FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Huyu mwenye masikio Kama popo w nini?messi nadhani anatuharibia timu sasa kwa kutuchagulia wachezaji,naye asepe,nakumbuka alisababisha IBRA aondoke,villa aondoke,henry naye aondoke,its time to let go of him

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe acha upotoshaji Messi sio technical director wala nani i doubt about upenzi wako na Barca una matango pori mengi sana
Transfer ya Lamasia graduate wanaohusika ni management
 

Jamaa hadi anastaafu hamna mtu amewahi kumfunga hatrick
From the dream/golden team
 
Hiki Ndio kipindi murua kuwatambua wale mashabiki waliovamia Barca kwa mbio za mwenge na wale mashabiki kindakindaki

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Tukimpata Draxler itakua tumefanya jambo la mbolea sana, jamaa anajua sana. Hiyo hela tunayotaka tumnunue coutinho waliokataa mi naona tusiongeze tumchukue tu Saul Niguez wa athletic madrid.
 
Uchambuzi maridadi kabisa kutoka kwa mchambuzi mahiri anayefahamu kwa ndani historia ya chanzo na anguko la ufalme wa Barcelona katika Bara la Ulaya na dunia nzima...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
La Masia Vs Football market!


Ile Barcelona iliyomtetemesha mzee Alex Ferguson kwenye fainali ya UEFA pale Wembley haikuandaliwa kwa miaka miwili.

Yule Xavi Hernandez aliyeweza kupiga pasi nyingi kuliko jumla ya pasi za timu pinzani hakuandaliwa kwa miaka miwili.

Hata yule Andres Iniesta aliyepewa heshima na washabiki wa Los Blancos pale Santiago Bernabeu hakuandaliwa kwa misimu mitatu!

Yalikua maandalizi ya miaka na miaka. Barcelona walikubali kukaa kinyonge kwa miaka kadhaa huku wakiandaa kikosi Bora kabisa kupata kutokea kwenye historia ya soka!

Lakini zama zinabadilika. Tuko kwenye kipindi ambacho ushindani wa soka la kibiashara hauruhusu eti timu ijipange kwa miaka kadhaa kutengeneza kikosi.

Tuko kwenye kipindi ambacho team ikiyumba kwa msimu mmoja tu, mashabiki, kocha mpaka uongozi wa timu unakua kwenye wakati mgumu!
Ndio maana Barcelona wamejikuta wakiachana na utamaduni wao ili kuendana na hali.

Wanachopitia Barcelona sasa hivi ni kipindi cha mpito, ambacho kitawahitaji kuandaa kikosi kitakachowarudishia heshima yao kwenye soka!

Swali ni je, Barcelona wako tayari kuhangaika kwa miaka zaidi ya mitatu au minne kuandaa kikosi kutoka kwenye academy ya La masia? Au wataendelea kupambana na ushindani kwa kununua wachezaji ili kulinda heshima yao? Sina majibu, ila naamini kitu kimoja;

BARCELONA ITASIMAMA TENA!

- KANA -
 
well said...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukimpata Draxler itakua tumefanya jambo la mbolea sana, jamaa anajua sana. Hiyo hela tunayotaka tumnunue coutinho waliokataa mi naona tusiongeze tumchukue tu Saul Niguez wa athletic madrid.
Kumpata Saul ni ndoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…