Tatizo liko WAPI? mbona kauli ni nyingi tu zenye kuelekeza jambo kwa umma zikiwa katika hali ya IMANI !!
Kama nchi INAPONYWA kwa kauli hizi za viongozi , bila KUMTANGULIZA MUNGU jamii itaanguka.
Kwani kutamka RAMADHAN shida itatoweka ! inaleta ukakasi gani? Mipango na mikakati ya serikali imeangukia wakati huo kuwa na unafuu.
Kwann mtoa taarifa asijieleze hivyo. TUSIFUMBE macho pia, nchi yetu ipo na IMANI iliyo NUSU KWA NUSU hivyo kama taifa KUJIFANYA kupuuzia wengine wakiwa katka kutekeleza moja ya maagizo ya Imani yao serikali ISIWAJALI.
Sukari ni bidhaa myhimu kwa matumizi wakati wa MFUNGO, tupendane kama taifa tuache kujadili vitu vidogovidogo katka taifa lenye TABU nyingi.
Mbona mishahara huwa inawahi kutoka kipindi cha CHRISTMASS ? jibu ni jepesi au mbona PASAKA ikiangukia karibu na mwisho wa mwezi mshahara unawahi kutoka? Majibu ni mepesi.
Kwann MAULID, AU IDD wakati wa sherehe zake mishahara huchelewa kutoka ? Majibu ni mepesi.
Tusilqzimishe kunusa harufu za udini WAKATI haipo.
Mm ni Mkatoliki .
Mtaguso wa 2 unatuaminisha kuwa popote pale Mwanadamu alipo na juhudi ya kumtafuta Mungu wa Kweli anayo nafasi ya kwenda Mbinguni.
Popote iwe Mkristo dhehebu lolote, iwe Muislamu Zidisha swala ishi kwa haki Pepo ni yako.