FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

Haikuwa kimara hii garage ilikuwa Tabata, na kuna ndugu yetu alikuwa hapo kwenye hiyo garage alienda kutoa ushahidi Marekani ingawa walilipwa hela nzuri
 
Jamaa hawafai hatari
 
Achane nae mtu baada ya kuchambua vitu anashabikia dini. Kama ukiwa na mtazamo wa dini waisraeli ndio wana haki na palestina maana uyahudi ndio baba wa ukristo na uislamu. Lakini ukitoa dini pembeni na ukatumia uwezo wa kuchambua na kufikiria unapata kuwa wapalestina wana haki. Tatizo dini hatujui kuitumia waafrika, ndo maana tunarudi nyuma. Sio kila kitu inabeba kama kilivyo inabidi uweke reasoning wazee
 
Ubabe hauepukiki kwenye maisha ukishapata hela utajua
 
Ahmed Ghailan alikuwa ni mtumishi au agent wa Alqaeda,so alikuwa kazini,ameshiriki mission nyingi mpaka kuja kudakwa.
Kuna wakati alikuwa bodyguard wa Osama kwa mujibu wa FBI
Sidhani kama alifikia level za kuwa bodyguard kabisaa. Kuna mahala nilisona alikuwa personal chef wa Bin Laden. Kikubwa Osama alimkubali saaana huyo mwamba.

Kuna mshkaji mwengine hivi ana sijui ndo huyo huyo. Familia ilipata mpunga wa kutosha wakahama kutoka Zanzibar wakaja kununua uwanja maeneo ya kigogo-Mburahati wakajenga nyumba ya kishua miaka fulani mbeleni baada ya kadhia hiyo kuisha jamaa kufungwa.
 
Hizo connection hata mi nilizitamani
 
Hahaaaaa
 
Hii ni porojo za mtaani. Huyu jamaa alipatikana kwa weledi mkubwa wa kijasusi.wataalamu wa mabomu walichukua sampling na kuzifanyia uchunguzi kugunsua bomu lililotumika ni la aina gani, uzito gani na limetengenezwa wapi. Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa bomu liliundwa hapa hapa nchini...swali likaja ni wapi inaweza kuwa lilitengenezwa?Hoja ikaja kujua vitu vilivyotumika kutengeneza hilo bomu na vilipatikana wapi....kitu kikubwa kutumika ni gesi hivyo majasusi walienda kwenye kampuni ya uzalishaji gesi TOL iliyokuwa inamilikiwa na serikali kutambua mauzo makubwa ya gesi yalifanyika lini na mnunuzi ni nani...Ndipo walipogundua karakana ya bw Lyimo ilifanya manunuzi hayo....na hivyo ndo alivyohusika ...hata hivyo walisaidia sana kumpata mtuhumiwa ghailani kwani mmoja wa wafanyakazi alishawahi kukutana na Ghailani maeneo ya Ilala hivyo wakatambua mahali magaidi walipoishi.Pia yule mfanyakazi alisaidia kupatikana kwa taswira ya ghailani kupitia maswali ya majasusi....ni story ndefu hadi kumpata mama ntilie aliyekuwa anawapelekea chakula katika hiyo nyumba ambayo alikuwa haiingii mgeni na ukaribu wa kimapenzi alioanzisha na ghailani yaliyopelekea kunasa mazungumzo yao ya simu na kutambua mahali alipo Ghailani na kumkamata kama kuku akiwa anahudumia mgahawa mmoja huko South Africa
 
Mi niliandika kutoka kichwani kwa ninayofahamu,huyu bwana juu ametoa google.ila ninachofahamu Ghailan alikamatiwa Pakistani sasa huyu bwana amekopi wapi sijui kuwa Ghailan alikamatiwa South Africa
Aisee version zipo nyingi sana kumbe. Mimi nilihadithiwa alikamatwa Dubai akifanya kazi ya hotelia. Waliomkamata walibook table wakaomba wahudumiwe na huyo jamaa kwa jina lake alilotumia huko. Alivyopeleka huduma askari wa kimarekani wakamsalimia kwa kiswahili jamaa akapagawa...sijui ilikuwa chai ile
 
Kwa miaka mingi tangu Niko utoto chakula Cha mifugo Ubungo kinauzwa pale kwa akina mama wauza samaki na mafundi saa...kuna kama kigorofa mshenzi hivi ..kile kogorfa ni Cha zamani ajabu...kumbe yule Mzee mwenye ile nyumba naye alishiriki...no wonder palikuja kudorora sana pale...
 
Yes ndiyo huyo mkuu

To
Yule aliyekuwa fundi Tabata. Kama ndiye alivyokufa akasafirishwa kwenda kuzikwa Moshi.
Nina ndugu walikuwa wanafanya naye kazi Tabata. Ilikuwa mara kwa mara maaskari wa Marekani walikuwa wanaenda kumtbelea Tabata dampo pale gereji. Siku fulani maaskari wakaenda pale then wakapewa taarifa kuwa jamaa alikufa na tushamzika kwao Moshi.

Sijui hawakuamini. Wakachukua mafundi walioenda msibani. Wakawasha gari mpaka kijijini kwa jamaa alipozikwa wakaona kaburi wakahoji watu wakapiga picha ndo ikawa mwisho wa kumfatilia yule jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…