Fatma Karume: Kwa mara ya kwanza naona aibu kuwa Mzanzibari

Mwambieni kuwa baba yake aliingia madarakani 2000 kwa kumwaga damu nyingi akisaidiwa na Mkapa, kipindi hicho hakuona aibu kuwa mzanzibari? Au kwa vile baba ndio alikuwa anaitaka hiyo nafasi.!
Tumia akili basi
 
Kwani baba yake Mzee Karume alikuwa ni Mkenya? Ukatili na udhalimu mkubwa umefanywa na Baba yake alipokuwa Rais wa Zanzibar. Asijitoe akili kuwa Wazanzibar hawawezi kuwa Waovu.
Kumbuka kuna marais Karume wawili waliowahi kutawala Zanzibar.

Sasa wewe umemlenga yupi?

Kama unamuongelea yule wa kwanza ni sawa, lakini kama ni huyu wa mwisho, mi naona ana ustaarabu flani, alileta maridhiano na Maalim Sefu akawa makamu wa rais!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiz hasira za huyu dada kwa serikali zilisababishwa na kitu gani? Kuna yule bint wasarungi wanashida gani hasa.
 
Mama amevunja rekodi ya kulewa madaraka ndani ya muda mfupi.
Tatizo lenu hamjitambui tu
Mlijua vizuri sana kwamba mama ni ccm,na alikua makamu mwenyekiti wa bunge la katiba lakini mkajipa matumaini feki
Subirini mpaka 2030 na mbowe atafungwa tu hamuwezi kufanya lolote
 
Kwahiyo kama babu yake alifanya uovu pia baba ake alifanya unyama na yeye aendelee kusapoti uovu?
Hivi huwa unafikir kweli kabla ya kuandika???
 
Kwahiyo kama babu yake alifanya uovu pia baba ake alifanya unyama na yeye aendelee kusapoti uovu?
Hivi huwa unafikir kweli kabla ya kuandika???
Kabla ya kuhoji ikiwa nafikiri kweli kabla ya kuandika ulitakiwa ujiulize wewe kwanza ikiwa una uwezo wa kusoma na kuelewa kilichoandikwa kabla ya ku-comment!

Ungekuwa unaelewa kinachoandikwa ungefahamu hoja hapa sio ku-support uovu bali hoja ni unafiki wa kujifanya kushangaa kinachofanywa na Samia kama Mzanzibari huku akijaribu kuaminisha watu kwamba viongozi kutoka Zanzibar hawana hiyo tabia.

Kila anayezijua siasa za ZNZ pia anafahamu anachofanya Samia sio kigeni kwa watawala wa Wazanzibar including baba yake mwenyewe!! Sasa how come ajifanye kuona aibu hivi sasa wakati mwaka jana tu hapa watawala wa Zanzibar walihalalisha unyama dhidi ya Wafuasi wa ACT?

How come ajifanye kuona aibu hivi sasa wakati juzi tu hapa, I mean 2015 Watawala wa ZNZ walihalalisha kupororwa ushindi wa CUF?

How come leo ajifanye kuona aibu kana kwamba ni jambo la ajabu kwakati ni miaka 20 tu iliyopita makumi ya wafuasi wa CUF waliuawa wakati wa utawala wa baba yake mwenyewe?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…