Fatma Karume: Yaani leo nimethibitisha Adelardus (AG) hajui Katiba, anadai Serikali ina mihimili mitatu na yeye ndie anasimamia yote


Bunge ni idara au wizara ya serikali?
 

Hujui tofauti kati ya Dola na Serikali. Kajielimishe.
 
Government has three branches, which are Legislature, Executive and Judiciary.

My question is what are the swahili words for the Government and executive?
Inaitwa Mihimili mitatu ya Dola ambapo serikali ni mhimili mmojawapo, sio Mihimili mitatu ya serikali.
 
Mkuu,
Mimi natofautiana na Fatma. Huyu AG yuko sahihi kabisa na hajataka kupindisha maneno. Mihimili mingine yote iko chini ya serikali.

Fatma anazungumzia Katiba-maandishi ambapo yuko sawa kwa upande wake. Na AG anazungumzia Katiba-Kiuhalisia ambapo serikali imeiweka mfukoni Mihimili mingine imekua iko chini yake (refer theory ya Mhimili-Chimbifu)

Sasa kwa sasa hatufati Tena maandishi yanasema nini, katiba yote imekua ni utashi wa mtu anavyojisikia. So hapa ndipo dhana ya Mhimili-Chimbifu inaposhika hatamu.

Ingekua tunafuata Katiba, Fatma angekua sahihi kwa 101%. Ila kwa vile tunafuata uhalisia ulivyo katika kipindi hiki, hao Mahakama na Bunge wote wameufyata kwa Bwana Mkubwa, Mkuu wa Chimbifu empire, so AG anakua yuko sahihi.
 
Hypothetically

Mwenyekiti wa Kijiji ni mjumbe wa kamati ya Usalama ya Wilaya, unataka kuniambia Mwenyekiti ni msimamizi wa kamati ya Usalama ya Wilaya?

Mwanasheria Mkuu sio msimamizi bali mshauri na hapo ndipo usahihi wa Fatma ulipo.
Mwenyekiti gani huyo wa kijiji anakuwa mjumbe wa kamati ya usalama wilaya aseee .... Elimu yetu ni tatizo sana wajumbe wa kamati ya usalama ni
1) MKUU WA WILAYA,
2)KATIBU TAWALA WILAYA,
3)MKUU WA MAGEREZA WILAYA,
4)MKUU WA POLISI WILAYA,
5)MKUFUNZI WA MGAMBO WILAYA, 6)MKUU WA ZIMAMOTO WILAYA,
7)AFISA UHAMIAJI WILAYA ,
8)MKUU WA TAKUKURU WILAYA,
HAta mkurugenzi anaalikwa tu hata Mwenyekiti wa hlamshauri (diwani)/Meya haiingii huyo mwenyekiti wa kijiji anaingiaje kwa mfano
 
Mwenzenu kaweka Hadi reference, Nyie mnamshambulia yeye Kama yeye. Tatizo Ni Nini mataga?
Tatizo ni upeo...
Wa la saba wanatosha!!!
Kama kusoma haya madogo waliyotafuniwa vipi mikataba na kujadili mambo yenye kuhitaji maarifa na akili?
 
Mwenzenu kaweka Hadi reference, Nyie mnamshambulia yeye Kama yeye. Tatizo Ni Nini mataga?
Mkuu hilo ni zao la elimu yetu,unaanzaje kubishana na msomi na wewe ni mweupe kichwani mataga yaache yaendelee kutaga mayai.
 
Umemalizaaaaaaaaaaah
 
AG kiazi, no wonder ofisi yake inaandika sheria za hovyo hovyo.
Hili ni kipindi kigumu sana katika historia ya Tanzania.
#1 mwenyewe ni mashaka matupu katika uelewa wa sheria na katiba, huku Spika ni utata mtupu maana hapo hakuna kitu kabisa ni ubabe tuu. Sasa AG naye kumbe ndio walewale?
Hiki ni kipindi kigumu na kibaya sana katika historia ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…