FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FCB fans

1. Hakuna sababu ya kupanic kwa gem ya jana. Ushindi ni mtamu lakini kwa mwanzo huu wa msimu hautufai. Kufungwa kutaongeza kasi ya usajili

2. kuna el classico nne mwaka huu, moja ndo hiyo jana, tatu bado. Tusitegemee kushinda zote. This was Super Cup

3. Gem imenifurahisha maana nimeona ukuta ulioimarika zaidi tofauti na msim uliopita. Ikumbukwe tatizo la FCB lilikua ukuta

4. Denis Suarez anaweza kuziba pengo la neymar, japo sio kwa 100%. Amecheza vizuri sana

5. usajili wa Paulinho si wa kubeza, ni tactical zaidi. Kocha amelenga kutumia viungo wakabaji wawili (double pivot) Busquest na Paulinho, ili kuongeza posession. Viungo wakabaji sio wengi duniani

6. Tutakua na msim mzuri sana mwaka huu, maana timu ni nzuri regardless ya kufungwa jana. Coutinho ataongrza nguvu attacking midfield
 
mkuu suarez nakosa kupelekea mipira hata hivyo anajitahidi sana kwa kikosi cha sa hivi kinawatesa sana Messi na suarez,kumbuka hata ile penati ya jana ni jitihada tu za suarez za ku force king
 
usajiri wa paulinho sio wa kocha hilo lipo wazi,
 
Good News for Barcelona's fans: Release clause ya Paulinho ni €120M. I'm sure no body, even PSG can pay that amount
 
usajiri wa paulinho sio wa kocha hilo lipo wazi,
si wa kocha ila benchi la ufundi. perhaps Lucho's report. Iko waz kabisa kwamba Busquests kazidiwa majukumu, na ikitokea kaumia tutegemee the worst. Sergi Roberto anaandaliwa mazingira ya kuchukua hiyo namba, lakini si haraka kihivyo. Kwa maoni yako unafikiri nani alifaa kumsaidia Busq? Ngolo Kante? Arturo Vidal? Wanyama? Atleast Paulinho anafanana na phylosophy ya team
 
Well, the trolling was so terrible in here. Kwakua mmetulia acha tuongee facts sasa:

Something is wrong with Luis Suarez. Ukiangalia tangu mechi za mwisho za msimu uliopita, mechi za pre season na el classico ya last weekend, amekua na tatizo kwenye finishing.

Anakosa nafasi nyingi za wazi, kitu ambacho sio kawaida yake. Barcelona imekua ikishinda kwa kuoutscore wapinzani. Hatujawahi kua na perfect defense!

Kwa upande mwingine, kile kipigo cha Jana chaweza kua a blessing in disguise. Maana sasa usajili utapewa kipaumbele. Hasa Coutinho na Dembele.

Left wing inahitaji mtu anaeweza kustrech wide na kudrible to the box. Zile cross za Deulofeu sio style yetu.

Otherwise, we were beaten fairly and flat. And the ugly truth is kwa sasa Los Blancos wako na kikosi imara kutuzidi.

Tushukuru hizi weakness zimeonekana mapema.

FORCA BARCA!

- KANA -
 
Maridadi kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Borusia wamekubali Kumuachia Dembele kwa Pound 90M sasa wanajadiliana na Barca Kuhusu Pound kama 27M kwa ajili ya performance ya mchezaji yaani Dembele akiperform vizuri Barca basi walipwe hiyo 27m
 
Wana Barca wenzangu, poleni kwa yaliyitukuta, ila ni heri yametokea Mapema ili tujirekebishe.

Kuna mambo kadhaa tunahitaji kuyajua na kuyajubali kuhusu mechi ya juzi.

1. Tukifungwa mechi ya juzi
2. Team ilicheza vizuri sana
3. Wakati tunatafuta goal la pili, tulifanyiwa shambulizi la kushitukiza ambalo Vidal alichelewa kurudi Ronaldo akafunga
4. Wakati pressure ilikuwa kubwa kutaka kusawazisha goal la pili, tulipoteza mpira kimasihara, wakati pass inatolewa kwa Assensio, rakitic kama sikosei aliusindikiza ule mpira kwa macho,wakati huo Vidal hakuwa tena kwenye position yake, Goal la tatu.

4. Sijui ni kwa nini kocha anamwamini Vidali dhidi ya team ambayo ni deadly kwa mashambulizi ya kushitukiza

5. Sergi Robert anatakiwa anatakiwa aanze badala ya Rakitic

6. Tunatakiwa kutumia nafasi vizuri kwa kila nafasi tunayopata

7. Mechi ijayo tutashinda na kuchukua kombe
 


Kuchukua kombe inabidi umpige Real Madrid 3 - 0, na kupata matokeo hayo labda Zidane awaweke bench wachezaji wote na kumuacha Keylor Navas peke yake uwanjani
 
Kuchukua kombe inabidi umpige Real Madrid 3 - 0, na kupata matokeo hayo labda Zidane awaweke bench wachezaji wote na kumuacha Keylor Navas peke yake uwanjani
Huijui Barcelona vizuri wewe, hata wakati inapitia misukosuko, ina uwezo huo
 
Huijui Barcelona vizuri wewe, hata wakati inapitia misukosuko, ina uwezo huo


Anayeijua Barcelona vizuri ni Gerard Pique ambaye yuko busy trolling on Twitter, uwanjani juzi bao 3 zote kahusika. Ha Ha Ha! Gotta love that clown man.
 
Wakuu njooni mumchukue coutinho hata bure hali yenu ni mbaya sana msimu huu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
bodi inasajili wachezaji iwatakao tunamtaka seri+inigo tunaletewa paunyoko. bora tushuke daraja tuuu kwa ungese huu tucheze segunda division
 
bodi inasajili wachezaji iwatakao tunamtaka seri+inigo tunaletewa paunyoko. bora tushuke daraja tuuu kwa ungese huu tucheze segunda division
Hahaaaa imebidi nicheke kwanza maana mm nina hasira lkn ww kiboko mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…