Fatuma Karume: Mwambieni Ndugai Kanuni za Bunge si Sheria za Nchi, hazituhusu sisi

Fatuma Karume: Mwambieni Ndugai Kanuni za Bunge si Sheria za Nchi, hazituhusu sisi

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Swali kwa Job:

Kwani Wanahabari ni Wabunge mpaka uwapeleke kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge?

Ushauri wangu ni:
Job soma kanuni ya 2 ya Kanuni za Bunge. Kanuni zenu zinatumika kuendesha Bunge na si NCHI. Hazituhusu sisi. Si SHERIA za Nchi.

Bunge si Mahakama. Halina MAMLAKA la kumuhukumu mtu yeyote. Job anataka kuingilia MAMLAKA ya Mahakama. Kama wanahabari wamevunja SHERIA awapeleka Mahakamani. Kanuni za Maadili za Bunge hawezi kuzitumia kuwahukumu wanahabari. Bunge si MAHAKAMA!"

Wakili msomi Fatma Karume

E4vDRXeWYAEbU1_.jpg
 
Mzee Ndugai sijui ana tatizo gani kiakili, au anatesti mitambo ya kamati za "KUSAGA KUNGUNI" ili ziitishe kikao cha dharura dhidi yake.

Mzee kama huyu ndio wanaishia kuwa wale wazee wakuda na wanafiki wa kitongoji. Ukizinguana nae anakutafutia hata skendo ya kutembea na mke wa mtu.
 
Kama kwenye maswala madogo hivi hayafuatwi kisheria, basi kuna kanuni pia zinakiukwa sana hasa bunge lile lilopita lenye wapinzani
 
Katika watu wa hovyo wasiostahili nafasi ya uongozi popote, huyu Ndugai ndiye namba moja.

Huko bungeni inafaa waanze kumshughulikia na kumtoa kwenye nafasi hiyo. Kinga aliyokuwa akiitegemea sasa haipo, ya nini kuendelea kuaibisha bunge letu na mtu asiyekuwa na sifa za uongozi kama huyo abaki kuwa spika wake?

Bado anatishia watu na vyombo vya habari na vikamati vyake utadhani na yeye ana mabunduki ya kwenda kuwatishia hao anaowalaumu kwa kumpa ukweli juu ya udhaifu wake mkubwa kiuongozi.
 
Paschal Mayala aliwahi kuitwa kwenye kamati kwani alikua Mbunge?

CAG aliwahi kuitwa kwenye kamati, kwani yeye alikua mbunge?

Fatuma aache kujibu hoja kimipasho, ajibu kama mtaalamu wa sheria, je kisheria bunge linaweza kumuita nani na nani kwenye makati ama hawaruhusiwi kumuita mtu yoyote asie mbunge kwenye kamati.

Sasa kumwambia Ndugai asome kifungu gani inatusaidia nini sisi tusieolewa sheria?
 
Amekuwekea attachment isome vizuri
 
Wewe ukisoma hicho kiambatanisho kuna mahala unaona wamendika utaratibu wa kuwaita watu kwenye kamati za bunge?
Mashabiki na wafuasi mataga mna matatizo Sana, bado mnaishi ktk ulimwengu wa zidumu fikira za mwenyekiti wa CCM. Ukisoma hiyo Cap 2.1 imeanza na ufafanuzi mzuri Tu.
 
Zilikuwa enzi za jiwe na job ulikuwa ni mmoja wa mikono miovu ya jiwe.

Back
Top Bottom