FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

JUMATANO mida ya saa 4:45 usiku kwa majira ya EAST AFRICA siku hyo ni siku ya mauaji ya halaiki ni siku ya historia kwa wenger ambayo hawez isahau katika maisha yake ni usiku wa MSN ukiongozwa na KING wa soka duniani
Yani mkuu saa mbili nitakuwa nishatulia kwenye kiti kusubr kibano hiki cha kalne maana mzee wenga jana tu kapewa kichapo nawale madogo na huku anasikia watu wamefikisha mechi 37 hawajafungwa yaani wanataka kuweka record ya mechi 50 sasa sijui mzee wetu wenger anaishije sasahv
 
SAMUEL ETO'O: "sikucheza na Messi, Messi ndiye aliyekuja kucheza na mimi"

Mchezaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto’o ambaye sasa ni mchezaji wa klabu ya Antorlop ya Uturuki alifafanua kupitia kipindi cha michezo kinachoonyeshwa na television ya Uturuki kwamba hakucheza na Messi, bali Messi ndiye aliyekuja kucheza na yeye.

"nilimuona wakati anakuwa, akianzia Barca Juvenile A akahitimu na kufuzu kuingia Barcelona B, mimi Ronaldinho, Puyol, Beleti, Deco na Lil Thuran tulikuwa tunaenda kumshuhudia kule mini estadi ambapo ndio uwanja unaotumika kwa vijana wa Barcelona B"

"mara ya kwanza nilisikia habari zake katika vyumba vya kubadilishia nguo lakini nilipuuza"

"baadae habari zake zikaenea sana hata baada ya kuiwezesha Barcelona B kutwaa mataji ya vijana wadogo ya uefa, la liga, copa del rey na klabu bingwa ya dunia"

"niliamua kumfwata na kuhudhuria mechi zake nimshuhudie kwa macho"

"nilimshangaa tangu siku ya kwanza nilipomwona uwanjani, ilinibidi nimfwate na nikamuuliza jina akaniambia anaitwa Leo, tukamwalika aje kufanya mazoezi na sisi, alifurahi sana"

"wakina Ronaldinho waliniambia ukimpa mpira alafu umkabe atakuaibisha na ukubwa wako wote"

"Alinivutia sana ikabidi tuongee na Rijkaard ili awe anafanya mazoezi nasi, Rijkaard akatukubalia tuwe naye na tumkuze, kilichokuwa kikitokea mazoezini sitaki kusema ila jambo la Messi kuungana na sisi lilikuwa kama ndoto iliyotokea kuwa kweli kwa haraka sana kwake"

"Hata alipoanza kupata dakika katika kikosi cha kwanza alinikuta tulimlea na alituheshimu kama kaka zake hivyo basi Messi alikuja kucheza na mimi ila mimi sikucheza na Messi"

"Tangu naanza soka mpaka hapa nilipo sijaona mchezaji mwenye kipaji cha ajabu kama chake, iwe kwenye runinga au kwa macho, hakuna! Messi ni bora tangu 2004 na ameweza kumantain mpaka sasa ni vile tu 2004 hamkumjua ila mimi niliyemjua alikuwa bora sana, hivyo basi Messi ni bora tena kwa mbali sana zaidi ya Cristiano Ronaldo, Ronaldo ni mchezaji mzuri lakini kwa ubora hamfikii Messi, Messi atakuwa bora kwa zaidi ya miaka 10 ijayo kitu ambacho Ronaldo atabaki akikitazama, tuko na tutaona"

Eto'o alipoulizwa kuhusu Arda Turan: “ni mmoja wa wachezaji wazuri wa Uturuki, pamoja na kufunga magoli mawili mpaka sasa bado hajaizoea Barcelona, ameanza kuizoea lakini bado hajaizoea na karibia ataizoea"
 
Messi with Barcelona since Luis Enrique is coach:
94 Games
94 Goals
42 Assists
Involved in 136 goals in just 94 games.
 
d86cf6df8f9c94a1eaa6a4f34306ed63.jpg
[emoji13] [emoji13]
 
PNC 1 , Arsenal huwa wanacheza vizuri sana mechi za away from home, nyingi hushinda, 2-0 yetu sio safe sana, itabidi Barca wawamalize mapema sana zile speed then mwisho wa siku tuwaadhibu kwa wiki ili Wenger akapumzike
 
PNC 1 , Arsenal huwa wanacheza vizuri sana mechi za away from home, nyingi hushinda, 2-0 yetu sio safe sana, itabidi Barca wawamalize mapema sana zile speed then mwisho wa siku tuwaadhibu kwa wiki ili Wenger akapumzike
haswaaaaaa dawa ya mabishoo ni kuwa bishoo zaid yao TUTAWAPIGA WEEK
 
>>HUU NI WAKATI MZURI WA BARCELONA KUWEKA HISTORIA YA KUSHINDA TREBLE MARA MBILI MFULULIZO:-

BARCELONA inafurahia matunda ya historia kubwa nchini Hispania kwasasa kama timu iliyocheza michezo mingi zaidi (37) bila kufungwa nchini Hispania.

Ikiwa tayari imeshamalizia robo tatu ya msimu angali ajinsi Barcelona ilivyokuwa bora msimu huu:-

>>Achilia mbali Rafinha, kocha Enrique ameweza kupambana vizuri juu ya matatizo ya majeruhi katika timu ya Barcelona, hii ni kutokana na staili yake ya mzunguko "rotation" baina ya wachezaji na waweza ona matunda ya namna kikosi cha kwanza kinavyotumika ipasavyo huku kikiwa hakina majeruhi hasa kwa kipindi hiki ambacho ni muhimu sana na kinahitajika kwa hali na mali.

>>Huu ni msimu wa pili na hakuna dalili za timu yoyote kuweza kupata mbinu mbadala za kuizuia MSN eneo la ushambuliaji la Barcelona linalohesabika kama eneo hatari zaidi duniani.

>>Huku timu nyingine kubwa zikiendelea kupata misukosuko na kupoteza muelekeo katika ligi na makombe mbalimbali, MSN inaendelea kuwa bora siku hadi siku.

>>Mpaka sasa tayari kwa pamoja wamefikisha idadi ya magoli 100 kwa wakibakisha magoli 22 tu kuifikia rekodi yao waliyoieka msimu uliopita kwa kufunga jumla ya magoli 122 katika msimu mzima.

>>Tofauti ya pointi nane dhidi ya Atletico Madrid, na tofauti ya pointi kumi na mbili dhidi ya Real Madrid, tayari ishaanza La Liga ishaanza kuonekana muelekeo wake.

>>Barcelona ilipoisambaratisha Valencia kwa magoli 7-0 katika mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe La Mfalme iliweza kudhihirika kwamba Barcelona tayari wameshatinga katika fainali ya kombe hilo hata kabla ya marudio na hata baada ya marudio walijikusanyia aggregate ya 8-1 iliyowawezesha kucheza fainali mwezi May mwaka huu dhidi ya Sevilla.

>>Rekodi ya michezo 37 bila kufungwa inayoendelea kujiwekea Barcelona kimya kimya mpaka sasa inadhihirisha kwamba vijana hawa wamedhamiria vilivyo msimu huu na wamekusudia kuweka historia.

>>Baada ya Luis Enrique kusema kwamba, “Rekodi haina maana kwangu kama hatushindi makombe.” basi limewafungua macho wadau wengi wa soka duniani.

Kwani ni ukweli mtupu kwamba Barcelona wananjaa na vikombe huku wakijiwekea historia pasipo kutarajia.
Na kama wachezaji wanalielewa hilo basi Barcelona itakuwa mahala pa vikombe daima.

Hebu jaribu kufikiri, je Barca yaweza kuwa timu ya kwanza kushinda makombe matatu kwa mara mbili mfululizo? Kushinda kombe tu la Uefa mara mbili mfululizo ni bonge la historia hiyo haitoshi na sasa inaonekana kama wanayataka makombe yao yote waliyoshinda mwaka jana.

Huu waweza kuwa wakati muafaka kwa Barcelona historia kubwa kama hii na hizi ndio sababu:-
-Msimu ujao tutashuhudia mabadiliko makubwa sana miongoni mwa vilabu vikubwa duniani. Kwa nyumbani Hispania, mahasimu wakubwa wa Barcelona Real Madrid na Atletico wanadirisha moja tu la kuweza kusajili wachezaji ambapo rufaa yao ya kufungiwa imepelekwa mbele na watatumia mwaya wa dirisha lijalo la mwezi Juni kukusanya vipaji vingi kulingana na mahitaji yao ili watapofungiwa wawe wamejikamilisha.

-Sababu nyingine ni kubadilika kwa haki miliki za uonyeshaji wa mpira katika runinga nchini Hispania.
*Chama cha soka nchini Hispania (LFP) kimebadili baadhi ya vipengele vya haki miliki za television ambapo kila timu itapewa mgao sawa katika ligi hiyo bila kujali nani mkubwa na nani mdogo kama ilivyo sasa ambapo Barcelona na Madrid walikuwa wakipewa mgao mkubwa zaidi ya wengine.
*Hii italeta mabadiliko makubwa katika vikosi mbalimbali hususani timu ndogo ambapo zitapata mgao wa pesa sawa kama timu kubwa na zitakuwa na uwezo wa kununua mchezaji yeyote wamtakao kulingana na pesa walizonazo.

NJE YA HISPANIA:-
>>Guardiola kwenda Man City si habari nzuri kwa timu kibwa hususan Barcelona.
*Hii ni kutokana kwamba atawavutia wachezaji wengi na watapenda kuungana naye pale England.
*Ukizingatia kwamba mmiliki wa klabu ile anauwezo wa kumwaga kiasi chochote cha pesa mradi apate saini ya mchezaji amtakaye na kwakuwa Guardiola ni kocha asiyependa uzembe, siku zote hupendelea wachezaji wenye uwezo mkubwa na vipaji ambao ataendana nao na Barcelona ni miongoni mwa vilabu vyenye wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.

>>Kuna uvumi umeenea kwamba Mourinho huenda akajiunga na Manchester United, ukimchanganya Klopp pale Liverpool, Pep Man City na yeyote atakayefundisha Chelsea badala ya Hiddink, ni wazi kwamba ushindani utakuwa mkubwa sana.
*Makocha wote hawa watataka kuvunja na kutengeneza vikosi vitakavyoweza kuleta mafanikio na kuchuana katika mashindano tofauti.
*Huku Carlo Ancelotti akitengeneza nguvu kupitia Bayern Munich, na fainali za Euro zikiendelea kuchezwa, unaweza ukapata picha kwamba, hakutakuwa na lolote lililopo sasa litasalia hivihivi katika msimu ujao.

kutokana na hiyo, naweza kusema kwamba, huu ni wakati muafaka kwa Barcelona kutengeneza historia kubwa duniani ya kuchukua treble mara mbili hususan kombe la Uefa.

>>Wapinzani wengi wakubwa wanasota, huku timu nyingine zikiwa kwenye hali ya mpito na mabadiliko,

>>Timu ya Bayern Munich yaweza kuwa bora na imekamilika na kuweza kuisumbua Barcelona kwasasa lakini haionekani kama ina uwezo wa kuifikia Barcelona hasa baada ya msimu huu kufikia katikati ambapo ilianza kupoteza michezo mingi na kupata misukosuko na mpaka sasa inachuana na Dortmund katika mbio za Ubingwa wa Bundesliga kiti ambacho hakikuwa hivyo kwa miaka miwili iliyopita ambayo zilikuwa zinabaki mechi hata 10 na Bayern anatangazwa mshindi wa ligi.
*hata katika uefa Bayern msimu huu haina rekodi nzuri kama Barcelona.

>>Hivyo Barcelona inaonekana kama timu ngumu zaidi katika michuano ya Ulaya msimu huu ni wakati muafaka sasa kwa Barcelona kuchukua makombe matatu (treble) kwa mwaka wa pili mfululizo.
xxxx
 
UMENENA CARLO ANCELOTTI,,,, ""Ni Rahisi Na Starehe Kubwa Kumtazama #Messi Akicheza Dhidi Ya Timu Ya Adui,,,ila Ni Hofu,namaumivu Makubwa Kumkabili Anapocheza Dhidi Ya Timu Yako, mimi Ni Mmoja Wa Makocha Nlioweza Kwa Kiasi Kikubwa Kumkabili #Mwanaume Huyu Mara Kadhaa Nikiwa Na RMA,ila Kwa Ujumla Wake Haikuwa Kazi Rahisi,baada Ya Mechi Husika Unapomwona Beki Wako Anachelewa Kufika Ktk Mazoezi Yake Hupaswi Hata Kumlalamikia,kwa Kuwa Aliwajibika Zaidi Ya Mara Mbili Ktk Mechi Dhidi Ya Akina #messi,,..Huwa Ni Vigumu Kumkabili Messi Akiwa Fiti Kwa 100%...ni vigumu kumzuia,,.kipaji chake ni hatari xana kwa sababu hujui ni kitu gani atakifanya,hivyo kiukweli hakuna njia #rasmi ya kumtuliza star huyo.,,HAYO NI MAMENO YA CARLO ANCELOTI,,,KOCHA MTARAJIWA WA "THE BAVARIANS,,,
 
It's official. Lionel Messi is more
exciting than Cristiano Ronaldo!
Mar 15, 2016 Nissan
Nissan have teamed up with Loughborough
University to find out what makes football so
exciting for fansBritish men find watching Lionel
Messi more exciting than any other players in the
Uefa Champions League, according to a survey by
Nissan as part of their Excitement Index.
64% of Brits stated they found Messi exciting to
watch with Barcelona team-mate Luis Suarez
(47%) coming second and Real Madrid rival
Cristiano Ronaldo (25%) coming third.
British fans are also looking forward to Leicester
City's imminent debut season in next season's
Uefa Champions League.
22% of Brits claimed they find Leicester exciting to
watch, ranking them above the last two season's
beaten finalists, Atletico Madrid and Juventus!
Moving away from the pitch slightly, British men
get more excited about watching football than
having sex.
56% of men in Britain stated watching their
favourite team provides them with more
excitement than getting intimate with their loved
ones.
When asked to rate the two aspects of their lives
they found most exciting, nearly one in three
(30%) chose their football club, compared to less
than one in five (16%) who chose their job.
The research also identified 58% of Brits see the
Uefa Champions League final as the event they
most look forward to, with 23% keeping the date of
the final free in their diary each year.
The study was commissioned by Nissan as part of
the Nissan Excitement Index, which aims to
explore the science behind football fan excitement
ahead of this year’s Champions League Final in
Milan.
More than 5,000 people in the UK, Germany,
France, Italy and Spain were surveyed last month.
The car manufacturer has now teamed up with
sports science experts at Loughborough
University to understand the science behind what
makes football so exciting.
Nissan will be carrying out live 'excitement
experiments' with football fans during Uefa
Champions League games over the coming
weeks.
Keep your eyes peeled on Goal.com for the
results of the experiments as one of our very own
correspondents may be involved!
 
PNCCCCCCCC shkamoo kakaaaaaa!!!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Back
Top Bottom