Huyu Bwana yuko zake Kimara Corner kwenye kasri au tuite hekalu lake mithili ya ikulu ndogo ya Singida, anakula bata huku akilea wajukuu,ameshazeeka sasa.
Yeye na kizazi chake walipigwa ban wasikanyage USA wala kusogelea ubalazi wao.
Wakati ubalozi wa Marekani unalipuliwa nchini pamoja na Nairobi Kenya,polisi na wapelelezi wetu wakaanza kukamatakamta watu ovyo eti ni washukiwa,watu wasiopungua 200 walikuwa shimoni kule Central Police, DSM.
FBI wakapata taharifa kuwa kuna suspects wamekamatwa wako central,wakaomba kuwaona....kufika kule wakawaambia polisi wa bongo kuwa waachieni wote hakuna suspect hapa,hakuna gaidi anavaa yeboyebo amepauka kwa njaa.
Jamaa wakaingia chimbo wakaomba akaunti za wafanyabiashara na vionhozi wote wa kisiasa na wanaharakati ambao wameingiziwa mpunga mrefu ndani ya miezi kadhaa(sikumbuki)Thomas Lyimo mfanyabiashara aliyekuwa na garage yake Kimara kona na vibanda vya maziwa Dar nxima enzi hizo akajikuta matatani,ni baada ya kuonekana akaunti yake iliingiziwa pesa hazina maelezo,kipindi hicho sheria ya
money laundering haijatungwa.
Kufustilia kwa kina ni kweli bomu lililolipua ubalozi liliunganishiwa kimara kwenye garage yake.
Hayo yakifanyika mastermind alikuwa kijana mdogo toka Zanzibar Ahmed Khalfan Ghailan ndie alimuingizia huo mpunga kabla ya kukimbilia Nairobi na uarabuni.alikuwa kijana mfogo tu wa miaka 24 au 25,kwa sasa bwana Ghailan ni mtu mzima sasa.
anakaribia miaka 50 yuko Guantanamo Bay Camp chini ya ilinzi mkali
Huwapendi USA ila una vingi vya kujifunza kwao