FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

naona karata kubwa ipo kwa Jorge Sampaoli wa Sevilla. jamaa ni bonge la tactician. jamaa ana historia nzuri sana. Eusebio ni mzuri lakini walimtimua sababu barca B ilikua inazingua. sampaoli ni moja ya makocha bora kwa sasa
Kumbuka Eusebio aliipandisha Barca B ligi kuu lakini sababu ya sheria Cordoba wakachukua nafasi hiyo na baada ya hapo vijana wengi wakaondoka Denis Suarez, Munir nk na hivyo Barca b haiko stable na ukizingatia alikuwa daraja la kwanza. ..jamaa anafanya kazi nzuri sociedad na saizi wanashindana na atletico nafasi ya 4

Candidates waliotajwa ni sampaoli ,eusebio ,valverde ,lakini sioni kama sampaoli ataondoka sevilla hivi sasa

Endapo Luis Enrique asipo ongeza mkataba namuona kabisa eusebio anatua..sampaoli ana fit nafasi ila probability kumpata
 
DNA ya Barcelona ni high pressing ,Guardiola aliijenga Barca kwa misingi ya Cruyff timu ikipoteza pass ndani ya Sekunde inarudi kwenye himaya ,Barca inaundwa na viungo 3 na siyo washambuliaji

Barca hii haifanyi pressing ,midfield ipo slow ,na Barca hii ikikutana na timu inayo press inapata tabu sana refer game ya Betis,sociedad anoeta,ATM sec leg,nk

Viungo wanazingua haswa Rakitic footwork yake mbovu ,Gomes sijui kakumbwa na nini huyu..

Endapo Luis Enrique asipo saini

Basi Eusebio Sacristan kocha wa Sociedad ana nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ,kwanza ni mwanafunzi wa Cruyff, amekaa Barca muda mrefu ,falsafa yake ni pressing sana,na tiki taka kaibadilisha sana real sociedad na malegends wanampigia chapuo ..mie naona sacristan anafaa kuchukua post na ana nafasi kubwa ..koe man ,sampaoli sidhani

Barca hii miyeyusho sana na Enrique ni chanzo timu inacheza pass nyingi backline kuliko kwenye kiungo huku akitegemea MSN

PSG wakifanya pressing nou camp Barca hatoki ,kiungo cha Barca haiwezi kuhimili pressing
Maestro Xavi hayupo tena hata Guardiola akirudi hamna kipya hapo
 
Barca inapaswa kujengwa upya hasa kwenye midfield,Lucho ameitengeneza timu kwenye foward (Messi,Suarez,Neymar) tofauti na utamaduni wa Barca.Iniesta anahitaji mrithi Batromeu/Rosell walifanya kosa kubwa sana kumuachia Thiago na kutomsajili Kroos ni ngumu sana kupata viungo wanaofit kwenye mfumo wa Barca kwa sasa Verrati,Herrera,Thiago,Weigl wanafaa kutengeneza safu mpya ya kiungo
 
  • Thanks
Reactions: GUI
kocha amekua kama Mourinho kipindi kile chelsea hana first eleven hadi leo Enrique this season sasa unaliingiza lile Robot Andres Gomes na kumuacha Rakitic halafu tunaruhusu adui awe na mpira na kuruhusu mipira ya kupenya mingi kweli?huyu S Roberto hadi leo kwanini uwe na imani nae wakati umemjaribia sana hii namba haiwezi kuicheza hii ni sawa?tumefungwa kwa sababu za kiufundi yaani ni kocha
Huyu kocha ni bure kabisa, nilishindwa kuelewa imekuaje kumuingiza Gomez na Iniesta? Mimi ninaona kabisa hata Iniesta hastahili kuanza kikosi cha kwanza.

Viungo vinapaswa vichezwe na Busquet, Rakitic na Arda. Yaani sijui kwanini mpaka sasa hatuna kiungo mchezeshaji kama Fabregas.
 
we need team transformation lucho tunakupenda sana lakini naona tunaelekea tamati ,team tangu msimu umeanza haina harmony ya ku press mipira iinstead individual talents ndio zinatumika kuna haja ya Pap arudin aje astaafie pale
Ukiachana na ubaguzi Pep, jamaa ni mwalimu mzuri sana wa mpira.
 
Ila mkuu si Rakitic aliingia na magoli yake mawili Barca leo wamezidiwa na ile chance aliyopoteza yule dogo anacheza namba mbili si bora Alves angepewa tu mkataba mwingine
Ndo maana Dani Alves kailalamikia Board kwa kukataa kumuongezea mkataba, tumemuacha jamaa kipindi ambacho tulikuwa tunamhitaji.

Sergio amejitahidi kwa sehemu yake ila Sergio sio beki, tukumbuke hilo. Hii Game ya PSG Dani Alves angekuwepo asingeruhusu wale wajinga akina Draxler wapite wanavyotaka, Sergio na Umtiti wanaogopa kuchukua kadi.
 
Kwa kweli Wakuu mwaka huu tunaweza ambalia Copa Del Ray tu. Timu haina kiungo mchezeshaji wala mshambuliaji, nasema haina mshambuliaji sababu Iniesta mpira nae unaanza kwenda kushoto. Kiungo mchezeshaji wa timu mpaka sasa hajulikani na sioni dalili zozote za kumpata. Pale katikati Sergio Busquet anabaki kubeba mzigo tu. Game ya PSG tumeyaona kabisa madhaifu yetu ila mimi lawama natupa kwa kocha na kwa wachezaji hususani Gomes, Roberto na Umtiti, hawa vijana ni wapuuzi sana yaani wanapitwa kizembe mno, wanashindwa hata kuomba Kadi ya Njano. Angekuwepo Mascherano na Alves sidhani kama tungewaona PSG wakizichezea beki na viungo watakavyo.
 
Alex vidal angekuwepo angecheza nafasi ya Se robert halafu robert angeche midifielder lkn no way luis enrique out. Hv mnajua kama luis enrique anabebwa na wachezaji?
 
Kaka kuwa mpole Madrid inashinda March hii
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] zimebak dakika 10 mechi kuisha na mmoroco anarukaruka

MKUU FANYA KAZI NYINGINE MSHAPOTEZA
 
Tigo wamewaponza Madrid eti halichachi ndo usipashe moto muulize Madrid ka kimelika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
HIVI KWANINI HUYU KOCHA ASIPANDISHE.VIJANA KAMA HAWA

TYAR BARCA B IMESHAINGIA NUSU FINAL UEFA

 
Back
Top Bottom