Fatma Karume aondolewa kwenye orodha ya mawakili (Permanent removal), akutwa na hatia ya kukiuka maadili

Fatma Karume aondolewa kwenye orodha ya mawakili (Permanent removal), akutwa na hatia ya kukiuka maadili

Nilisiki anafanya kaz kimataifa..ameondolewa hapa ataendelea huko ulaya..
 
Kumpiga Chura teke ni kumuongezea mwendo.

Mwenyezi Mungu msimamie Fatma ,Mlango mmoja ukifungwa mwingine uko wazi .
 
Kikao cha kamati ya maadili ya Mawakili kilichokaa leo tarehe 23/9/2020 kimemkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kiwango cha juu, wakili Fatma Karume mwenye roll namba 848 na hivyo kuamuru jina lake liondolewe (permanent removal) katika orodha ya mawakili Tanganyika.

September mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.

Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.

Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili

===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.

"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Tutamrudisha baada ya uchaguzi baada ya chadema kushika nchi
 
Tanzania baada ya uchaguzi wa 2015, tulipoteza busara ya kuoeana haki na kufuata katiba. Ninachoogopa sasa ni huyu Dada akaulizwa kuhusu Uraia wake, japokuwa nj mtoto wa Raisi msataafu. Kwa mizizi yao ina michanganyiko mingi, inasemekana wana Ungazija, Maliwi, Usomali, ushirazi. Japokuwa idadi kubwa ya wazanzibari wamechanganya sana

Tukianza kuulizana Asili zetu hatutofika wala hatutoweza kuthibitisha ,inawezekana Asili unayoijua kuwa ni ya kwenu ikawa ndivyo sivyo Mkuu.
 
Unajua Uzalendo lkn Maadili hujui...

Hairuhusiwi kuiba research ya mtu na kujidai ni ya kwako - plagiarism is a crime..

Hairuhusiwi kufanya biashara ukiwa Ikulu...haiwezekani familia inaanzisha Kampuni ya Ujenzi na inajipa tender za kujenga Uwanja wa ndege wa Kimataifa kijijini kwao na kununua Ndege za familia kwa Fedha za Umma, huo ni Ujinga tu amechuma Majanga atakula na nduguze na wanae
Mnadanganywa. Hizo habari ni za uongo uongo.
 
Tukianza kuulizana Asili zetu hatutofika wala hatutoweza kuthibitisha ,inawezekana Asili unayoijua kuwa ni ya kwenu ikawa ndivyo sivyo Mkuu.
Tunaovyoenda tushafika huko, hata Raisi wanasema alitokea Burundi
 
Wanaona raha kubaki na mawakili vilaza tu, watu competent mnawaondoa, mnataka muwatawale mawazo yao na uhuru wao wanakataa kwasababu wanajitambua, endeleeni kubaki na hao mawakili wasiojielewa muwatumie mtakavyo ila jamii iliyostaarabika inajua tatizo liko wapi.
Angekua na content asingefikia hapo....Ni kilaza tu
 
Back
Top Bottom