Fastjet ni kero tupu!

Fastjet ni kero tupu!

Habari zenu wanajamvi,

Kuna baadhi ya mambo yananichanganya kuhusu hawa fastJet,

1.Bei zao wanazotutangazia hazina ukweli wowote na hazikaribiani na ukweli,
Mfano leo kwenye website yako wamatutangazia ndege yao ya kwanza kutoka Dar kwenda KIA ni tsh32,000 ,nimepiga simu wanasema ni Tsh107000=.

2.Ukichelewa hata dakika moja baada ya reporting time hawakujui,kwani wameshachukua chao,wanakunyima safari.Hii imemtokea jamaa yangu mmoja leo jioni,walikuwa zaidi ya abiria 8 lakini hawakuwasikiliza zaidi ya kuwapa majibu ya kukatisha tamaa na kejeli,

3.majibu yao kwa ujumla wanaonekana kama abiria wanaopanda hiyo ndege wanapanda bure,au ni kama msaada flani,hawamthamini abiria kabisa,


4.Watanzania wenzangu tunaofanya hapo fastjet na wateja ebu jaribuni kuipa thamani pesa yetu ilingane na huduma tunayopewa na tunayotoa kwa wateja,hatuhitaji msaada wenu,

Mwenye kero kama zangu tiririka hapa

tusiwalaumu Fastjet kiukwel hata precision pia hayo mambo yapo wameanzisha ndege ya mbeya 249,000 lakini unaambiwa ndege imejaa zipo seat za 390,000 me nadhani nikufanya booking mapema sio ya papo kwa papo na tuamke sasa watanzania sio unangoja dk za majeruhi ndo wakimbilia airport kwan kumbuka pia wao wanatenga muda wakucheck ticket na mengineyo sasa wanapofunga counter ndo unafika sijui watafungua counter mara ngapi.
 
unadhihirisha ujinga wako. reporting time ni masaa mawili kabla ya ndege kuondoka. alafu wakakuandikia mara 4 kwamba check in closes 40 minutes before depature, sasa wewe ulikua wapi mda wote huo hadi kuchelewa dakika moja?....uzembe wako.!!
 
Rahisi huumiza! Nilisema humu wajuaji wa kusema wakanikandia, hakuna ada ya 32,000 kwa umbali wote huo!
 
Unalipa 32000 au hata 100,000,kwenda kurudi kj na unachelewa???nyie ndio wapuuzi wote 8,mshafanya hilo daladala.basi la mkoa lenyewe halisubiri abiria itakua ndege.nawapa sifa hao staff maana wangewaendekeza nyie itakuwa taabu mtataka hata kutumiwa gari nyumbani kuwachukua na buku 30 zenu nyambaf.


U made my evening! Waambieeeeee

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakuu unapoingia mkataba wowote ule soma masharti.
 
whilst I am not the spokesperson of fastjet, I would like to warn all those who travel with LCCs that these companies make profits from 1) no frills services,2) lighter aircraft by being strict on luggage, filling aircraft with the fuel at the best take off weight possible (therefore save fuel), tighter seat pitch (you notice there is no business class etc, and the seat pitch is just enough for you to sit) etc, etc, but also "fast turnaround times" to make the maximum utilization of aircraft, So planing and deplaning has to be swift. To them even half a minute delay means lost profits. Tanzanians should understand that that is what the LCC business model dictates
 
Pole sana mojaone kwa yaliyo kukuta.
fastjet toka tumeanza safari zetu nchini, tumekuwa na rekodi nzuri ya kuwahi kuanza safari na kufika ndani ya muda muafaka. tumeweza kufanikisha yote haya kwa sababu abiria wanawahi kufika airport. hatujawahi acha abiria hata siku moja aliyewahi. muda wa chek in unaisha dakika 40 kabla ya saa ya ndege kuanza safari yake hivyo unashauriwa kila mara hata kweenye ticket tunaandika ufike masaa mawili kabla.
Na kuhusu nauli, matangazo yetu yanasema nauli inaanzia 32000 bila ushuru ambao ni 11000 jumla yake inakuwa 43000 na kuendelea, haimaanishi nauli ni fixed hapana, tuna class ya nauli nyingi ambazo ni nafuu sana sana.

WELCOME ONBOARD
 
Habari zenu wanajamvi,

Kuna baadhi ya mambo yananichanganya kuhusu hawa fastJet,

1.Bei zao wanazotutangazia hazina ukweli wowote na hazikaribiani na ukweli,
Mfano leo kwenye website yako wamatutangazia ndege yao ya kwanza kutoka Dar kwenda KIA ni tsh32,000 ,nimepiga simu wanasema ni Tsh107000=.

2.Ukichelewa hata dakika moja baada ya reporting time hawakujui,kwani wameshachukua chao,wanakunyima safari.Hii imemtokea jamaa yangu mmoja leo jioni,walikuwa zaidi ya abiria 8 lakini hawakuwasikiliza zaidi ya kuwapa majibu ya kukatisha tamaa na kejeli,

3.majibu yao kwa ujumla wanaonekana kama abiria wanaopanda hiyo ndege wanapanda bure,au ni kama msaada flani,hawamthamini abiria kabisa,


4.Watanzania wenzangu tunaofanya hapo fastjet na wateja ebu jaribuni kuipa thamani pesa yetu ilingane na huduma tunayopewa na tunayotoa kwa wateja,hatuhitaji msaada wenu,

Mwenye kero kama zangu tiririka hapa

Kama kweli ulichelewa kwa dakika moja, basi wana haki kuwa ulichelewa. ATCL unaweza kuchelewa unavyotaka ndio maana ni kampuni hovyo, inawezekana una point nzuri, lakini ya kusumbuliwa na kukejeliwa baada ya kuchelewa, inawezekana wana haki. Post yake ingekuwa na maana zaidi kama ungewahi kuliko kuchelewa.
 
sasa wewe unakata tiket kwa sh 37000 au 107000,halafu unachelewa,unafikiri ni daladala hilo? jifunzeni kwenda na muda,kwa hiyo kwa akili zenu mlitaka wawape ndege ingine iwapeleke? acheni zenu hizo ndio maana ikaitwa fastjet,ukichelewa imekula kwako!
 
:smile: hahaaaa galoreeeee..time is very important 1 minute inaezakua na thamani ya 10,000 au 100,000..dakika moja ulochelewa inakula 107,000 yako jua muda nao ni pesa...tutajifunza tuu maana ya time is money msijali ndugu zangu poleni kwa hayo ndo mambo ya analog to digital mdogo mdogo mpaka mtazoea na kieleweke...ila international flight kufungua counter kwa ajili ya delay yako mwenyewe hapo nakataa..nafanya sana kazi za transfer za hapa .i.c.t.r (u.n) hakunaga kitu kama hicho ndugu yangu:shut-mouth:
 
Hawa ni wasanii kinyama.Ukitaka kuwajua,airisha safari yako utaona,na hasa ukiwa umelipa kwa MPESA.Utasikia mtandao unasumbua,hapa utakaa hata miezi miwili bila kurudishiwa haki yako.
 
Back
Top Bottom