Sasa kati yangu mimi na wewe nani analeta story za vijiwe vya kahawa
Moja;Simba hakuna mchezaji anayedai,wachezaji ambao hawakwenda kanda ya ziwa walisimamishwa kwa utovu wa nidhamu na uongozi ulishalitolea ufafanuzi hilo swala
View attachment 1246456View attachment 1246457
Sasa tuambie wewe uko kwenye vijiwe vyenu vya kahawa walikudanganya nani na nani wanadai na wanadai shilingi ngapi na ni lini hao wachezaji walithibitisha kuwa wanadai kwenye chanzo/chombo chochote cha habari cha kuaminika.
Mbili;Unasema kaunda kwa sasa hakuko ivyo,mara ya mwisho dar ulikuja lini mkuu?...wiki iliyopita mvua imenyesha sana hali iliyokuwa pale kaunda kwa sisi tunaopita kila siku pale maji yamejaa,uwanja hauonekani kabisa...sasa iyo kaunda unayoisema wewe kuwa sikuhizi haipo ivyo unaisema ipi mkuu...ukiweka picha inayoonesha kaunda ya siku hizi ilivyo itapendeza zaidi
Labda nikusaidie tu mkuu,kwa sababu huenda nazungumza na mtu ambaye hajawahi fika na kuuona huo uwanja na sio mwenyeji wa dar,uwanja wa kaunda upo eneo korofi ambalo mvua zikinyesha kidogo basi mafuriko na maji yanajaa kulifunika kabisa eneo lote kama unavyoona kwenye hizo picha,juzi kati mwezi wa saba kuna greda niliona linatinduatindua na kusawazisha hapo kaunda but mvua ilivyonyesha yamerudi yaleyale....but mkuu kwa akili zako hilo eneo kwenye picha hapo unaweza kujenga uwanja wa mpira??mvua zikinyesha mtakuwa mnacheza kwenye mafuriko/dimbwi la maji????
Mwisho;hiyo mikataba ya udhamini mnayosema mnapiga hela nyingi mnayoingia na makampuni mbona haiwekwi hadharani mnaishia tu ku sign gizani...kama sio pesa kupigwa na wajanja wachache
Mashabiki wa yanga naona mnajitutumua sana kuonyesha kuwa hali yenu ya uchumi ni nzuri na mnataka kujilinganisha na simba....ukweli ni kuwa kwa hali za timu na uchumi wao kwa sasa hivi simba na yanga ni mbingu na ardhi