kwa kweli i hope hii finali itakuwa safi, maana timu zote mbili zinacheza mpira mzuri, na mara nyingi utakuta mshabiki wa Man ni mshabiki wa Barca pia, ila kwenye hii game wale wa liver na washika bunduki watajibanza sehemu, kujuwa nani ataibuka kidedea inakuwa ngumu, Man wazuri nyuma mpaka mbele il Barca wana spirit kama ya betri ya duracell, sijui kama historia ina nafasi yake hapa, ila kwenye uwanja huo huo Ajax '96 alikwenda kama mtetezi na akashindwa kwa penati, van der sar akiwa golini, lakin hayo ni ya kale, tutegeme finali nzuri yenye kushambuliana kwa zamu