leo unayoyasema sio kweli mimi nimelipa 86K go and Return na nilikuwa na kabegi kadogo tu ka mgongoni sijakalipia hata sh kumi na service zao ni nzuri sana wale wazungu wamejipanga na ni mkweli ni mkombozi kwetu japokuwa kupata hiyo bei lazima ufanye booking mapema ukichelewa bei inakuwa juu japokuwa sio kama Precision air.
 
Hebu kwa uwazi fanya mchanganuo unavyojua wewe kwa airline zote mbili utuambie, ipi ni rahisi.
halafu jaribu kuwaza, je wale frequent fliers, wanakuwa na mizigo kiasi gani?
na wenye mizigo wanasafiri mara ngapi kwa mwaka??
Kama wewe namimi wote tunazo ticket au quotations zote mbili nadhani tunajua ipi ni cheaper, au sio??

Lakini kuwa bei rahisi sio kigezo cha kupendwa
Kuna wale watakaobaki na uaminifu kwa Precision kwa sababu nyingi sana.

sidhani kama soko lao litayumba, wana mambo mengi tu mazuri ikiwapo mtandao mkubwa, uzoefu, connection-watu muhimu Tanzania-si unajua (know-who)

Wanayo mengi mabaya pia:
Wafanyakazi kwenye ndege ni wachafu, uniform zao ni chakavu
Wameanza kuwa na cancellations na delays nyingi
Walibweteka, sasa wamepata mshindani watashikishwa adabu
 
wewe utakuwa umetumwa,tena na preshishen!majungu tu!
 
eeee hizi ndege zikiongezeka na uwanja wa mwanza uendelezwe mbona uchumi utakua maaana mtu kuliko kuzunguka na gari masaa anatumia saa moja unusu hadi aendapo.
Wameleta challenge hadi Precision kapunuza bei ya Mwanza na kupeleka Boeing yake mara tatu kwa siku

Ushindani mzuri aisee. Kuna siku nilinunua tiketi ya DAR-MZA-DAR kwa precision nikawaambia wanipangie tarehe na saa ambazo safari zangu zitafanywa na Jet, wakakubali. Siku nasafiri wanatuambia Boeing mbovu kumbe inapiga ruti za Nairobi. Kuna jamaa mmoja yeye ndo walimwibia kabisa maana alikuwa amenunua tiketi ya bussiness class na ile ATR tuliyosafiri nayo ilikuwa ya daraja moja tu yaani haina sehemu ya bussiness class.
 
Spot on mkuu hata mimi nilitaka kutoa mfano huo huo, actually nafikili FastJet hiko affiliated na moja wapo ya kampuni ulizo taja hapo juu na zinafanya kazi bila wasi wasi na wanapata faida. Big Up Mkuu, mimi wasi wasi wangu nikufanyiwa hujuma na mizengwe na mapapa, abiria watapatikana kwa kuwa nauli haijazidiana sana na ya mabasi, we sema hata wamiliki wa mabasi wanaweza kuwafanyia hujuma. Ninacho washauri wawe wangalifu wanako nunua mafuta ya ndege yanaweza kuchakachuliwa kukatokea catastrophe.

Pamoja sana mkuu. Kwenye suala la mafuta nafikiri kuna kampuni maalum ya kunywesha ndege mafuta kwenye airports zetu (japo Bongo kila kitu kinawezekana), GOD forbid.
 
MIm nadhani hizo bei za FastJet ni za muda tuu! I mean, ile promotion ya elf 32 itakwisha very soon. Wiki hii nilitaka ticket ya kutoka Mza kuja Dar, nikaambiwa zimekwisha - zile za 32k. Lakini nilipojaribu kununua tokea Dar nimelipa Tzs 107,000! Kisha nikalipa elf 8 kwa begi, jumla 115,000, nina imani kama nilihitaji kula chakula ingependa hadi Tzs 125,000! Precision wanazo za tiketi za Tzs 139,000! Uhitaji kusumbuliwa pembeni kuangalia tiketi na kulipia tiketi mzigo wako (actually airlines nyingi hata za kimataifa at least 20kg is a standard kwa msafiri uwe unasafiri mara ya kwanza ama ni frequent flier). So, the difference will be only Tz 14,000! Sidhani kama wako cheap that way hao wa FastJet kama ambavyo we are made to believe.
Mkuu ya nini kuandikia mate wakti wino upo, Fast Jet wameweka kila kitu kwenye mtandao wasiliana nao!! Wanawapa changamoto Precision Air!!

 
fastjet, easyjet na ryanair kampuni hizi ni cheap sana kwa usafiri wa ndege uk pamoja na mchanganuo huo uliosema bado suala la gharama nafuu uko pale pale ukilinganisha na makampuni ya mengine ya ndege kwa mfano kipindi hiki kutoka birmingham kwenda paris unalipa £40 ni bei ya kutupwa makampuni mengine hayacharge hivi, mleta hoja pamoja na kusema sisi watanzania hatujui mahesabu ya kujua gharama halisi ila ukweli hii ni changamoto kubwa imeletwa hasa kwenye industry ya ndege na precision air inabidi wazikabili changamoto hizi kwa vitendo na sio kwa porojo kwenye media maana tunasifika sana kwa kuongea bila matendo, kama mtakumbuka mobile zimeanza kuingia nchini vodacome walikuwa wanauza line pekee tu kwa tsh 15,000/= na gharama ilikuwa kubwa kweli yalipoongezeka makampuni mengine gharama zikaanza kupungua mpka line unapata bure na gharama za mawasiliano zilipungua, ukweli precision walikuwa wanapata profit za kutosha sasa hivi wameona hizo changamoto maneno yameanza, pigeni kazi ni sisi wenyewe tuliruhusu biashara huria na uzuri ni shirika la nje lingekuwa na mtz watu wangesema ni la mafisadi.


Mimi line ya Vodacom nilinunua tshs 22,500 enzi hizo. 15,000 ni juzi sana mkuu.
 
Tutaanza kushika mabomba kwenye ndege muda si mrefu. hahahaha kweli watanzania mnapenda vya bure!

Hongera wewe unayependa vya bei. Trust me, hata wewe ni negotiator mzuri sana ukienda kufanya shopping li upunguziwe bei. Sasa hapo. Sijui ni bure, ama umejenga mafufu zaidi. Bure navyoelewa huchangii chochote.
 
Hiyo nauli ya elfu 32 ipo kweli? Leo nimetembelea mtandao wao sijaiona. Nauli ya chini kabisa Dar-KIA-Dar ni 218,000/-.
Hatuwalinganishi na Presion bali uongo uliopitiliza. Precision walipoanza safari za South Africa kwa USD 70 ilikuwa kweli kabisa, sio hawa Fastjet.

Mkuu ticket za ndege zinaenda na season. Ukikata mapema bei huwa chini. Lakini ukikata leo na kutaka kuondoka kesho tegemea kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali. Plan your trip in advance. Kama unaondoka January mwisho siyo vibaya uka book sasa ticket yako, na utaona nauli iko chini. Faster faster zinafaa wakati wa emergency, na wao ndiyo wanatengeneza pesa.
 
rmashauri ukiona business ambayo mtu ni dominant hakika yeye anaweza amua kufanya kile atakacho ila kama ushindani upo faida kwa wateja mfano sasa ni mtu kuchagua apande ipi
Precision tatizo lake ni kuwa na ndege nyingi ila anafanya kazi zake kienyeji kama mganga.
Anatakiwa apunguze bei maana route zake ni nyingi sana laa sivyo hawa Fastjet hakika watamkimbiza kwenye soko hili.
 
Last edited by a moderator:
rmashauri ukiona business ambayo mtu ni dominant hakika yeye anaweza amua kufanya kile atakacho ila kama ushindani upo faida kwa wateja mfano sasa ni mtu kuchagua apande ipi
Precision tatizo lake ni kuwa na ndege nyingi ila anafanya kazi zake kienyeji kama mganga.
Anatakiwa apunguze bei maana route zake ni nyingi sana laa sivyo hawa Fastjet hakika watamkimbiza kwenye soko hili.
 
Last edited by a moderator:
Kweli asiyejua maana haambiwi maana.Hawa fastjet ni wafanyabiashara kama wengine tu.Kama unaelewa kuwa tiketi za ndege huwa zinaenda na season huwezi pata shida hata kidogo.Wao wako kibiashara na sasa ile promotion yao ya 45,000/=nadhani tutaisikia kwenye matangazo yao tu.Nilienda ofisi zao Mwanza tarehe 03/12/2012 nikitaka booking ya "round trip" kama waitavyo wao,wengi tumezoea inaitwa return ticket to Dar ya kuruka mwanza tarehe 20/12 na kurudi tarehe 17/01/2013 wakanifanyia mahesabu na jibu likaja ni 249,000/=na one way ni 107,000/= nafuu iko wapi......?watanzania tujue kuwa biashara haina urafiki.Wamekuja huku kuchuma ila cha msingi watasaidia kuongeza ubora na kuondoa"uswahili"wa baadhi ya mashirika yanayo-cancel trip kihuni utadhani hizo safari wametutuma wao ama wametulipia
 
mimi kama mmoja wa watu wanaosafiri sana niliposikia huduma mpya za fastjet tanzania kwa gharama nafuu ya Tsh 32000 nikasema mkombozi kafika Tanzania kwa watu wa Dar-Mwanza na KLM. Nikasema hvi kama napanda dar express dar to arusha kwa Tsh 28000 kwa masaa karibu kumi, leo naambiwa natumia Tsh32000 tu kwa muda wa saa 1 na dk kama 20 hv, kwanza nilistaajabu ktk hali iliyonifanya nijaribu kufanya utafiti wa hiyo fare yao.nilianza kwa kutembelea website yao ktk booking category.nilipoona jinsi mchanganuo wa cost yao ulivyo nikasema jamaa wameshajua kuwa watanzania ni watu wasiojua kufatilia jambo. Iko hivi fare exclusive vat and other cost ni Tsh 32000, ukibeba kabag kadogo utakalipia Tsh 8000, bag lisilozidi Kg 20(sport bag) utalilipia Tsh 32000. sasa hapa acha hiyo VAT ambayo ikianza kulipwa utalipa wewe, airport charge ambayo ni Tsh 10000.fanya sum utaona how much you should pay. kwa mantki hiyo watanzania hapa tumejidanganya wenyewe kwani kilichotumika ni busness tricks ktk kuvuta mind za clients. ndo mana kama mtafatilia gazeti la The Citizen la ijumaa iliyopita kama sikosei kuna mwakilishi toka precision airline kaelezea sana ktk hili na mwisho akasema hivi " Haitachukua muda kwa Watanzania kuelewa gharama halisi watakayolipa kwani ktk biashara hii ya usafiri utagundua gharama za uendeshaji zipo sawa na 40% ya mapato hutumika ktk oil" akaendelea kwa kusema hajaona drop down yoyote ktk booking yao kwa maana kuwa hawajaathiriwa vyovyote vile na ujio wa Fastjet zaidi ya kupata changamoto zaidi ktk uboreshaji wa huduma zao.
My take:
Ni wazi kuwa wenye ufahamu zaidi ktk huduma za usafiri wa anga wamegundua kuwa kama kuna diffence basi itakuwa ndogo na si kama inavyotamkwa na watu ktk vyombo vya habari. so tuwe tunasoma angalau watanzania wenzangu maana kila jambo ni sisi tu watanzania tunadanganywa thats too sad kusema kuwa hata wawekezaji wamegundua watanzania wengi ni mbumbumbu ktk masuala yanayowahusu wenyewe.
Hili ndo tatizo la kuandika maada huku upo ndumu. Kwanza unakiri kuwa Fastjet wapo cheaper than precision so badala ya kushukuru kwa hiyo tofauti ndogo ndo kwaanza unakuja hadithi za mizigo kilo zaidi 20. Wewe umeambiwa hiyo ni ndege ya mizigo..!? Pambafu..!
 
Sina hakika na nauli lakini hii tabia ya KUDANGANYWA imezidi mno. Tunaambiwa ving'amuzi vinapatikana nchi nzima wakati SIO, hivi hawa watu HAWAMUOGOPI MUNGU?
Usinichekeshe ndugu yangu!ikifika Disemba 31!Analogia itazimwa na kuwasha Digitali wakati huko kwetu Lukange hakuna hiyo Mitambo!tunapenda kuendesha mambo kimabavu huku tukijua tunayosema hayatekelezeki!
 
Wanayo mengi mabaya pia:
Wafanyakazi kwenye ndege ni wachafu, uniform zao ni chakavu
Wameanza kuwa na cancellations na delays nyingi
Walibweteka, sasa wamepata mshindani watashikishwa adabu
Hapo kwenye sare wangewaazima Shirika letu la ndege sidhani zile za kwao zilizo shoneshwa nje kama zimeshatumika vilivyo!
 
Back
Top Bottom