Fastjet: Kwa wale mlikuwa mnadhani itakuwa msaada kwa watanzania, someni hapa.

kampuni za mabasi ya mikoani endapo watapandisha nauli wajiandae kubeba mabegi yatakayotumwa kama parcel ,abiria wengi wtapanda ndege kwenda na kurudi hii ni changamoto fast jet waongeze ndege biashara ipo .
 
Kwani hawaruhusu mtu kupanda na chapati zake?
hili ni tatizo letu lingine, safari ya dakika 45 - saa 1 na dakika 25 hivi unakuwa na njaa gani hiyo!?
Si ajabu kukuta mtu kwenye daladala mara kituo cha kwanza utasikia "maji, maji, maji ...lete", kituo chapili "kalanga, kalanga, ....lete" nk Na unashangaa mtu asiyeweza kumudu kutoka Mbagara-Kariakoo bila kulakula njiani!
 
Mkuu ya nini kuandikia mate wakti wino upo, Fast Jet wameweka kila kitu kwenye mtandao wasiliana nao!! Wanawapa changamoto Precision Air!!

 
Tutaanza kushika mabomba kwenye ndege muda si mrefu. hahahaha kweli watanzania mnapenda vya bure!
Wewe sasa ni mgonjwa unashushiwa nauli unadai Watanzania wanapenda vya bure, huoni kuna unafuu mkubwa kwa nauli ya Dar kwenda na kurudi Tshs 90,000/=???? Hiyo ndio biashara watu wameona kuna chance ya kuteka soko la usafiri wa anga TZ, KARIBUNI FAST JET Mkombozi!!!

 
Nilikuwa miongoni mwa abiria wa kwanza kupanda ndege yao ya kwanza kabisa kuruka kwenda Mwanza trh 29Nov na nimerudi Dar Leo unayoyasema sio kweli mimi nimelipa 86K go and Return na nilikuwa na kabegi kadogo tu ka mgongoni sijakalipia hata sh kumi na service zao ni nzuri sana wale wazungu wamejipanga na ni mkweli ni mkombozi kwetu japokuwa kupata hiyo bei lazima ufanye booking mapema ukichelewa bei inakuwa juu japokuwa sio kama Precision air.
 

Wanayo mengi mabaya pia:
Wafanyakazi kwenye ndege ni wachafu, uniform zao ni chakavu
Wameanza kuwa na cancellations na delays nyingi
Walibweteka, sasa wamepata mshindani watashikishwa adabu
 
wewe utakuwa umetumwa,tena na preshishen!majungu tu!
 

Ushindani mzuri aisee. Kuna siku nilinunua tiketi ya DAR-MZA-DAR kwa precision nikawaambia wanipangie tarehe na saa ambazo safari zangu zitafanywa na Jet, wakakubali. Siku nasafiri wanatuambia Boeing mbovu kumbe inapiga ruti za Nairobi. Kuna jamaa mmoja yeye ndo walimwibia kabisa maana alikuwa amenunua tiketi ya bussiness class na ile ATR tuliyosafiri nayo ilikuwa ya daraja moja tu yaani haina sehemu ya bussiness class.
 

Pamoja sana mkuu. Kwenye suala la mafuta nafikiri kuna kampuni maalum ya kunywesha ndege mafuta kwenye airports zetu (japo Bongo kila kitu kinawezekana), GOD forbid.
 
MIm nadhani hizo bei za FastJet ni za muda tuu! I mean, ile promotion ya elf 32 itakwisha very soon. Wiki hii nilitaka ticket ya kutoka Mza kuja Dar, nikaambiwa zimekwisha - zile za 32k. Lakini nilipojaribu kununua tokea Dar nimelipa Tzs 107,000! Kisha nikalipa elf 8 kwa begi, jumla 115,000, nina imani kama nilihitaji kula chakula ingependa hadi Tzs 125,000! Precision wanazo za tiketi za Tzs 139,000! Uhitaji kusumbuliwa pembeni kuangalia tiketi na kulipia tiketi mzigo wako (actually airlines nyingi hata za kimataifa at least 20kg is a standard kwa msafiri uwe unasafiri mara ya kwanza ama ni frequent flier). So, the difference will be only Tz 14,000! Sidhani kama wako cheap that way hao wa FastJet kama ambavyo we are made to believe.
Mkuu ya nini kuandikia mate wakti wino upo, Fast Jet wameweka kila kitu kwenye mtandao wasiliana nao!! Wanawapa changamoto Precision Air!!

 


Mimi line ya Vodacom nilinunua tshs 22,500 enzi hizo. 15,000 ni juzi sana mkuu.
 
Tutaanza kushika mabomba kwenye ndege muda si mrefu. hahahaha kweli watanzania mnapenda vya bure!

Hongera wewe unayependa vya bei. Trust me, hata wewe ni negotiator mzuri sana ukienda kufanya shopping li upunguziwe bei. Sasa hapo. Sijui ni bure, ama umejenga mafufu zaidi. Bure navyoelewa huchangii chochote.
 

Mkuu ticket za ndege zinaenda na season. Ukikata mapema bei huwa chini. Lakini ukikata leo na kutaka kuondoka kesho tegemea kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali. Plan your trip in advance. Kama unaondoka January mwisho siyo vibaya uka book sasa ticket yako, na utaona nauli iko chini. Faster faster zinafaa wakati wa emergency, na wao ndiyo wanatengeneza pesa.
 
rmashauri ukiona business ambayo mtu ni dominant hakika yeye anaweza amua kufanya kile atakacho ila kama ushindani upo faida kwa wateja mfano sasa ni mtu kuchagua apande ipi
Precision tatizo lake ni kuwa na ndege nyingi ila anafanya kazi zake kienyeji kama mganga.
Anatakiwa apunguze bei maana route zake ni nyingi sana laa sivyo hawa Fastjet hakika watamkimbiza kwenye soko hili.
 
Last edited by a moderator:
rmashauri ukiona business ambayo mtu ni dominant hakika yeye anaweza amua kufanya kile atakacho ila kama ushindani upo faida kwa wateja mfano sasa ni mtu kuchagua apande ipi
Precision tatizo lake ni kuwa na ndege nyingi ila anafanya kazi zake kienyeji kama mganga.
Anatakiwa apunguze bei maana route zake ni nyingi sana laa sivyo hawa Fastjet hakika watamkimbiza kwenye soko hili.
 
Last edited by a moderator:
Kweli asiyejua maana haambiwi maana.Hawa fastjet ni wafanyabiashara kama wengine tu.Kama unaelewa kuwa tiketi za ndege huwa zinaenda na season huwezi pata shida hata kidogo.Wao wako kibiashara na sasa ile promotion yao ya 45,000/=nadhani tutaisikia kwenye matangazo yao tu.Nilienda ofisi zao Mwanza tarehe 03/12/2012 nikitaka booking ya "round trip" kama waitavyo wao,wengi tumezoea inaitwa return ticket to Dar ya kuruka mwanza tarehe 20/12 na kurudi tarehe 17/01/2013 wakanifanyia mahesabu na jibu likaja ni 249,000/=na one way ni 107,000/= nafuu iko wapi......?watanzania tujue kuwa biashara haina urafiki.Wamekuja huku kuchuma ila cha msingi watasaidia kuongeza ubora na kuondoa"uswahili"wa baadhi ya mashirika yanayo-cancel trip kihuni utadhani hizo safari wametutuma wao ama wametulipia
 
Hili ndo tatizo la kuandika maada huku upo ndumu. Kwanza unakiri kuwa Fastjet wapo cheaper than precision so badala ya kushukuru kwa hiyo tofauti ndogo ndo kwaanza unakuja hadithi za mizigo kilo zaidi 20. Wewe umeambiwa hiyo ni ndege ya mizigo..!? Pambafu..!
 
Sina hakika na nauli lakini hii tabia ya KUDANGANYWA imezidi mno. Tunaambiwa ving'amuzi vinapatikana nchi nzima wakati SIO, hivi hawa watu HAWAMUOGOPI MUNGU?
Usinichekeshe ndugu yangu!ikifika Disemba 31!Analogia itazimwa na kuwasha Digitali wakati huko kwetu Lukange hakuna hiyo Mitambo!tunapenda kuendesha mambo kimabavu huku tukijua tunayosema hayatekelezeki!
 
Wanayo mengi mabaya pia:
Wafanyakazi kwenye ndege ni wachafu, uniform zao ni chakavu
Wameanza kuwa na cancellations na delays nyingi
Walibweteka, sasa wamepata mshindani watashikishwa adabu
Hapo kwenye sare wangewaazima Shirika letu la ndege sidhani zile za kwao zilizo shoneshwa nje kama zimeshatumika vilivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…