FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Ndio ujue
Kwanza lazima wawafunge
Pili mkishinda nyingiiiii, yaan siku hiyo kwao wanakuwa walilala bar labda
Itakuwa 3-1, yaan hiyo pia wawe wamepewa na red card.
Bado upo
 
kilichotokea sauti imekauka fcb tulikua wanne tu kati ya watu 30+
hauko peke yako naona comments nyingi za watu wa mbele wanalalamika kukaukiwa na sauti na kushindwa kulala usiku
 
Viva Barca[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 

Kocha mkuu wa PSG Unai Emery alichanganyikiwa baada ya mechi ya marejeano dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp kufatia kuchapwa bao 6-1 na kuondoshwa kwenye mashindano ya UEFA Champions League hatua ya 16 bora.

Goli la Edinson Cavani ambalo lilionekana kumaliza matumaini ya Barca kusonga mbele baada ya kuzidisha mzigo wa magoli matatu kwa miamba hiyo ya Hispania lakini bado haikuwa kikwazo kwao kufuzu kwenda robo fainali.

Lakini PSG waliachwa kwenye darasa la kujifunza kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya.

“Kwa kila mmoja ndani ya Paris Saint-Germain, viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki hii ilikuwa ni siku mbaya kwao. Kilichotokea uwanjani ni kitu ambacho hakuwahi kukipitia,” alisema Emery.

“Tumepoteza nafasi nzuri ya kusonga mbele. Tulitaka kukua kulingana na mchezo, kipindi cha kwanza hatukucheza kwa kiwango tulichotaka. Tulitaka kucheza kama mchezo wa kwanza, tulitaka kucheza mtindo wa counter-attack. Baada ya goli la tatu timu ilikuwa vizuri, tulihitaji kupata matokeo mazuri kwa kufunga goli la pili.”

“Ndani ya dakika tano, tulipoteza kila kitu. Hatukuwa na uwezo wa kujilinda. Ni experience mbaya kwetu, lakini ni somo. Najifunza kupitia kushindwa, ni wazi tumepoteza fursa nzuri.”

source:Alichokisema kocha wa PSG baada ya kufanyiwa fedheha Nou Camp | ShaffihDauda
 
tusikilize na hii mkuu cc@Everlenk.

Hahahaahahahha acha kabisa haikuwa rahisiiii!!! ......[emoji443] [emoji444] Kuna mambo yalikuja kama mabaya kumbe yana kusudi na kuna mengine yalikuja kama mazuri kumbe yana mwisho mbaya lakini katika hayo yote tulimuona Bwana akitetea maisha yetu .....[emoji444] [emoji444] [emoji443] ......

Asante kaka kwa jisong lizuri sana huwa nalipendaaa mnoooooo...... yaani jana sikutaka hata kuingia humu tulipofika goli tatu nikaacha hata kuangalia tv nikaawa naiombea tu Barca lile goli la PSG lilininyong'onyeza sana but nikajipa moyo nikazidisha sala nikasema nooooooo haiwezekani Barca aishie round hiii.... mwisho wa siku watu weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!........
 
Shemeji heri ya mwaka mpya...

Jana ndo nimethibitisha ugonjwa utakaoniua sio presha tena. Lile goli la Cavani lilifanya mapigo ya moyo kwenda kasi tofauti... Kwa upendo kabisa nikazima TV nikaenda kulala...

Baadae nikaamshwa milio ya simu... nikajua wabaya wangu wananizodoa... Baadaye ikabidi niingie LiveScore...

Sijui niliendaje bar usiku ule....

Barca walinitibu maradhi ya presha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…