FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Inabidi tuendeleze hii winning mentality, high morale of the game,


Alafu kama vipi hiki ki Europa tukibebe tu

Naamini katika msemo
simba akikosa nyama hata nyasi anakula
Ueropa tuhesabu ipo kabatini..Xavi ameleta mapinduzi makubwa kwa wachezaji wa kawaida akiendelea hivi kuna shaka rekodi za Pep kuvunjwa na kinachonifurahisha ana mbinu nyingi mpira wa TiKtak mara atapiga Counta mara wata press vibaya mbaya vitoto vitamu bwana...pale tuingize matoleo mapya mdogo mdogo hasa beki kiongozi.
 
First lady wa Barca fc nimerudi baada ya kuwa frustuated na timu.Barca are back playing football from the front-it is now a matter of time kabla hatujarudi at the helm of world soccer- Thanks Xavi-you are GOD sent
 
XAVI BALL

Inawezekana kabisa Xavi Hernandez bado hajapata ile best eleven yake , bado anabadilisha wachezaji takribani kila mechi na inaeleweka sana kwanini anafanya hivyo lakini kitu ambacho cha msingi ambacho amefanya ni " MENTALITY YA WACHEZAJI " inaonekana dhahiri anataka wachezaji wajitume sana uwanjani , hataki abiria uwanjani . Na wachezaji wametii

Athletic Bilbao ni moja ya timu ndani ya La Liga ambayo inasifika kwa kujituma sana, pressing sana, wanakimbia sana lakini Xavi kaenda nao moto kwa moto , na baada ya hapo ufundi ukaamua mechi

Pressing ya Barcelona , kuna kianzio kipo ...( Aubameyang ) akianza tu basi Ferran na Adama wanafuata halafu viungo watatu wa kati wale wawili wa juu wanaongezeka kufunga njia za pasi , Bilbao walihitaji ufanisi zaidi kutoka nyuma vinginevyo Barca walikuwa wanakula KUKU tu

Msingi ambao Xavi alikuwa nao wakati akicheza naona anautumia sasa hivi " Tunazuia tukiwa na mpira " ( Defending with the ball ) , mabeki wawili wa kati wanatanua , kiungo mzuiaji anaenda katikati yao , mabeki wa pembeni wanasogea juu huku viungo wawili wa juu ( namba 8 wawili ) wanakuwa mstari mmoja ( vertical ) na wale mabeki wa kati waliotanua ili kufungua njia ya pasi ya mbele . Wanamiliki sana mpira

NOTE

1: Ousmane Dembele anaongea na miguu yake tu , akizomewa yeye anajibu na miguu halafu unamshangilia mwenyewe

2: Vesga na Unai kwenye kiungo cha Bilbao walizidiwa aisee, wakiwa na mpira wanafanyiwa pressing , bila mpira wanafukuza vivuli tu

3: Barca wanafunga magoli mengi mengi sasa hivi [emoji91]

4: PEDRI PEDRI PEDRI [emoji91][emoji460]️

Matokeo : Barca 4-0 Bilbao
 
The Maestro
FB_IMG_1646082924269.jpg
 
Kati ya wizi mkubwa uliowahi tokea ni hizi free transfer barca alizofanya [emoji28][emoji28]
Laporta ni jambazi, na mbinguni atapasikia tu dadek zake!

Alafu siku hizi kuna mtindo umeanza pale Barca ambao sidhani kama Laliga wataruhusu. Maana kumekua na mtindo, Iniesta anavaa jezi imeandikwa Pedri, alafu anaingia kucheza wakati sisi tunajua amestaafu!

Sasa hivi waliokua wanatuchukulia poa, tayari wameanza kua na adabu. Taratibu tu kitaeleweka!
 
Back
Top Bottom