Mpaka sasa, team iko inajitahidi sana kufanya vizuri. Kuna kitu kimoja tu Xavi anazingua, kuanza na kikosi cha kawaida kwenye mechi muhimu.
Ile game ya waturuki, tulitakiwa kuanza na our best squad. Tungewapiga nyingi sana, then tukaenda kwao tukiwa hatuna presha. Badala yake, Xavi anamuanzisha Eric Garcia badla ya Pique. Anamuanzisha Nico badala ya Sergio. Anamuanzisha Depay alietoka majeruhi juzi, badala ya Auba. Kama vile bado haitoshi, anamuacha Ferran aendelee kurukaruka na kukosa nafasi za wazi kwenye mechi muhimu.
Naamini tutawatoa waturuki hapo kwao, ila kazi ingekua rahisi zaidi kama tungeanza na kikosi cha kueleweka pale Camp Nou. We have a bad reputation when it comes to second leg games. Niko nasubiri game ya leo nione mambo yatakua vipi!