La Liga: Barca kubeba ubingwa siku ya mwisho ya ligi kwa mara 10
Katika makombe 23 waliyoshinda FC Barcelona ya La Liga, tisa kati ya hayo walishinda siku ya mwisho ya ligi. Jumamosi wiki hii, wanaweza kushinda kombe lao la 10 katika siku ya mwisho ya ligi. Karibia nusu ya idadi ya makombe ya La Liga waliyobeba iliwabidi kupambana mpaka siku ya mwisho…..
Msimu wa 1928-29
Barca na Real Madrid walimaliza msimu wa kwanza wa ligi wakiwa wamefungana pointi (23), lakini Barca wakawa na mchezo mmoja wa ziada dhidi ya Arenas de Getxo na hawakufeli. Walishinda 0-2 na kutwaa ubingwa.
Msimu wa 1947-48
Barcelona na Valencia walifika mpaka siku ya mwisho ya ligi wakiwa na pointi sawa – pointi 34. Mchezo wa mwisho Barca wakashinda dhidi ya Athletic (3-0). Valencia wakafungwa 5-2 na Celta Vigo.
Msimu wa 1948-49
Barca walikuwa wakiongoza kwa pointi 2 mbele ua Real Madrid na Madrid waliokuwa na pointi 35 na 33, lakini kama angefungwa kwenye mchezo wa mwisho. Hata hivyo Wakatalunya wakaenda kushinda 2-1 dhidi ya Espanyol, wakashinda ligi kwa tofauti ya pointi 2.
Msimu wa 1952-53
Siku ya mwisho nyingine katika uwanja wa Les Corts. Kikosi cha Barca kilifika mpaka siku ya mwisho kikiwa na pointi 40 sawa na Valencia. Mchezo wa mwisho wakawafunga Athletic 3-2. Valencia wakapoteza. Mwishowe Barcelona wakashinda ligi kwa tofauti ya pointi 2.
Msimu wa 1959-60
kikosi cha Herrera cha Barca kiliwafunga Real Zaragoza (5-0) katika uwanja wa Camp Nou na wakashinda ligi kwa tofauti ya magoli dhidi ya RealMadrid, baada ya kulingana kila kitu. Wote walimaliza na pointi 46.
Msimu wa 1991-92
Barca walihitaji ushindi dhidi ya Athletic pale Camp Nou na wakfanikiwa kushinda 2-0, na Madrid wakafungwa na Tenerife, John Cruyff akashinda ubingwa akiwa na pointi 55 dhidi ya 54 za Madrid.
Msimu wa 1992-93
Kilichotokea msimu uliopita ndicho kilichotokea kutoka safari hii. Barca walihitaji ushindi dhidi ya Real Sociedad at Camp Nou katika siku ya mwisho ya ligi, wakashinda 1-0 na Madrid wakafungwa huko Tenerife. Barca wakashinda ubingwa kwa pointi 58 dhidi ya 57 za RealMadrid.
Msimu wa 1993-94
Barca wakiwa chini ya Cruyff walishinda ubingwa kwa mara nyingine tena siku ya mwisho. Iliwabidi kushinda dhidi ya Sevilla pale Camp Nou na wakashinda 5-2 na wakawa wanaomba Depertivo washindwe uwanjani kwao Riazor dhidi ya Valencia – wakatoka sare ya 0-0.
Msimu wa 2009-10
Barcelona na Madrid, kama ilivyo msimu huu, ilibidi wapambane mpaka siku ya mwisho ya ligi. Siku ya mwisho Barca wakafanikiwa kuifunga Vallodolid 4-0, wakati Madrid wakafeli kushinda. Barca akabeba ubingwa kwa pointi 99 dhidi ya 96 za Madrid.