FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Kwanini wasifanye utaratibu kwamba Barca ibaki kwenye league palepale?
Hii kura na ikitokea catalunya wamejitenga itakuwa mbaya sana kwa laliga maan basque nao waliitisha kura kama hii mwaka 2008 ikashindwa mahakamani. Huko ndiko kulikuwa na wale waasi wa ETA. Hawa wakiona katalunya wamefanikiwa nao watalianzisha. Kwahiyo huku zitatoka Barca, espanyol na Girona. Kule basque kuna bilbao, sociedad. Alaves na eibar. Timu 7 hizo. Zitaharibu kabisa ligi. Naombea hao wanaotaka kujitenga washindwe kabisa. jackline 1 tupe nini itakuwa hatma ya Barca huko. Timu yetu pendwa inaweza kufa kiutaniutani hivihivi.
 
Haya mambo kama Zanzibar,ukiruhusu kura ya kujitoa Wazanzibar watajitoa katika muungano halikhadalika huku hivyo hivyo kura itasababisha wajiondoe- kwa foreigners tunashangaa whats the fuss lakini wenyewe wanataka kujiondoa.Mimi naona serikali ikomae tuu kama ilivyofanya Basqueland-there is too much to lose
 
Their political confricts is not our business, lakini ningefurahi kuona Barca ikiendelea kucheza la liga hata kama ikitokea Cataluña imejitenga.
Ni kweli, lakini spain siasa zimeingia sana na kuathiri mpira na timu.
Their political conflicts is not our business, lakini ningefurahi kuona Barca ikiendelea kucheza la liga hata kama ikitokea Cataluña imejitenga.
Ni kweli, kweli ila tatizo siasa zao zimeingia sana na kuathiri mpira na timu yetu pendwa. Ngumu kutenganisha siasa na mpira huko spain, hasa kwa Barca na Bilbao. Ona juzi tumecheza bila mashabiki. Somehow inakuwa our business.
 
Kuna msemo kuwa taasisi ni tofuti na mwanadamu, kwamba mwanadamu akifa na habari yake huishia hapo lkn taasisi akitoka mtu mtu anaingia mtu kuendeleza alipoachia alietoka. Lkn kwa issue ya uhai wa Barca ninamashaka na uhai wake. Hii inaanzia tangu pale uongozi ulipopishana na Johan Cryff akabeba bag yake kurudi nyumbani Netherlands. Baada ya pale ukiangalia uhai wa Barca unapata mashaka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…