FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

Huyu Bwana yuko zake Kimara Bucha kwenye kasri au tuite hekalu lake mithili ya ikulu ndogo ya Singida, anakula bata huku akilea wajukuu,ameshazeeka sasa.

Yeye na kizazi chake walipigwa ban wasikanyage USA wala kusogelea ubalazi wao.

Wakati ubalozi wa Marekani unalipuliwa nchini pamoja na Nairobi Kenya, polisi na wapelelezi wetu wakaanza kukamatakamta watu ovyo eti ni washukiwa,watu wasiopungua 200 walikuwa shimoni kule Central Police, DSM.

FBI wakapata taharifa kuwa kuna suspects wamekamatwa wako central, wakaomba kuwaona. Kufika kule wakawaambia polisi wa bongo kuwa waachieni wote hakuna suspect hapa, hakuna gaidi anavaa yeboyebo amepauka kwa njaa.hawa ni vibaka tu,IGP akaambiwa u know anything about terrorism?

Jamaa wakaingia chimbo wakaomba akaunti za wafanyabiashara na vionhozi wote wa kisiasa na wanaharakati ambao wameingiziwa mpunga mrefu ndani ya miezi kadhaa (sikumbuki) Thomas Lyimo mfanyabiashara aliyekuwa na garage yake Kimara bucha na vibanda vya maziwa Dar nzima enzi hizo akajikuta matatani, ni baada ya kuonekana akaunti yake iliingiziwa pesa hazina maelezo, kipindi hicho sheria ya money laundering haijatungwa.

Kufustilia kwa kina ni kweli bomu lililolipua ubalozi liliunganishiwa kimara kwenye garage yake.

Hayo yakifanyika mastermind alikuwa kijana mdogo toka Zanzibar Ahmed Khalfan Ghailan,mshirika wa Alqaeda ambaye baadae anakuja kuwa mtu wa karibu kabisa na Osama Bin Laden
ndie alimuingizia huo mpunga kabla ya kukimbilia Nairobi na uarabuni.alikuwa kijana mfogo tu wa miaka 24 au 25, kwa sasa bwana Ghailan ni mtu mzima sasa anakaribia miaka 50 yuko Guantanamo Bay Camp chini ya ilinzi mkali.

Huwapendi USA ila una vingi vya kujifunza kwao

OKW BOBAN SUNZU
Haikuwa kimara hii garage ilikuwa Tabata, na kuna ndugu yetu alikuwa hapo kwenye hiyo garage alienda kutoa ushahidi Marekani ingawa walilipwa hela nzuri
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Walipokuja FBI walichunguza mabaki ya Bomu. Bomu liliwekwa kwenye Boza la Maji(lori la Isunzu rangi ya Blue lilokuwa linapereka maji pale ubalozini) kwenye yale Mabaki waligundua gesi zilizotumika kuunda lile bomu. Walienda TOL na kuomba majina ya walionunua gesi kwa kipindi cha miezi 3 iliyopita na ndipo walipogundua kuwa mzee Lymo alinunua kiasi fulani cha gesi husika. Walipo muoji na kutaja alitumiaje hiyo gesi. Ndipo FBI wakaamia Ilala kwenye Nyumba waliopanga vijana wa Osama! The rest is history
Jamaa hawafai hatari
 
Ndio maana nikasema hatutoelewana.

Mimi mwenyewe nina uwezo wa kuweka nukuu randomly tu za extremists wa kikristo katika vipindi tofauti tofauti vya historia au nukuu za Crusaders kama Papa Urban wa pili au Peter the Hermit au nikanukuu vifungu vya agano la kale na agano jipya randomly nikaonesha kuwa "umeona Biblia nayo imeamrisha mauaji na ugaidi".

Kisha nikasababisha mjadala usiokwisha ambao hauna tija zaidi ya kushindana nani anaweza kumshambulia mwenzie bila kufika mwisho.

Nakupa ushindi.
Achane nae mtu baada ya kuchambua vitu anashabikia dini. Kama ukiwa na mtazamo wa dini waisraeli ndio wana haki na palestina maana uyahudi ndio baba wa ukristo na uislamu. Lakini ukitoa dini pembeni na ukatumia uwezo wa kuchambua na kufikiria unapata kuwa wapalestina wana haki. Tatizo dini hatujui kuitumia waafrika, ndo maana tunarudi nyuma. Sio kila kitu inabeba kama kilivyo inabidi uweke reasoning wazee
 
Hata Nelson Mandela alikuwa kwny orodha ya magaidi kwa mujibu wa Report za US na akaondolewa kwny hiyo orodha baada ya kustaafu

inategemea mawazo yako ni huru au yapo 'kwa mujibu '

ukiwa US sasa hivi kutumia Tiktok ni kosa ila kufirana sio kosa japo yote ni mambo binafsi


sio Mimi tu ninaepinga Ubabe wa US …hata Trump kasema akishinda urais anamaliza kwanza vita ndio anaenda kuapishwa
Ubabe hauepukiki kwenye maisha ukishapata hela utajua
 
Ahmed Ghailan alikuwa ni mtumishi au agent wa Alqaeda,so alikuwa kazini,ameshiriki mission nyingi mpaka kuja kudakwa.
Kuna wakati alikuwa bodyguard wa Osama kwa mujibu wa FBI
Sidhani kama alifikia level za kuwa bodyguard kabisaa. Kuna mahala nilisona alikuwa personal chef wa Bin Laden. Kikubwa Osama alimkubali saaana huyo mwamba.

Kuna mshkaji mwengine hivi ana sijui ndo huyo huyo. Familia ilipata mpunga wa kutosha wakahama kutoka Zanzibar wakaja kununua uwanja maeneo ya kigogo-Mburahati wakajenga nyumba ya kishua miaka fulani mbeleni baada ya kadhia hiyo kuisha jamaa kufungwa.
 
Sidhani kama alifikia level za kuwa bodyguard kabisaa. Kuna mahala nilisona alikuwa personal chef wa Bin Laden. Kikubwa Osama alimkubali saaana huyo mwamba.

Kuna mshkaji mwengine hivi ana sijui ndo huyo huyo. Familia ilipata mpunga wa kutosha wakahama kutoka Zanzibar wakaja kununua uwanja maeneo ya kigogo-Mburahati wakajenga nyumba ya kishua miaka fulani mbeleni baada ya kadhia hiyo kuisha jamaa kufungwa.
Hizo connection hata mi nilizitamani
 
Wachaga wengi wenye maduka (Kwa mangi) wana redio iko tuned Radio Maria muda wote unaweza sema utakatifu ndio huu sasa, cha ajabu ktk kila kilo moja ya unga, mchele, sukari na mafuta ya kupikia lazima anapiga kiasi fulani na hicho anachopiga ndio anakula yeye unakuta mara nyingi wanapikia humohumo dukani. Kingine ana uza tena kupata hela ya vitunguu, nyanya, ndizi na nyama.

Achana na kina Mangi aisee....[emoji23][emoji23][emoji23]
Hahaaaaa
 
Hii ni porojo za mtaani. Huyu jamaa alipatikana kwa weledi mkubwa wa kijasusi.wataalamu wa mabomu walichukua sampling na kuzifanyia uchunguzi kugunsua bomu lililotumika ni la aina gani, uzito gani na limetengenezwa wapi. Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa bomu liliundwa hapa hapa nchini...swali likaja ni wapi inaweza kuwa lilitengenezwa?Hoja ikaja kujua vitu vilivyotumika kutengeneza hilo bomu na vilipatikana wapi....kitu kikubwa kutumika ni gesi hivyo majasusi walienda kwenye kampuni ya uzalishaji gesi TOL iliyokuwa inamilikiwa na serikali kutambua mauzo makubwa ya gesi yalifanyika lini na mnunuzi ni nani...Ndipo walipogundua karakana ya bw Lyimo ilifanya manunuzi hayo....na hivyo ndo alivyohusika ...hata hivyo walisaidia sana kumpata mtuhumiwa ghailani kwani mmoja wa wafanyakazi alishawahi kukutana na Ghailani maeneo ya Ilala hivyo wakatambua mahali magaidi walipoishi.Pia yule mfanyakazi alisaidia kupatikana kwa taswira ya ghailani kupitia maswali ya majasusi....ni story ndefu hadi kumpata mama ntilie aliyekuwa anawapelekea chakula katika hiyo nyumba ambayo alikuwa haiingii mgeni na ukaribu wa kimapenzi alioanzisha na ghailani yaliyopelekea kunasa mazungumzo yao ya simu na kutambua mahali alipo Ghailani na kumkamata kama kuku akiwa anahudumia mgahawa mmoja huko South Africa
 
Mi niliandika kutoka kichwani kwa ninayofahamu,huyu bwana juu ametoa google.ila ninachofahamu Ghailan alikamatiwa Pakistani sasa huyu bwana amekopi wapi sijui kuwa Ghailan alikamatiwa South Africa
Aisee version zipo nyingi sana kumbe. Mimi nilihadithiwa alikamatwa Dubai akifanya kazi ya hotelia. Waliomkamata walibook table wakaomba wahudumiwe na huyo jamaa kwa jina lake alilotumia huko. Alivyopeleka huduma askari wa kimarekani wakamsalimia kwa kiswahili jamaa akapagawa...sijui ilikuwa chai ile
 
Acha kudanganya watu stori kamili iko hivi:
Ni kuwa baada ya vijana kudakwa na kusotwa ostabay hao jamaa walipokuja walienda pale ob wakatizama na kuamuru waachiwe wote. Sasa pale bomu lilipolipukia walikuta chasesi ya gari wakaibeba wakaipima zile namba na kugundu mwenye gari wamfuata mwenye gari akakamatwa baada ya hapo yule mwenye gari kumbe alikuwa kamuuzia mtu maingine akatoa vibali vyote vya kuuziana akaonyesha na baada ya hapo akaenda onyesha aliemuuzia akadakwa,hapo aieuza akaachiwa hiyu mliliki baadavha kudakwa akauliza dereva yuko wapi akamtaja na dereva akatafutwa na kudaka ndio dereva alipodakwa ndio akasema sasa amelidishwa na jamaa wakachukue mzigo garage pale bucher ndio huo mlipuko alienda beba bila yeye kujua ndio huyo mzee katika kuchunguzwa akakuta na hela kwenye acount ila hiyo hela huyu mzee aliingiziwa kama malipo ya kazi pale garege kwake ila hakujua kama ni kilipuzi,ila huyu mzee alisaidia kumtaja mteja wake na hapo ndio kazi sasa ya kuwadaka waliopanga huu mpango ambao walidakwa ni pamoja na jamaa mmoja pale ubungo (zamani wakiuza chakula cha mifugo) huyu yeye ndio aliwapokea hao jamaa kutoka majuu akawapa hifashi hadi kutekeleza hiyo shughuli na alikamatwa mpaka sasa bado wanae huko nje.
Naomba niishie hapo
Kwa miaka mingi tangu Niko utoto chakula Cha mifugo Ubungo kinauzwa pale kwa akina mama wauza samaki na mafundi saa...kuna kama kigorofa mshenzi hivi ..kile kogorfa ni Cha zamani ajabu...kumbe yule Mzee mwenye ile nyumba naye alishiriki...no wonder palikuja kudorora sana pale...
 
Yes ndiyo huyo mkuu

To
Yule aliyekuwa fundi Tabata. Kama ndiye alivyokufa akasafirishwa kwenda kuzikwa Moshi.
Nina ndugu walikuwa wanafanya naye kazi Tabata. Ilikuwa mara kwa mara maaskari wa Marekani walikuwa wanaenda kumtbelea Tabata dampo pale gereji. Siku fulani maaskari wakaenda pale then wakapewa taarifa kuwa jamaa alikufa na tushamzika kwao Moshi.

Sijui hawakuamini. Wakachukua mafundi walioenda msibani. Wakawasha gari mpaka kijijini kwa jamaa alipozikwa wakaona kaburi wakahoji watu wakapiga picha ndo ikawa mwisho wa kumfatilia yule jamaa
 
Back
Top Bottom