Fatuma Karume: Mwambieni Ndugai Kanuni za Bunge si Sheria za Nchi, hazituhusu sisi

Bunge au kamati ya Bunge ina uwezo wa kikatiba wa kumwita mtu asiye mbunge kama kuna taarifa linataka kuipata kutoka kwa huyo mtu, lakini siyo kwa nia ya kutaka kumwadhibu, kama aavyotishia huyo mpuuzi.

Mtu asiye mbunge, hawezi kuhukumiwa kwa kutumia kanuni za Bunge.
 
Paschal Mayala aliwahi kuitwa kwenye kamati kwani alikua Mbunge?

CAG aliwahi kuitwa kwenye kamati, kwani yeye alikua mbunge?

kwa utawala ule hata wewe ungeweza kuitwa mbele ya kamati ya skauti kwa kosa la kipuuzi tu na ungetii amri.

nani alikuwa na ubavu wa kupinga amri au wito chini ya utawala wa jiwe?. nani?...mtaje tumjue.
 
Wewe pia ni mwongo. Spika hawezi kuamuru asiye mbunge apelekwe bungeni kwa pingu. Kinachofanyika ni spika kuiomba mahakama itoe kibali cha aliyekaidi wito wa bunge kupelekwa bungeni kwa lazima.

Na hiyo haihusiani na mtu asiye mbunge kutoa maoni yake, zaidi ni pale bunge linapofanya uchunguzi wa jambo fulani, na anayeitwa na bunge anaonekana kuwa katika nafasi ya kulisaidia bunge kupata taarifa sahihi.

Kiufupi, bunge halina uwezo wa kumwadhibu mtu asiye mbunge. Mtu asiye mbunge hafungwi na kanuni za bunge, bali anafungwa na sheria na katiba ya nchi. Katiba ndiyo inayomtaka mwananchi kuitikio wito wa Bunge.
 
Kwani ile sheria ya Kinga, mamlaka ya bunge haituhusu? Maana wanaisema sana
Kanuni za Bunge zipo kwaajili ya shughuli za bunge na wabunge. Wewe usiye mbunge, utaenda Bungeni ka sheria au katiba ya nchi inakutaka ufanye hivyo.

Kanuni za Bunge hazina meno nje ya Bunge na wabunge.
 
Tumsamehe bure alishakiri ana cheti mirembe
 

Ili tujue unazungumzia unachokijua, tuwekee kufunga ch sheria kinachomruhusu spika kumuita mtu yoyote kwenye kamati ya maadili.
 
Walipewa adhabu gani hao walioitwa? Walikwenda kutembea tu@@ghh

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
So walivyomuita Pascal Mayalla bungeni hawakuwa na haki ya kufanya vile?
Ndio maana yake. Kanuni za bunge zinatunika kwa minajiri ya shughuli za Bunge na wabunge. Otherwise ni sawa na Mahakama kuwajibisha wanahabari au mkulima kwa kanuni za kiutumishi za Mahakama.
 
Mkuu Hakimu Mfawidhi, haya masuala ya kuelimishana hayataki hasira, wewe toa elimu yako wa faida ya Umaa. Ukiweka hasira nawe pia tukushangaa.
 

Wewe ni kiasi fulani kimejaa maji! Mosi, orodha iliyo na jina Lissu haikutolewa na Bunge bali Serikali. Tuhuma za uongo unazozisema ni kosa la jinai, lina vifungu vya sheria na adhabu! Kamati ya Bunge ni kwa ajili ya mambo ya Bunge bila kuathiri masharti ya Katiba. Mazoea ya jambo sio sheria!! Pili sikufananisha Bunge la Marekani na letu, nimetufautisha (hivi unajua compare and contrast kweli wewe) na nimetoa kama mfano. Nia ya hilo ni kutaka kuonesha jambo hili hili la kuita watu linaratibiwaje. Hata kwetu kuna kitu kinaitwa Azimio la Bunge. Ndio hili lilipaswa kufanywa kwanza kisha kutajwa na Spika. Spika hawezi kuwa mlalamikaji na pia akawa hakimu na kisha akatoa hukumu ambayo mtuhumiwa hana mahala ya kutafuta redress. Ujinga wa kiwango hii mnautoa wapi watu wa hovyo ninyi?? Hakimu Mfawidhi Bush Lawyer!! Huna chochote unajua zaidi ya kujifanya unajua mambo kijiweni.

Na ni kweli, acha kujadiliana na mimi jambo hilo. Uko very shallow. Kamati ya Maadili ya Bunge ni kwa ajili ya Bunge. Si kwa ajili ya wafanyakazi hata wa umma kwa sabau huko kuna Kamati ya Maadili (iliyowahoji Prof. Tibaijuka na akina Ngeleja na Chenge sakata la Escrow). Vyombo vilivosajiriwa kisheria vina mabaraza ambayo husimamia maadili!! Magazeti kufungiwa yalifungiwa na Kamati ya Bunge?? Ukitaka kuangalia utoaji haki lazima kuwe independence kati ya mshitaki, mshitakiwa na mtoa adhabu. Kama hata hujui tofauti ndoto hiyo - unakosa uhalali wa kujadili na akili yangu. Kukuthibitishia hilo, CAG na Mayalla hawakufanywa chochote kwa mujibu wa sheria. Kuitwa kule ilikuwa ni kiki tu. Kama hii unayofanya hapa kujifanya mjuaji kumbe binge la kiazi!!
 
So walivyomuita Pascal Mayalla bungeni hawakuwa na haki ya kufanya vile?

Hawakuwa na haki hiyo kabisa, ni kosa kumuita mtu yeyote ndani ya kamati ya maadili ya bunge kama mtu huyo si mbunge au jambo hilo liwe limefanyika nje ya bunge na mtu si mbunge alafu umuite kwenye kamati ya maadili ya bunge. Ni sawa ww ni Chadema, unafanya kosa linahusu Chadema, alafu eti CCM wakuite katika kamati ya maadili yao.
 
Kuna katuni za ovyo zinamhusuvJobo mbona hajawaita kwenye kamati
 
Chanduga anaishi 1947, mwehu!
 
Ni kweli kabisa...

Ni sawa na kumuhukumu mwanajeshi kwenye mahakama zetu za kawaida wakati wana mambo yao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…