FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

yeah right, bahati si mweusi... bahati mbaya niliangalia idadi ya weusi alipokuja na sasa, naweza mimi ndio nikawa mbaguzi
 
Barca walichemsha sana kumsajili Zlatan
 
lakini mbona ni weusi tu ndio wanauzwa barca na sio mweusi akiingia??

Deco Souza,Ronnie,Alex Hleb,Gianluca Zamblota,Martin Caceres,Henrique,Victor Sanchez,Santiago Ezquero na sasa Ibracadabla!! Hawa siyo weusi,kuna wengi tu. Kocha ana uhuru wa kuamua aina ya wachezaji anaopenda kuwa nao kulingana na style yake ya uchezaji anayotaka na kwa maslahi ya timu zaidi na wala si rangi wala Utaifa, ikitokea timu haifanikiwi hilo ni suala jingine,Rijkaard alipotua Barca alitoa Waholanzi wenzake wote akamwacha Gio pekee,kwani hata Cocu, van Bommel, Marc Overmars walikuwa bado fit,lakini kwa vile hawafit kwenye style yake hakuwahitaji. Mambo haya yapo katika vilabu vyote vikubwa barani ulaya na kwingineko. Ukianza kuzungumzia rangi ya mchezaji au kupenda timu kwa vile tu ina mchezaji mweusi au yellow skin, wewe utaonekana kama either unajibagua au unabagua. Racist Should Stay Away From Sports!!
 
Barca walichemsha sana kumsajili Zlatan

Hapana, hawakuchemsha,ila wamechemsha kumtoa sasa,kafunga goli 17 La Liga, nyingi ni decisive,wakati anasajiliwa alikuwa majeruhi,tatizo ni adaptation,na kelele za Mino(wakala wake)
 
...natamani thread hii angekabidhiwa BJ...
 
he he hehe..., nawe unapotea sana siku hizi.
Barcelona wakoje huko? Naskia Real Madrid keshawasha indicator, anawaacha!
Nilichomoka kidogo.Hawa jamaa naona wako vizuri,lakini tutaangalia tutamalizaje, si tumeanza vipi. There are still 34 more games to play,including 2 El Clasicos!
 
Sporting Gijón 0-2 Valencia CF
Levante UD 0-0 Real Madrid
Athletic Club 1-3 FC Barcelona
RCD Mallorca 2-0 R.Sociedad
RCD Espanyol 1-0 Osasuna
Deportivo 0-2 UD Almería
Racing 0-1 Getafe CF
Hercules 2-0 Sevilla FC
At.Madrid 1-0 Zaragoza
Málaga CF 0-0 Villarreal CF

Naona hata sisi huku tunaanza kuchanganya,La Liga at its Best. Hayo ni matokeo ya round ya 5 mwishoni mwa wiki.
 
...natamani thread hii angekabidhiwa BJ...

Itabidi nitangaze rasmi nia ya kuihama Man U, wananipa presha tu kama timu za Africa WC hii...Nawapa mechi nne, kama wanaendelea hivi basi nitabaki kushangalia kwa mazoea..
 
Itabidi nitangaze rasmi nia ya kuihama Man U, wananipa presha tu kama timu za Africa WC hii...Nawapa mechi nne, kama wanaendelea hivi basi nitabaki kushangalia kwa mazoea..
Karibu hapa kwetu. Camp Nou Experience! You will experience Barca like never before, sisi hatuna pressure, hata tukifungwa mradi Ball Possession ni 75% kwa 25%,kiroho kwatu...!!
 
Gratitude for Berdyev
Before Guardiola had spoken, Rubin Kazan manager Berdyev had described Barça as “the best team in the world”. The FCB boss thanked him for his words, but added that “he said the same thing last season and we dropped 5 points against them!”
 
rubin kazan vs barcelona
hawa rubin kazan walituchapa msimu ulioisha nyumbani nou camp,leo dawa yao ipo jikoni hukohuko kwao kwenye theluji
 
kuna mwenye kumbukumbu ya Fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ya mwaka 1994 ilikuwaje?
 
Karibu hapa kwetu. Camp Nou Experience! You will experience Barca like never before, sisi hatuna pressure, hata tukifungwa mradi Ball Possession ni 75% kwa 25%,kiroho kwatu...!!

Asante nimeshakaribia, subiri nisake ratiba ya mechi zake..Ramos,Iniesta etc wananikonga
 
kuna mwenye kumbukumbu ya Fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ya mwaka 1994 ilikuwaje?
wewe mchokozi unatuchokoza barca,haya tulichapwa 4-0,desailly nae alifunga bao kwa ac milan,ilikuwa athens,kipa wa barca alikuwa andoni zubizaretta,kama unakumbuka world cup1998 france alifungwa bao na sunday oliseh spain vs nigeria walishinda nigeria 3-2 enzi hizo kina raul ndio chipukiza na akafunga bao lake la kwanza la world cup vs nigeria,kipa msaidizi wa barca alikuwa carles busquets babake sergio busquets kiungo wa barca sasa hivi,enzi hizo milan kuna gullit,van basten,paulo maldini na daniel massaro,barca unawakuta hristo stoichkov,romario na pep guardioala
 

Asante mkuu.
Nilikuwa napita tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…