XAVI BALL
Inawezekana kabisa Xavi Hernandez bado hajapata ile best eleven yake , bado anabadilisha wachezaji takribani kila mechi na inaeleweka sana kwanini anafanya hivyo lakini kitu ambacho cha msingi ambacho amefanya ni " MENTALITY YA WACHEZAJI " inaonekana dhahiri anataka wachezaji wajitume sana uwanjani , hataki abiria uwanjani . Na wachezaji wametii
Athletic Bilbao ni moja ya timu ndani ya La Liga ambayo inasifika kwa kujituma sana, pressing sana, wanakimbia sana lakini Xavi kaenda nao moto kwa moto , na baada ya hapo ufundi ukaamua mechi
Pressing ya Barcelona , kuna kianzio kipo ...( Aubameyang ) akianza tu basi Ferran na Adama wanafuata halafu viungo watatu wa kati wale wawili wa juu wanaongezeka kufunga njia za pasi , Bilbao walihitaji ufanisi zaidi kutoka nyuma vinginevyo Barca walikuwa wanakula KUKU tu
Msingi ambao Xavi alikuwa nao wakati akicheza naona anautumia sasa hivi " Tunazuia tukiwa na mpira " ( Defending with the ball ) , mabeki wawili wa kati wanatanua , kiungo mzuiaji anaenda katikati yao , mabeki wa pembeni wanasogea juu huku viungo wawili wa juu ( namba 8 wawili ) wanakuwa mstari mmoja ( vertical ) na wale mabeki wa kati waliotanua ili kufungua njia ya pasi ya mbele . Wanamiliki sana mpira
NOTE
1: Ousmane Dembele anaongea na miguu yake tu , akizomewa yeye anajibu na miguu halafu unamshangilia mwenyewe
2: Vesga na Unai kwenye kiungo cha Bilbao walizidiwa aisee, wakiwa na mpira wanafanyiwa pressing , bila mpira wanafukuza vivuli tu
3: Barca wanafunga magoli mengi mengi sasa hivi [emoji91]
4: PEDRI PEDRI PEDRI [emoji91][emoji460]️
Matokeo : Barca 4-0 Bilbao