Long time no see cules!
Naiona project mpya hapo camp Nou, inaleta matumaini. Eric Garcia, Ronald Araujo, Oscar Mingueza, Sergino Dest pamoja na Emmerson, wanaweza kua solution kwa matatizo ya defence tuliyokua nayo.
Upande wa midfield, Frankie De jong anazidi kukomaa na Pedri Gonzalez anazidi kuimarika. Upande mwingine, Professor Ricard Puig na Trincao, bado ni promising young talents japo hawapati muda wa kucheza.
Kule mbele, naona Dembele ameanza kuamka japo majeruhi bado ni tishio kwake. The whole universe knows who Ansu Fati is, tunamuombea quick recovery. Alaix Moriba pia hayuko nyuma, he's showing much potential in the future.
Mpaka kufikia hapo, hiyo list imekosa mtu mmoja pekee, "world class striker". Tukimpata huyo, nadhani resources za project zitakua zimekamilika. Kazi itabaki kwa mwalimu kuwaamini vijana na kuwapa nafasi.
Kazi itatabaki kwa viongozi wa timu na mashabiki kutulia na kukipa muda kikosi kiimarike. Tumezoea ushindi na mataji, ndio maana presha inakua kubwa sana kwa team sababu ya expectations. Hata hizi sajili za akina Aguero ni presha tu ya kutaka mafanikio ya haraka.
Mi nadhani next season, Busquets awe mtu wa kupumzika, Alba amekiwasha sana msimu huu, ila anahitaji kuwapa nafasi vijana. Nadhani wazee pekee wa kuanza wawe Messi, Griezman na Stergen.hawa wengine wawe substitutes tu. Huwezi kujenga kikosi kipya ikiwa bado unawategemea na kuwapa nafasi zaidi wachezaji wa zamani.
Haya yakifanyika, tunaweza tusishinde vikombe, ila kufikia mwisho wa msimu tutakua tumejenga kikosi cha kupambana Ulaya.
Swali linabaki, does Koeman has what it takes to see this project through?
Adios Amigos!